2007 KCSE KISWAHILI MOCK BUNGOMA PAST PAPER 3
![]()
FREE 2007 KISWAHILI MOCK BUNGOMA PAST PAPER 3
FREE 2007 KISWAHILI MOCK BUNGOMA PAST PAPER 3
102/3 KISWAHILI KARATASI YA TATU FASIHI JULY / AUGUST 2007 MUDA: SAA MBILI NA NUSU
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUNGOMA 2007 HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA (K C S E)
102/3 KISWAHILI KARATASI YA TATU JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO * Jibu maswali manne pekee, swali la kwanza ni la lazima * Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki (Tamthilia, riwaya, hadithi fupi na Fasihi simulizi * Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
Karatasi hii ina kurasa nne zilizopigwa chapa Mtahiniwa ahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo 1 Soma shairi hili kisha ujibu mawali yanayofuata SABUNI YA ROHO Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia? Ndiwe suluhu la zama, waja wakukimbilia, Waja wanakutazama, madeni wakalipia, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani, Utanunua majoho, majumba na nyumbani, Umezitakasa roho, umekuwa mhisani, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
Matajiri wakujua, wema wako wameonja, Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja, Sura Zao 'mefufua, Wanazuru kila nyanja, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
Ndiwe mvunja mlima, onana na masikini Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni Wabebe waliokwama, wainue walio chini, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
Ndiwe mvunja mlima,wapi kapata uwezo? Umezua uhasama, waja kupata mizozo, Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwazo, Ndiwe sabuni ya roho, Ndiwe mvunja mlima
Umevunja usuhuba, familia zazozana, Walokuwa mahabuba, kila mara wagombana, Roho zao umekaba, majumbani wachinjana, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu, Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu, Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika, Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
( a) Mshairi anaongea na nani katika shairi hili? [alama 1]
( b) Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa [alama 3]
( c) Anayezungumziwa katika shairi hili amesababisha balaa gani? [alama 2]
( d) Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe? [alama 4]
( e) Fafanua maudhui ya ubeti wa sita [alama 2]
( f) Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake
Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi [alama 3]
( g) Fafanua maana ya:
Sura zao "mefufua, wanazuru kila nyanja [alama 1]
( h) Andika ubeti wa saba katika lugha nathari [ alama 4]
TAMTHLIA KITHAKA WA MBERIA:Kifo Kisimani
2 'Kazi ya mikono yangu yenyewe: nimechoma mwiba tayari Kisu kilipata
( a) Fafanua muktadha wa dondoo hili [alama4]
( b) Ni mambo gani yaliyosababisha kuzuka kwa 'Mwiba' Unaotajwa katika
dondoo hili [alama 4]
( c) Kwa kutumia mifano mitatu, dhihirisha jinsi wanawake walivyochangia
katika ukombozi wa Butangi [alama5]
( d) Eleza hatima ya msemaji wa maneno haya [alama 7]
RIWAYA Z Burhani:MWISHO WA KOSA: Jibu swali 3 au 4 3 " Mbio za sakafuni huishia ukingoni " Thibitisha ukweli wa madai haya kwa kurejelea wahusika watano kutoka katika riwaya ya 'Mwisho wa kosa ' [alama 20]
4 "
( a) Fafanua muktadha wa dondoo hili [alama 4]
( b) Kauli hii ilikuwa na athari zipi kwa msemaji na wasemewa? [alama 4]
( c) Dondoo hili linadhihirisha migongano iliyoko kati ya wale wenye fikra
za kisasa na wanaodaiwa kuwa na fikra za kipuuzi na za kizamani Fafanua
visa vine vinavyotoa ithibati ya madai haya [alama 12]
HADITHI FUPI K W Wamitula: Mayai waziri wa maradhi Jibu swali 5 au la 6
Mayai waziri wa maradhi 5 [
( a) Ni kweli kuwa picha hizi zinatoa muhtasari wa maisha ya mayai waziri
wa maradhi
Taja picha zingine alizozitazama huku ukieleza sababu za kuzipenda au
kuzichukia
(Alama 10)
( b) Hadithi ya mayai waziri wa maradhi inaangazia matatizo yanayozikabili
nchi za kiafrika Thibitisha kauli hii kufafanua matatizo yoyote matano
(Alama 10)
6 Uteuzi wa moyoni Fafanua changamoto zinazomkabili mwanamke katika hadithi ya 'uteuzi wa moyoni' [alama 20]
FASIHI SIMULIZI
7
( a)
(i)Ngano ni nini? [alama 1]
(ii) Eleza tofauti iliyoko kati ya visasili na visakale [alama 4]
(iii) Fafanua majukumu yoyote muhimu ya ngano katika jamii [alama 5]
( b)
(i) Eleza umuhimu wa vitendawili katika jamii [Alama 3]
(ii) Tega na utegue vitendawili vyovyote viwili vilivyo na lugha ya
takriri na lugha ya mlio [alama 2]
(iii) Taja sifa zozote tatu za methali [alama 3]
(iv) Taja methali yoyote iliyo na lugha ya balagha kisha ueleze maana
yake ya ndani
[alama 2]
2007 KISWAHILI MOCK BUNGOMA PAST PAPER 3
