KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kusikiliza na Kuzungumza - Kiswahili Kidato Cha 1Shughuli

Katika sehemu hii, utapata maelezo zaidi juu ya somo husika. Bonyeza mada yoyote kati ya zilizoorodheshwa ili ufaidi!
 


Matumizi ya lugha katika muktadha
Mojawapo ya sifa zinazotawala matumizi ya lugha katika jamii ni muktadha
lugha inatumika,wahusika na uhusiano wao pamoja na lengo la mawasiliano. 

Zoezi

Katika sehemu hii unatakiwa kubonyeza mazoezi yaliyoorodheshwa ili uweze kujipima iwapo umeyapata yaliyofunzwa katika somo hili. Vilevile unaweza kuupima uelewaji wako wa mada hata kabla hujashughulikia mafunzo ili uweze kujua unayopaswa kutilia mkazo zaidi.

Matumizi ya Lugha Shuleni
Hebu tuone vile muktadha wa shuleni unavyotawala matumizi ya lugha.Tazama na usikilize video ya mazungumzo kati ya mwalimu wa zamu na wanafunzi shuleni.Zingatia matumizi ya lugha katika muktadha huu halafu ujibu maswali yanayofuata.
 

Hitimisho
Imedhihirika ya kwamba lugha katika muktadha fulani hutawaliwa na lengo linalotokana na haja au shughuli inayoendeshwa katika muktadha huo,wahusika,uhusiano kati yao na umri wao.

Matumizi ya Lugha Mtaani
Tazama na usikilize video ya mazungumzo kati ya vijana mtaani.
Chunguza matumizi ya lugha katika muktadha huu halafu ujibu maswali yanayofuataUTANGULIZI
Andika maana zaidi ya moja ya maneno yafuatayo:-

 1. Barabara
 2. Ila

Provide space for learner to type in

Majibu

 1. Barabara Njia kuu

-Sawasawa / shwari / sawa
  2. Ila    -     kasoro / dosari
    -     isipokuwa   

 1. Provide positive reinforcement for correct answers vizuri sana and encouragement for incorrect answers jaribu tena.
 2. Allow learner to try twice then give correct answer

Shadda
Maana mbalimbali za maneno 'barabara' na 'ila' zinatokana na kile tunachokiita shadda. Shadda ni mkazo unaowekwa kwenye silabi fulani za neno wakati wa kutamka ili kutoa maana inayolengwa na mzungumzaji.Mathalani,tulipoweka mkazo silabi ya pili ya neno bara'bara,tulipata maana yake ni sawasawa, shwari au sawa.
Tunapotamka neno lilo hilo, yaani '
barabara' bila kuweka mkazo wowote, maana yake inabadilika na kuwa njia kuu au baraste. Kama tulivyofanya katika neno barabara,tunaweza kuweka mkazo tunapotamka neno ila na kupata maana mbili tofauti.
Tunatambua kuwa tukiweka shadda baada ya silabi ya kwanza kama vile
i'la, maana inayolengwa ni dosari au kasoro au udhaifu.Hata hivyo,tukitamka neno lilo hilo bila kuweka mkazo wowote,maana inakuwa Isipokuwa au lakini.
 


Tanbihi
Ikumbukwe kuwa shadda na kiimbo hutawaliwa zaidi na alama hisi (!), kiulizi (?)na kikomo / kitone (.) katika maandishi.Bila shaka,tumetambua kuwa sentensi tuliyotamka ni ile ile. Hata hivyo, sentensi hiyo hiyo inaweza kutamkwa kwa namna mbalimbali na kuwasilisha ujumbe tofauti.Tunapoongea, sauti huweza kupanda na kushuka kutegemea lengo la mawasiliano. Kupanda na kushuka kwa sauti husababisha kuwepo kwa mkazo ambao hudhihirisha maana inayodhamiriwa na mzungumzaji. Mathalani, huenda msemaji angetaka:Kuarifu au kutoa kauli ya taarifa Kwa mfano, Nilifunguliwa lango.
Kuamrisha;Kwa mfano, Fungua lango!
Kutoa rai au ombi. Kwa mfano, Nifungulie lango.
Kuuliza Kwa mfano; Nifungue lango?
Kuonyesha hisia kama vile kushangaa, kubeza au kudharau.
Kwa mfano; Umefungua lango!

1. Kuarifu au kutoa kauli ya taarifa:Kwa mfano, Nilifunguliwa lango.

2. Kuamrisha; Kwa mfano, Fungua lango!

3. Kutoa rai au ombi. Kwa mfano, Nifungulie lango.
4. Kuuliza Kwa mfano;Nifungue lango?5.Kuonyesha hisia kama vile kushangaa, kubeza au kudharau.; Kwa mfano; Umefungua lango!
Maana ya Kiimbo
Ukirejelea sentensi ya Anakula nyoka maana tatu zinajitokeza kutegemea kupanda na kushuka kwa sauti (kiimbo) wakati wa kuzungumza kwa mfano.
Anakula nyoka. Hii ni kauli ya taarifa. Mtu anafahamishwa ujumbe.
Anakula nyoka!- Hii yaonyesha hisia labda za kushangaa. Mtu anashangaa kwa kusikia ujumbe huo na anarudia kwa njia inayoonyesha hisia za kushangaa.
Anakula nyoka? -Hii ina maana kuwa swali limeulizwa. Yawezekana mtu ameona kana kwamba mwingine anakula hicho kinacholiwa, lakini hana uhakika na ndipo anauliza ili apate uhakika.

Umuhimu wa Shadda na Kiimbo

Tumeweza kutambua kuwa shadda hutokeza kwenye silabi katika neno tunapotamka.
Kiimbo nacho hutokeza katika sentensi tunapozungumza.Hizi ndizo tofauti za kipekee kati ya Shadda na Kiimbo.
Shadda na kiimbo ni hali mbili za kimatamshi ambazo ni muhimu sana katika mazungumzo.Kutokana na shadda, maana inayodhamiriwa katika neno hujitokeza.Vivyo hivyo, ni kutokana na kiimbo ndipo tunaweza kubainisha anacholenga kuwasilisha mzungumzaji katika sentensi.


Vitate na Vitanza NdimiUmemudu? Jiburudishe na uboreshe matamshi yako.

vitateMaana ya Vitate

Maneno yanayokaribiana kimatamshi lakini maana zake ni tofauti  kama tulivyoona  hapo awali huitwa VITATE.

Kwa mfano
Zana ;sana,
Tosha ; tosa/toza.

Vitanza Ndimi
Hebu; Sikiliza vitanza ndimi vifuatavyo vikitamkwa kisha uvitamke kwa usahihi na kwa muda uliopewa.
Viatu vile vitatu ni vya watu watatu waliotatua hali tata kwetu Jumatatu. (Tamka kwa sekunde 5)
Mamluki amerukia milki ya malkia na mali ya Miriamu.
(Tamka kwa sekunde 5)
Wanawali wa Awali hawali wali wa awali ila wali wao.(Tamka kwa sekunde 5)
Ali hali kwa kila hali maana hana hali.
(Tamka kwa sekunde 3)
Matata yenye utata unaotatiza ya dadake Tata yalitatuliwa na dadake Tatu. (Tamka kwa sekunde 5)

Maana ya Vitanza Ndimi

Bila shaka, umekabiliana na changamoto katika kutamka sentensi

ulizopewa hasa kwa muda uliotolewa. Sentensi hizi ni mifano

ya vitanza ndimi.

Hili ni fungu la maneno yanayotatanisha wakati wa kuyatamka

kwa sababu ya kuwepo kwa sauti zinazokaribiana kimatamshi.
Aghalabu watu wengi hukwama wanapojaribu kutamka vitanza
ndimi na wengine hushindwa kuvitamka.

ZOEZI 3
1.Hebu; Sikiliza vitanza ndimi vifuatavyo vikitamkwa kisha uvitamke kwa usahihi na kwa muda uliopewa.
Provide the following in sound. Get a person who can pronounce the given Kiswahili tongue twisters correctly and within the shortest time possible.

  Viatu vile vitatu ni vya watu watatu waliotatua hali tata kwetu Jumatatu (Tamka kwa sekunde 5)
  Mamluki amerukia milki ya malkia na mali ya Miriamu (Tamka kwa sekunde 5)
  Wanawali wa Awali hawali wali wa awali ila wali wao(Tamka kwa sekunde 5)
  Ali hali kwa kila hali maana hana hali (Tamka kwa sekunde 3)
  Matata yenye utata unaotatitiza  ya dadake Tata yalitatuliwa na dadake Tatu (Tamka kwa sekunde 5)

 

2. Hebu Vitamke vitanza ndimi vifuatavyo  kwa usahihi na kwa muda uliopewa.
(Let the learners  pronounce the tongue twisters within the given time. Then provide the right pronounciation in sound by getting a person who can pronounce the given Kiswahili tongue twisters correctly and within the shortest time possible. The learner can gauge their pronounciation)

   Kadogo mdogo alifinyanga udongo wa kutengeneza vyungu vidogo (Tamka kwa sekunde 3)
   Kuku wako na vikuku vyako haviko huko kwake viko kwako (Tamka kwa sekunde 3)
   Lori lile la Lari lenye rangi limeregea rege rege. (Tamka kwa sekunde 3)
   Mto ule umefura furifuri na kuwafurusha watu wenye safura. (Tamka kwa sekunde 4)


Hebu Vitamke vitanza ndimi vifuatavyo kwa usahihi na kwa muda uliopewa.
Kadogo mdogo alifinyanga udongo wa kutengeneza vyungu vidogo. (Tamka kwa sekunde 3)
Kuku wako na vikuku vyako haviko huko kwake viko kwako. (Tamka kwa sekunde 3)
Lori lile la Lari lenye rangi limeregea rege rege. (Tamka kwa sekunde 3)
Mto ule umefura furifuri na kuwafurusha watu wenye safura. (Tamka kwa sekunde 4)

Umuhimu wa Vitanza Ndimi
Vitanza ndimi vina umuhimu mkubwa hasa katika jamii kama ifuatavyo;
Huwafunza na kuwazoesha wanajamii kuwa na matamshi bora na hivyo kuimarisha matamshi.
Hujenga uwezo na ukakamavu wa kuongea au kuzungumza bila kutatizika.
Hufikirisha hasa ndipo mtu aelewe maana ya anachokisema.
Hukuza uwezo wa ubunifu.
Hunoa bongo za wanajamii ambao baadaye wanaweza kuwa walumbi.
Huburudisha wanajamii.
Hujenga stadi ya umakinifu katika kusikiliza.
Maana ya Methali

Methali ni semi fupi za kimapokeo zinazotueleza kwa muhtasari

fikira au mawazo mazito yanayotokana na uzoefu na tajriba ya

jamii .
Methali huwasilisha ujumbe wake kwa matumizi ya lugha

ya mafumbo na inayojenga picha akilini mwa mwanadamu.


Zoezi 1
Onyesha kipande cha kwanza na kipande cha pili katika methali zifuatazo kwa kutumia alama ya mkwaju

 1. Vita havina macho
 2. Chovya chovya humaliza buyu la asali
 3. Kuteleza si kuanguka
 4. Chururu si ndo ndo ndo
 5. Ngoja ngoja huumiza matumbo
 6. Mwenye macho haambiwa tazama

Majibu

 1. Vita / havina macho
 2. Chovya chovya / humaliza buyu la asali
 3. Kuteleza / si kuanguka
 4. Chururu / si ndo ndo ndo
 5. Ngoja ngoja / huumiza matumbo
 6. Mwenye macho / haambiwa tazama
The blue stroke indicates the division required. Provide positive reinforcement for correct answers vyema / vizuri and an encouragement for wrong answers jaribu tena

Sifa za Methali
Methali ni mojawapo ya vipera vya semi katika fasihi simulizi
Methali huwa na sifa zifuatazo;-
1. Huwa maneno machache yanayoweza kukumbukwa kwa urahisi. Kwa mfano: heshima si utumwa,Mwerevu hajinyoi
2. Mara nyingi huwa na vipande viwili kwa mfano,
Kipande cha kwanza................. Kipande cha pili
Mwangaza mbili..........................Moja humponyoka
Asiyekubali kushindwa................. Si mshindani
Mchumia juani............................. Hulia kivulini
3. Sifa nyingine ya methali ni kuwa hutumia picha au istiari. Istiari ni ulinganishi uliofichika ambapo maneno ya kulinganisha kama vile mithili ya, mfano wa na kadhalika hayatumiki.
Hebu tazama picha zifuatazo

Mpanda ngazi hushuka


Mtaka cha mvunguni sharti ainameUjana ni moshi ukienda haurudiDalili ya mvua ni mawingu

Kila ndege huruka kwa bawa zake


5. Methali nyingi hujengwa kwa kutia chuku au kutia chumvi.Kwa mfano

 1. Polepole ya kobe humfikisha mbali


Ulimi ni upanga


Mfinyanzi hulia gaeni
Chovya chovya humaliza buyu la asali


Maji ya kifuu bahari ya chungu


6. Aghalabu kipande cha kwanza kinaweza kikapingana na kipande cha pili. Kwa mfano:-
Kipande cha kwanza..............................Kipande cha pili
Haraka haraka ............................ haina baraka
Amani haiji ................................ ila kwa ncha ya upanga
Mtaka yote ................................ hukosa yote
Mwenye shibe ............................ hamjui mwenye njaa
Kulenga..................................... si kufuma

 

Umuhimu wa methali
Mbali na sifa zake methali pia zina umuhimu wake katika jamii. Kwa mfano:-
1. Kueleza na kutahadharisha jamii kwa mfano,Asiyeskia la mkuu huvunjika guu2. Kuadilisha jamii kwa mfano, Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu3.Kufahamisha juu ya utamaduni, historia na mazingira ya watu, kwa mfano, Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani4.Kupevusha akili, kwa mfano,Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonoweOrder this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu