KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kusoma - Kiswahili Kidato Cha 1

Maudhui
Katika baadhi ya mashairi ujumbe, maudhui au habari wa mtunzi hujitokeza wazi lakini katika mashairi mengine ujumbe umejificha. Kwa mfano shairi hili ujumbe umejitokeza waziwazi kama vile watoto kuajiriwa, kunyimwa haki zao na kunyanyaswa.

 1. This is true or false exercise
Give positive reinforcement for the correct answer such as vizuri sana and encouragent for the wrong answer such as jaribu tena

MAZUNGUMZO KULINGANA NA MUKTADHA

Lugha utakayoitumia shuleni ni tofauti sana na utakayoitumia

hotelini na hata unapozungumza na marafiki wakati wa likizo.

Ukweli ni kwamba matumizi ya lugha hutegemea muktadha.

Somo hili litakusaidia kuainisha miktadha tofauti na lugha

inavyotumika humo.

USHAIRI
Akili By Mathias Mnyampala

Mpima jambo la mbele, huyo anayo akili,

Mpima hili na lile, hakosi mtu adili,

Hasa mtu kama yule, sifa anastahili,

Mtu hapati akili, ila mpima ya mbele.


Zoezi 3

Onyesha ni kweli ama si kweli kuhusu sentensi zifuatazo.

 1. Shairi hili lina kibwagizo  (kweli / si kweli)
 2. Kudhulumiwa kwa watoto kunajitokeza katika shairi (kweli / si kweli)
 3. hali ya umaskini haijashughulikiwa kamwe katika shairi hili (kweli / si kweli)
 4. Kila ubeti katika shairi hili una mishororo mine (kweli / si kweli)
 5. Vina vyote katika shairi hili vinafanana (kweli / si kweli)

Majibu

 1. Kweli
 2. kweli
 3. si kweli
 4. kweli
 5. Si kweli

Zoezi 2
Oanisha maneno yafuatayo na vifupisho vinavyoonyesha ni maneno ya aina gani kwa kutumia mishale.
k.m Ruka (T)

 1. This is a matching exercise by use of arrows.
 2. Provide response for correct matching as vizuri sana and jaribu tena for encouraging incorrect matching
 3.  Make provision for a scanned page from Kamusi showing short forms
 1. Ala!    (N)
 2. Wewe    (T)
 3. Sana      (V)
 4. Kiko      (E)
 5. Na      (W)
 6. Pika    (U)
 7. Mrembo   (I)

Majibu
The correct matching answer is

 1. Ala!    (I)
 2. Wewe    (W)
 3. Sana      (E)
 4. Kiko      (N)
 5. Na      (U)
 6. Pika    (T)
 7. Mrembo   (V)

SHABAHA
Kufikia mwisho wa somo hili uweze

 • Kutaja na kueleza baadhi ya sheria katika  mashairi ya arudhi.
 • Kueleza ujumbe wa mtunzi wa shairi.


Maana ya Shairi
Kutokana na zoezi ulilofanya umeona kuwa shairi ni mtungo wa kisanaa wenye mpangilio maalumu kwa lugha ya mkato.
Asili ya shairi ni nyimbo.
Zamani watu walikuwa wakiimba nyimbo za:-

 1. kuwabembeleza watoto walale
 2. jandoni
 3. harusi

Nyimbo hizo zikaja kuwekwa kanuni za utunzi kama vile vina, mizani, beti na kisha ushairi ukatokea.


Zoezi1
Sema kweli au si kweli.


Umuhimu wa shairi


 • Kufundisha maadili mema kama vile heshima, usafi, ukarimu, kusaidiana na kuvumiliana
  Kuikosoa jamii na kuipa mwelekeo kama vile kurekebisha maovu kama ufisadi, kujaribu kuishauri jamii kuhusu jinsi ya kukabiliana na magonjwa kama vile ukimwi na njaa
  Kuburudisha.

Mateso ya Watoto
1.Ninalia na kulia, nakumbuka na umia,
Namwomba naye Jalia, nipate cha kutumia,
Nikikumbuka dunia, nataka hata zimia,
Mateso yetu watoto, ni Mola anayejua.2. Ofisa kanichukua, kule kwetu ni Bungoma
Nikaletwa Kaliua, nikamlelee Wema
Maendeleo amua, miezi sita kukwama,
Mateso yetu watoto, ni Mola anayejua.


3.Baba kuwa safarini,nanyimwa nacho chakula,
Malalo yangu bandani,kunukiwa na milala,
Mapema osha sahani,na mabaki ninakula.
Mateso yetu watoto,ni Mola anayejua.

4.Mwili wangu,kidhofika,babu auliza hali,
Nami kujibu nataka, mama kazidi ukali,
Wapi nitenda fika, ndugu kwa Mola wasili,
Mateso yetu watoto, ni Mola anayejua.


5. Nilikwenda migodini, napo kumbukumbu kovu,
La kufikiwa shimoni, mguu wangu mbovu,
Sasa nami masikini, nimebaki mlemavu,
Mateso yetu watoto, ni Mola anayejua.Katika shairi ulilosoma umetambua ya kwamba:-

 1. Lina beti tano- ubeti ni kifungu kimoja au mgawanyiko maalum unaopatikana katika shairi
 2. Vina (kwa umoja Kina) ni sauti zinazotokea katika mwisho wa kipande cha mshororo.
 3. Mizani ni silabi au tamko moja katika neno la shairi
 4. mshororo ni msitari mmoja  katika shairi
 5. kibwagizo ni mshororo unaorudiwa katika betiMaudhui
Katika baadhi ya mashairi ujumbe, maudhui au habari wa mtunzi hujitokeza wazi lakini katika mashairi mengine ujumbe umejificha. Kwa mfano shairi hili ujumbe umejitokeza waziwazi kama vile watoto kuajiriwa, kunyimwa haki zao na kunyanyaswa.


Maana na umuhimu wa kamusi
Kamusi ni kitabu kinachohifadhi maneno yanayopatikana katika lugha fulani katika kipindi fulani cha wakati.


 Kamusi ni muhimu sana kwa jamii:

Hutoa maelezo ya maana za maneno na kutupa ufafanuzi unaotusaidia kuelewa maana za maneno mapya au mazito tunayokumbana nayo katika lugha.

Hutuwezesha kufahamu namna maneno yanavyoendelezwa

Hutuangazia aina ya neno yaani  kama neno ni nomino, kitenzi, kiwakilishi, kivumishi, kielezi, kihisishi au kihusishi

Hutuelekeza namna ya kutumia neno fulani. Aghalabu kamusi nyingine zinapotoa maelezo ya neno hufuatiliza na kuonyesha jinsi neno linavyotumiwa katika sentensi
Hutudokezea visawe vya maneno
Hutuonyesha kama neno hubadilisha umbo lake katika wingi toka umoja
Hufahamisha namna kitenzi kinavyoweza kunyambuliwa


Mpangilio wa maneno
Kamusi huyapanga maneno kwa njia ambayo humrahisishia mtumiaji kuyarejelea kama ifuatavyo:

 1. Maneno hupangwa kwa utaratibu wa kiabjadi au kialfabeti kuanzia A - Z kwa mfano

Amana
Amani
Bakuli
Baraza
Baridi
Chai
Chura
Daima
Dira
Wehu
Yai
Zama

Tanbihi
Ikiwa sauti za kwanza katika maneno zinafanana kwa mfano kama katika maneno Amana na Amani, mtu huenda kwa sauti ya pili, ikiwa pia hizo zinafanana, huenda kwa ya tatu au ya nne kama hali hiyo inajitokeza kwa sauti ya tatu, huendelea na hali hii mpaka sauti zitakapotofautiana, hapo ndipo huangalia ile inayokuja kwanza kiabjadi.
 1. Maneno hupangwa kwa njia elekezi. Pale juu pembeni mwa ukurasa huwekwa neno linalotangulia kutolewa maelezo katka ukurasa huo.Haya humrahisishia mtumiaji kukadiria kwa wepesi pale atalipata neno analolitafutia maana na hivyo kuokoa wakati.Iwapo neno ni kitenzi, kiambishi 'ku' kinachotangulia vitenzi hudondoshwa. Hivyo:

Kuchota huwa Chota
Kufariji huwa Fariji
Ku
pamba huwa pamba
Ku
safiri huwa Safiri
Ku
tembea huwa Tembea
Matumizi ya Vifupisho
Kamusi hutumia vifupisho kuonyesha aina za maneno ya Kiswahili,mathalani;
(
N) - Nomino
(
T) -Kitenzi
(
V)- Kivumishi
(
W) -Kiwakilishi
(
E) -Kielezi
(
U) -Kiunganishi
(
I) -Kihisishi


Hali kadhalika, kunavyo vifupisho vya maneno mbali mbali vinavyotumika katika kamusi navyo ni kama vile;


  Taz ikimaanisha; tazama
  M.f ikimaanisha; mfano
  K.v ikimaanisha kama vile
  N.k ikimaanisha; na kadhalika
  M.t ikimaanisha; methali
  Ms ikimaanisha; msemo
  Nh ikimaanisha; nahau


Umoja na Wingi
Kamusi pia hutambulisha umoja na wingi wa nomino.
Mfano.
Kitenge (N) vi -(vi-ni kiambishi kinachoonyesha wingi wa kitenge yaani vitenge)
Binadamu (N) (Hii haikuwekewa kiambishi chochote kwani hubakia vivyo hivyo katika umoja na wingi)
Shamba (N) ma ;(ma-ni kiambishi kinachoonyeshawingi wa shamba yaani mashamba)
Mgomba (N) mi - (mi -ni kiambishi kinachoonyesha wingi wa mgomba yaani migomba)


Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu