KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Sarufi Na Matumizi ya Lugha - Kiswahili Kidato Cha 1

utanguliziSauti,Silabi na Maneno
Sauti ndicho kipashio au kipengele cha chini kabisa katika lugha. Sauti hutumiwa kuunda silabi za maneno. Kwa mfano;
Maneno baba,oa na mjomba yameundwa kwa sauti zifuatazo:-

Baba ; b+a+b+a
Oa; o+a
Mjomba; m+j+o+m+b+a
Kabla ya kujenga maneno,sauti hizi hujenga silabi. Silabi ni tamko moja katika neno. kwa mfano,
Ba+ba ; = baba, O+a; = oa, M+jo+mba;= mjomba
Ndwe+le; = ndwele
Kama inavyodhihirika katika mifano hii, silabi inaweza kujengwa na:-Konsonati + irabi b+a
Irabi peke yake / o/a
Konsonati peke yake m
Konsonati mbili +irabi mb+a
Konsonati tatu + irabi ndwe+le


 

Sentensi
Hebu tazama jinsi maneno tuliyojenga yanaweza kuunda sentensi.
Sentensi ni mpangilio wa neno au maneno kisarufi unaoleta maana.
Kuna aina tatu za sentensi.
Hizi ni
Sentensi sahili, ambatano na changamano.
Sentensi
Sahili huwa ni sentensi iliyojengwa kwa kitenzi kimoja.
kwa mfano
Mwanafunzi anasoma.
Mjomba amevaa kanzu.
Sentensi
ambatano huwa ni sentensi mbili sahili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia kiunganishi, kwa mfano,
Dobi alifua nguo
kisha akazipiga pasi.
Ekomwa amechaguliwa kama diwani
na kisha akateuliwa kuwa meya.
Sentensi
changamano huwa ni sentensi iliyoundwa na sentensi mbili sahili ambazo zinategemeana.sentensi moja sahili haiwezi ikawasilisha maana bila sentensi sahili ya pili.
kwa mfano,
Yiene aliyepita mtihani wake vizuri amepata mfadhili.
Watoto wanaorandaranda mtaani watasakwa na kupelekwa shuleni
Mifano ya sentensi,
1.Wazazi hawashindwi kuwalea watoto
2.Kila mtu anapenda kuwa bingwa
3.Unafaa kuwa kimya katika maktaba
4.Vijana wanacheza mpira
Nomino na Vitenzi
Maneno yanayotumiwa kutajia vitu, viumbe, mahali, au hali kama tulivyoyaona  huitwa NOMINO.
Vile vile kuna maneno ambayo hutumiwa kurejelea vitendo katika sentensi. Maneno haya huitwa VITENZI. Kwa mfano,Kimbia


sukumana
Panda


Nawa
Mizizi na Viambishi katika Vitenzi

Hebu tazama vitenzi vifuatavyo;-

ana/pik/a
ata/pik/a
wata/pik/a
ameni/pik/ia

ana/imb/a
tuli/imb/iwa
mna/imb/iana
uli/imb/wa


Sehemu iliyo katika kisanduku huitwa mzizi wa kitenzi. Hii ni kwa sababu haibadiliki kitenzi kinaporefushwa mwanzo na mwisho wa mzizi.
Sehemu zinazotanguliza mzizi huitwa kiambishi awali[ana/pik/a], na zinazotokea baada ya mzizi huitwa kiambishi tamati [ana/pik/a] .Vivumishi
Pia kuna maneno ambayo hutumiwa kueleza zaidi kuhusu nomino. Maneno haya yenye kutoa sifa huitwa vivumishi kwa mfano;
Gari
nyekundu

Nyumba kubwa


Mzee kipara


Nyumba mbiliHitimisho
Kuna aina nyingine za maneno ambayo hutumika katika sentensi.Aina hizi ni;-
Viwakilishi
ni maneno au viambishi vinavyosimama badala ya nomino kwa mfano,
1.Lendeni alikuja.Tunaweza dondosha nomino Lendeni na tukasema Alikuja.Hapa kiambishi a kinasimama badala ya nomino Lendeni
2.Maduka yote yalifungwa. hapa tunaweza dondosha nomino maduka na tukasema yote yalifungwa. yote ni kiwakilishi kinachosimama badala ya nomino maduka.
3.Wakulima walipata hasara mwaka jana.Wao walipata hasara mwaka jana.katika sentensi ya pili wao ni kiwakilishi kinachosimama badala ya nomino wakulima
4.Mambo unayoambiwa unafaa uyazingatie kwa makini.
Hayo unayoambiwa yafaa uyazingatie kwa makini. Hayo ni kiwakilishi kinachosimama badala ya nomino mambo.

Vielezi;ni maneno ambayo hufahamisha zaidi kuhusu kitendo.Yanajibu maswali kama vile kitendo kilitendeka wapi?vipi?namna gani?lini? na kilitendwa mara ngapi?
kwa mfano,
1.Baba aliamrisha kijeshi. Neno kijeshi ni kielezi.
2.Tulikimbia uwanjani mara nyingi. Neno mara nyingi ni kielezi.

Viunganishi
ni maneno yanayotumika kuunganisha maneno mengine, vifungu au sentensi.
kwa mfano,
1.Chagua kitabu cha hisibati au cha sayansi. Neno au ni mfano wa kiunganishi.
2.Walifika vijana kwa wazee.

Vihisishi
ni maneno yanayoonyesha hisia mbalimbali kama vile hofu,furaha, mshangao, wasiwasi na kadhalika.
kwa mfano,
1.La Hasha!sitakubali kashfa hiyo.
2.Salale!Mtoto huyo amenusurika ajali hiyo.

Vihusishi
ni maneno yanayotumiwa kuonyesha uhusiano uliopo kati ya vitu viwili au zaidi.
kwa mfano,
1.Vitabu viko juu ya meza
2.Tangu mwakilishi wetu achaguliwe haonekani kijijini.
Kwa mujibu wa upatanisho wa kisarufi,  Kiswahili kina ngeli zifuatazo :-

Ngeli ya A-WA

Ngeli ya KI-VI

Ngeli ya U-I

Ngeli ya LI- YA

Ngeli ya U-YA

Ngeli ya U-ZI

Ngeli ya I-ZI

Ngeli ya U-U

Ngeli ya Ya-YA

Ngeli ya I-I

Ngeli ya KU

Ngeli ya Mahali PA-KU-MU,


Zoezi la 1

Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kujaza viambishi awali vinavyofaaNgeli ya Mahali

Ngeli hii hugawika mara tatu kulingana na viambishi awali vya upatanisho wa kisarufi.
Navyo ni;
Pa/po. Hiki huonyesha mahali mahsusi panapojulikana au panapoonekana.
Mfano.
Pale barabarani
pamemwagika petroli.

Hapo mlipoketi pana siafu.Ku/ko Hiki huonyesha mahali kusiko dhahiri au kusikojulikana vizuri.
Mfano.

Huku kuna starehe na anasa nyingi


Huko kwao kuna maendeleo mengi.


Mu/mo Hiki huonyesha mahali ndani ya kitu.
Mfano.
Mle ukumbini mmejaa watu.Shimoni mlimoingia panya mna nyoka.
Nomino katika hali ya

Udogo na ukubwa

Nomino katika hali ya udogo huingia katika ngeli ya KI-VI nazo nomino katika hali ya ukubwa huwa katika ngeli ya LI-YA
kwa mfanoHitimisho


Ni muhimu kukumbuka kuwa:-
  Nomino zote za viumbe wenye uhai ziko katika ngeli ya A-WA
  Nomino zote katika ngeli ya KU huundwa kutokana na vitenzi
  Ngeli ya YA-YA huusisha nomino ambazo kwa kawaida huwa majina ya vitu majimaji.Zoezi la 2

ANDIKA KULINGANA NA MAAGIZO YALIYO KWENYE MABANO :-


Kitambulisho kilichopatikana barabarani ni cha WafulaVitambulisho vilivyopatikana barabarani ni vya akina Wafula.


Cheti kilikabidhiwa aliyefuzu


Vyeti vilikabidhiwa waliofuzu


Kijia kile kinaelekea mtoni


Vijia vile vinaelekea mitoni

Mnyambuliko wa Vitenzi   


 


Maana ya Mnyambuliko

Mnyambuliko ni hali ya kuvuta kitenzi kwa kukipa viambishi tamati ili kuleta maana nyingine
kwa mfano,


Sehemu zilizo katika kisanduku zinaonyesha mnyambuliko katika kauli mbalimbali kama ifuatavyo

Zoezi 1
Sentensi zufuatazo zinahusu kitenzi katika kauli ya kutenda katika hali zilizotajwa.
Bainisha hali hizo na sentensi hizi


Kauli za kunyambua

 1. Tenda - hii ni hali ya kufanya kitendo kwa mfano, cheka, imba, ruka ,safiriTendewa - mtu hutendewa kitu / jambo na mwingine.

Pia mtu / watu hutenda jambo kwa niaba ya mwingine / wengine

 

kwa mfano, Alichekwa, somewa, imbiwa, rukiwa, safirishwa.
Vitenzi katika kauli hii huishia na
-iwa, -ewa, -liwa, lewa

Tendeka: - Huonyesha kutendeka au kukamilika kwa jambo fulani. Wakati na mtendaji havitiliwi maanani.


kwa mfano, Chekeza, imbika, rukika, safirika.Vitenzi katika kauli hii huishia na -ika, -ka

Tendeana: - Hii ni hali ya pande mbili kutendeana, upande mmoja unatenda na ule mwingine unatenda vile vile.Vitenzi katika hali hii huishia kwa -ana


Kutendea: - Kitenzi katika kauli hii hudokeza yafuatayo;

 1. Kifaa fulani kilitumiwa kutekeleza kitendo Fulani
 2. Kitendo kilitendewa mahali fulani
 3. Sababu ya kitendo fulani
 4. Kitendo kuelekea mtu au kitu fulani
 5. Kitendo kilitendwa kwa niaba ya mtu fulani

Vitenzi katika hali ya kutendea huisha na -ia au -ea

 Kauli za kunyambua ii

Kutendea, hali hii huonyesha kupokea tendomfano,

Nguo zimeanikwa


 
Mti umepand/wa/
Nyama imechom/wa/
Mto umevuk/wa/
Shamba litalim/wa/
Vitenzi katika kauli hii huisha na - wa,- lewa au -liwa


Kutendesha; -   Katika hali hii mtu au kitu fulani husababisha mtu / kitu
Kingine kutenda jambo fulani
Pia hutumiwa kuonyesha hali ya kulazimisha

kwa mfano, Kuendesha, rusha, pikisha, zamisha

Vitenzi katika kauli ya kutendesha huisha -ish, -esh, - za, na,-lishUtangulizi 


Nukta mkato/ semi koloni hutumiwa kutenganisha sentensi iliyo ndefu sana. Kwa mfano:(1) Hakuna jambo rahisi maishani; kijana, ukitaka cha mvunguni lazima ujitolee na ustahamili kuinama.(2) Mto wa Nairobi umechafuliwa sana; Itabidi tuungane mikono kuusafisha na kuhakikisha kuwa maji yake ni safi na yanaweza kutumiwa na binadamu pamoja na wanyama.


1.Nukta pacha /koloni hutumika kutanguliza maneno yaliyo katika orodha.Mfano:Mama alienda sokoni akanunua matunda: maembe, mapera, mafenesi,parachichi, matikiti, mapapai na machungwa2.Kuonyesha maneno ya msemaji katika mtindo wa tamthilia kwa mfano:Cherop: Njagi yuko wapi?Kariuki: AmetokaCherop: Na Simiyu atakuja leo?Kariuki: Bila shaka.3. Kutenganisha saa na dakika au saa,dakika na sekunde.Mfano10:30, 11:25:32 4.Katika misahafu kama vile Korani na Bibilia kuonyesha sura na aya.Luka 3:7-12Yunus a.s, 4:163Parandesi/mabano hutumiwa:
Kubainisha sauti za lugha mfano[a],  [e], [i ], [o], [u ]
Kufungia nambari au herufi katika kuorodhesha
. Mfano, kuwasili kula kulala na kadhalika
Hutoa maelezo kwa waigizaji
kwa mfano, Achieng (akilia) Kwa nini unaniacha? (anasinasina)Hutumiwa kutoa ufafanuzi zaidikwa mfano,Mombasa (mji wa pwani ya Kenya) ni maarufu sana kwa Utalii.Hubana kisawe cha maneno au kufungia maneno yanayotangulia au maelezo kuhusu neno katika sentensikwa mfano Ami ( nduguye baba) amefika.

 

 


 


Alama hisi hutumiwa kuonyesha hisia za moyoni kama vile furaha, mshangao,uchungu,mshtuko,majuto, huzuni na kadhalika, Mfano:
1.Lo
!mtoto amevunja sahani!
2.Hongera
!
3.Umefuzu mtoto mzuri
!
4.Laiti ningalijua
! Nisingelimkopesha!
5.Pole
! Sikujua ulipata msiba.


Hitimisho
Kuna alama nyingine zaidi za kuwakifisha kama vile:
ritifaa
( ' )
kiulizi
(?),
mkwaju/mshazari
(/)
alama za mtajo/za kunukuu/za usemi
(")
herufi kubwa (H, E)

Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu