KCSE ONLINE

Kiswahili Report

4.0 KISWAHILI (102)

4.1 MATOKEO YA MTIHANI WA SOMO LA KISWAHILJ MWAKA WA 2010

Jedwali hili linaonyesha matokeo ya mtihani wa somo Ia Kiswahili katika muda wa miaka minne (2007 hadi
2010).

Jedwali 4: Matokea ya mtihani wa Kiswahili (2007 2010)
 

Mwaka Karatasi Watahiniwa Alama ya
Juu
Alama ya
Wastani
Alama ya
Tanganislio
 
2007 1
2
3
Jumla
  40
80
80
200
15.80
32.22
43.49
91.51
6.42
11.91
13.12
27.00
2008 1
2
3
Jumla
  40
80
80
200
14.20
29.18
31.17
74.55
7.18
11.43
13.64
32.25
2009 1
2
3
Jumla
  40
80
80
200
15.40
29.03
32.72
77.15
6.93
11.96
13.11
32.00
2010 1
2
3
Jumla
  40
80
80
200
14.32
33.77
39.22
87.10
6.53
11.96
14.09
28.73

Jedwali hili Iaonyesha kuwa kwa ujumla:

4.1.1 Mama ya wastani ya karatasi ya 1002/1) ya mwaka wa 2010 imeshuka ikilinganishwa na mwaka wa
2009.

4.1.2 Matokeo ya karatasi ya pili (102/2) ya mwaka wa 2010 yameshuka yakilinganishwa na yale ya mwaka wa 2009.

4.1.3 Matokeo ya karatasi ya tatu (102/3) ya mwaka wa 2010 yameimarika kutoka alama ya wastani 32.72 mwaka Wa 2009 hadi 39.22 mwaka wa 2010.
4.1.4 Matokeo ya Kiswahili kama somo kwajumla katika mwaka wa 2010 yameimarika. Alarna ya wastani ya Kiswahili kama somo mwaka huu ni 87.10 yakilinganishwa na mwaka wa 2009 ambapo alama hii ilikuwa 77.15(ongezeko Ia 10.16)

Alama ya tanganisho inaonyesha kuwa kuna baadhi ya watahiniwa ambao waliweza kujipatia alama nyingi zaidi ya alama ya wastani mwaka wa 2010, ikilinganishwa na mwaka 2009. Alama hii ilikuwa 32.58.
 

4.2 INSHA (102/1)

Jedwali 5: Matokeo ya Karatasi ya kwanza ya miaka ya 20072010.
Mwaka 2007 20iiT 2009 2010
AlamayaWastani 15.80 14.20 15.40 14.32
Tananisho6.427.186.933
Jedwali hill laonyesha kwamba kwa miaka liii minne (2007-20 10), matokeo ya karatasi ya 102/1 yamekuwa yakipanda na kuteremka na kwamba watahiniwa wengi hawajaweza kujipatia alama zaidi ya nusu ya alarna zote ambazo zinaweza kutuzwa ambazo ni 40. Katika mwaka wa 2010, matokeo haya yaliteremka kwa kiasi eha alarna 1.08.
 

Tutachanganua swali la kwanza ambalo lilikuwa la lazima na ambalo halikufanywa vizuri.
Swali la 1
Andika wasifu wa ndugu yako ambayc ainepanga haifa ya kuchangisha pesa za kumgharamia masomo ya Chuo Kikuu.
Watahiniwa walikosa alama kwa sababu wengi hawakutofautisha kati ya wasifu, wasifukazi, wasifutanzia, tawasifu,ratiba,barua,kumbukumbu na kadhahka.
tTafadhali tazama mwongozo ulioambatanishwa katika ripoti hii iii uone jinsi insha hii ya hotuba ilivyostahili kuandikwa.
 

USHAURI KWA WALIMU
-Walimu wawatayarishe wanafunzi wao katilca maeneo yote bila ubaguzi kama ilivyo katika silabasi ya Taasisi ya Elimu.

4.3 MAPENDEKEZO:

-Walimu wazidi kuwapa wanafunzi mazoezi zaidi katika uandishi wa kiuamilifu.
-Walimu watumie silabasi za K.I.E na K.N.E.C katika ufundishaji wao.
-Wanafunzi wahimizwe kusoma magazeti na kujifahamisha na matukio ya kila siku katika jamii na mazingira yao-kitaifa na pia kimataifa; ilmuradi waweze kuyashughulikia maswali yanayohusu masuala ibuka iwapo yatatahiniwa.
Haitoshi kujifunga katika masuala yaliyo vitabuni pekee.
-Wanafijnzi waamasishwe kutafsiri maswali kwa uangalifu mkubwa huku wakizingatia maneno muhimu.
 

4.4 LUGHA (102/2)
 

Matokeo ya karatasi ya 102/2 yameimarika mwaka wa 2010. Matokeo haya ndiyo bora zaidi katika kipindi cha miaka minne.
Maswal i ya ufahamu na ufupisho/muhtasari ndiyo yaliyowatatiza watahiniwa. Tutayachanganua hapa.
Swali Ia 1

1 UFAHAMU (alarna 15)

Sorna kfungu kfiiotacho kisha ujibu ,naswaii
Suala Ia mahusiano ya wanadaniu katika jainii, uaiuishaji wake na udhihirikaji wake limewashughulisha wataalamu wa elimu jarnii kwa dahari ya miaka. Suala hili huwatafakarisha wataa!amu hao kutokana na umuhimu wake katika maisha ya binadarnu. Msingi rnkuu wa uainishaji wa mahusiano hayo ni kukichuza kipindi cha mahusiano yenyewe. Yapo mahusiano baina ya waja ambayo yanachukua inuda mfupi, kwa mfano saa au dakika chache, na inengine ainbayo huenda yakachukua miaka ayami.

Mahusiano ya inudanrefli kabisani yale yanayojulikanakama mahusiano ya kudurnu. Inainkinika kudai kuwa miundo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi huweza kuyadhibiti mahusiano hayo kwa kiasi kikubwa. Watu wengi huitakidi kuwa uhusiano uliopo baina ya mtu na jamaa yake utachukua inuda rarefu, na kwa hiyo ni uhusiano Wa kudumu. Hali liii hutokana na uhalisi kuwa tunahusiana na jarnaa zetu kwa kipindi kirefu labda tangu ukeinbe hadi utu uzima wetu. Uhusiano huu hautarajiwi kuvunjwa ia umbali Wa niasafa baina yetu; tunaendelea kuwasiliaua kwa barua au katika enzi liii ya utandawazi, kwa kutumia nyenzo za teknohama kama mtandao na simu za mkononi, na kudumisha uhusiano wetu wa kijaniaa. Ham hivyo, inawezekana baadhi ya mahusiano ya kijaznaa yasiwe ya kudumu. Mathalan, uhusiano uliopo baina ya rnke na niume, na ambao unatarajiwa kuwa wa kudumu au wa kipindi kirefu, unaweza kuvunjwa kwa kutokea kwa talaka. Talaka hiyo inavunja ule uwezekano wa uhusiano wa kudumu unaofurnbatwa na sitiari ya pingu za maisha.

Katika ngazi ya pili, snahusiano ya kipindi cha wastani, kuna mahusiano yanayohusisha marafiki zetu maishani, shuleni au kwenye taasisi zozote zile, majirani zetu, wenzetu katika niwahali ama kazi. washiriki kwenye sehemu za ibada au za burudani Ba wenzetu kwenye iyama tofauti na makuadi ya kujitolea. Inawezekana kudahili kuwa baadhi ya inahusiano haya, hususan baina ya marafiki na rnaj irani huweza kuwa ya niiongo na daima. Hali hii huweza kutegernea niuundo na mfiamo wa janiii. Kwa infano, kwa wanajamui wanaoishi kwenyejanibu fulani mahsusi, na kwa miaka tawili bila ya kuhajiri, uhusiano wao na majirani huweza kuwa wa kudumu. Hali hii inasigana na hali iliyoko kwenye maisha ya mijini. Maisha ya niijini yana sifa ya kubadilikabadilika. Isitoshe, kutokana na nifumo wa maisha ya kibepari yanieghosbi ubinafsi tuwingi. Mawimbi ya mabadililco na ubinafsi huweza kuutnomonyoa ukuta wa uhusiano Wa kudurnu.

Mwelekeo wa niaisha ya siku hizi ya uhainaji kutoka maeneo au viambo walikoishi watu unasababisha kuponibojea kwa mahusiano ya kudumu baina yao on inajirani zao. Uhusiano kati ya wenza katika mazingira ya kazi unahusiana kwa kiasi fulani na ule wa majirani. Vimbunga vya uflitwaji kazi, ubadilishaji wa kazi, hali zisizotegeniewa na miftimo ya kimataifa patnoja na hata tuifumo ya kisiasa huweza kijathiri mshjkaniano wa wanaohusika kazini,
Kiwango cha mwisho cha mahusiano ni uhusiano wa mpito an wa muda nifupi. Mahusiano ya ama hii hujiri katika muktadha ambapo pana hudurna fulani. Huduina hizi zinaweza kuwa za dukani, lcwenye seheniu za ibada, kwenye kituo cha niaflita, kwa kinyozi, kwa rnsusi na kadhalika. Kuna sababu kadha zinazotufanya kuyazungumzia mahusiano ya ama hii karna ya nipito. Kwanza, uwezekano wa rnabadiliko ya anayeitoa hudunia hiyo ni mkubwa. Si ajabu kuwa unaporudi kwa kinyozi an nisusi unatanibua aliyekushughulikia hayispo. Hata hivyo, kuna vighairi hususa pale ambapo mtoa hudurna anayehusika ni yule yule nimoja.

Mahusiano ya rnpito yanatawaliwa na �uhusiano wa chenibe chenibe.' Uhusiano wa chernbe cheinbe, bidhaa ya mfijoio wa kibepari, unamaanisha kuwa kinachonishughulisha mW ni chembe ndogo tu ya mwenzake, Chembe hiyo inaweza kuwa hudurna, kwa infano, gazeti analokuuzia tutu, viatu anavyokushonea, nguo anazokufulia. usus anaokufanyia n,k. Mahusiano ya ama hii yarnetovukwa na hisia za utu Ba zao Ia mifumo ya kisasa ya kiuchunii na kijamii. Mtu anayehusiana na mwezake kwa misingi ya chenibe ndogo tu, huenda asijali kama niwenzake ainekosa chakula. aniefutwa kazi, amefiliwa, ameibiwa na kadhalika.

Sualakuu tunalopaswakujiulizani:je. runahusiana vipi najamaa zetu, taasisi zetu, niarafiki zetu
na majirani zetu Je, uhusiano wetu na rain wenzetu ni wa ama gani Je, uhusiano wetu on nchi yetu ni Wa mpito au ni Wa kudurou

Kwa ujumla, niaswali ya kifungu yalihitaji mtahiniwa asome, aelewe na kuchanganua, kusanisi, kutafsiri, kutathmini na kutumia maudhui katika kifungu kujibu maswali.

Watahiniwa pia walikosa alama katika swali hili kwa sababu wengi hawakuwa na stadi ya kujieleza vizuri na wakafanya makosa mengi ya sarufi na tahajia.

(a) Taja kigezo muhirnu cha kuzungumzia mahusiano. (alarna 1)

 

(h) Eleza iniani ya wath kuhusu uhusiano baina yajamaa. (alama 1)
(c) Fafanua athari ya teknolojia kwenye mahusiano ya wath. (alarna 2)
(d) Eleza sababu nne kuu za kuharibika kwa mahusiano katika maisha ya leo. (alama 4)
(e) Taja sifa kuu ya mahusiano ya muda mfupi. (alama 2)
(f) Ye, kifungu, hiki kina ujumbe gani mkuu (alama 2)
Majibu
(a) Kukichungua au kukiangalia kipindi cha mahusiano yenyewe.
(b) Kuwa utakuwa ithusiano wa kudumu/utakuwa uhusiano wa muda mrefu.
(c) Huwezesha watu au jamaa walio mbali kuwasiliana/simu au mtandao huwa chanzo au nyenzo muhimu ya kudumisha uhusiano.
(d) Mabadiliko ya mara kwa mara/kuwepo kwa ubinafsi mwingi.
- Uharnaji wa watu kutoka viambo/mitaa yao
- Ufutwaji Wa wath kazini na kwa hivyo kutengana na wenzao.
- Ubadilishaji wa kazi.
- Kutotegemeka kwa kazi zenyewe.
- Nguvu na kani za kiuchumi ni nyingi. Mifumo ya kisiasa huweza kuathiri maisha.

(e) Uhusiano wa chembechembe/mtu hujihusisha na chembe ndogo ya mwenzake. Mahusiano yanapasa kutawaliwa na hisia za utu, undani yaani mahusiano yanayogusa nafsi zetu,ya dhati, ya kuwajibika kwa wenzetu na nehi yetu.
(0 (1) Inapingana;
(ii) yamej aa/yametawaliwa na
(iii) vinyume

 

Swali Ia phi: UFUPISHO/MUHTASARI

2 MUHTASARI (alama 15)

!amii ya lee inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni ya maai-ifa. Inawezekana kusema kuwa uchumi wa jamii za leo an zijazo utategemea maarifa zaidi kuliko utakavyotegernea wenzo wowote mwingine. Utambuzi Wa uwezo mkubwa wa maarifa katika maisha ya binadamu ndio msingi wa warn kusema �maarifa ni nguvu.

Maarifahuelezwahva tamathali hii kutokanana uwezo Wa: kuyadhibiti, kuyaendesha, kuyatawala na kuyaongoza maisha ya binadamu popote pale walipo. Mm ambaye arneyakosa maarifa fulani huwa ameikosa nguvu hiyo muhimu na maisha yake huathirika pakubwa. Kwa msingi hun, rnaarifa yanaweza kuangaliwa kama utajiri mkubwa ambao binadamu anaweza kuutumia kwa faida yake au kwa faida ya wanajamii wenzake. Ukweli huu ndio unaoelezwa na methali ya Kiswahili: �Elimu ni mali.' Elimu ni chimbuko Ia maarjfa muhimu maishani.

Msiigi wa utajiri na inaendeleo ya binadamu popote alipo basi ni maarifa. Je, maarifa kwa upande wake yana sifa gani Maarifa yenyewe hayana upinzani. Maarifa uliyo nayo huweza kuwa na warn wengine wengi pasiwe na upthzani baina yenu kwa kuwa kila rnmoja ana maarifa sawn. Kila minoja ana uhuru wa kuyammia maarifa hayo kama chanzo cha kuyazalisha maarifa mengine. Utumiaji wa maarifa yenyewe hanyamalizi maarifa hayo. Maarifa hayawezi kugusika ingawa mtu anaweza kuyanyumbua maarifa yenyewe kwa kuyatumia kwa namna tofauti.
Maarifa huingiliana na maarifa mengine. Maarifa aliyo nayo mtu mmoja huweza kuhusishwa aa maarifa aliyo nayo mtu mwingine iii kiivyaza an kuzuka na maarifa tofauti. Maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa namna arnbavyo mm hawezi kufanya bidhaa nyingine ile. Kwa mfano, ni muhali mm kulalarnika kuwa hawezi kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa sababu ana mzigo mzito wa maarifa kichwani.

Sifa nyingine muhimu ya maarifa ni kuwa yanaweza kuwasilishwa kwa njia za ishara an mitindo mingine ya kidhahania. Ikiwa unataka kukihamisha chombo fulani kutoka sehemu moja hadi aythgine, lazima uwazie ukubwa wake, uzito wake na labda hata umbali wa panapohusika. Maarifa huweza kubadilishwa au kugeuzwa na kuwa ishara ambazo huyafanya kuwasilishwa kwa njia nyepesi kuliko kwa mfano ikiwa mtu atayawasilisha katika muundo wa, kwa mfano, kitabu.

sambamba au kugotanishwa aa kipengele kingine cha maarifa. Huo huwa muktadha mzuri wa kuele�ka au kuwa na maana. Kwa mf ann, neno �mwerevu' huweza kuwa na maana kwa kuwekwa katika muktadha wa �mjiaga', �mjanja', �hodari' na kadhalika.

Maarifa huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo sana. Suala hili liaaeleweka kwa njia nyepesi tunapoangalia maarifa katika rnuktadha wa teknolojia. Data ziaazowahusu mamilioni ya warn, ambazo zingehitaji maelfu ya niaktaba na lukuki ya vitabu, huweza kuhifadhiwa kwenye kifaa kidogo kinachoweza kutiwa mfukoai.
Maarifa hayawezi kudhibitiwa an kuzuiliwa mahali fulani yasisainbae. Maarifa huenea haraka sana, Maarifa ni kitu kinachoepuka pingu za watu wanaopenda kuwadhibiti binadarnu wenzao. Hath pale ambapo mfumo wa kijamii an wa kisiasa unafanyajuu cl�ni kuwadhibiti raia au watu wenyewe, ni nmhali kuyadhibiti maarifa yenyewe. Inawezekana kuzidhibiti njia fulani za neneaji wa maarifa lakini maarifa hayo yatapata upenyu wa kusambaa. Ni kweli kuwa maarifa ni nguvu inayozishinda nguvu zote.

Swali hili lilihitaji mtahiniwa asome kifungu na kusanisi hoja muhimu na kuzifanyia muhtasari bila kuacha mawazo muhimu wala kupoteza manna asili ya kiflingu.

Mtahiniwa pia alihitaji stadi ya kutumia viunganishi vifaavyo iii kuleta mtiririko unaoridhisha.
Watahiniwa wengi walilemewa katika upande wa kutumia viunganishi iii kutiririsha mawazo. Wengi waliinua sehemu ambazo hazikuwa na uhusiano wowote kihoja. Stadi ya kujieleza kwa mtiririko ufaao lazima
ifundishwe.

Watahiniwa wengi walitatizika katika kudondoa hoja muhimu.
(a) Fupisha aya ya pili na ya tatu. (maneno 55 - 60)

Majibu
(a) - Maarifa huyadhibiti maisha ya binadarnu
-Maarifa ni nguvu muhimu maishani
-Utajiri na maendeleo hutegemea maarifa
-Maarifa hayana upinzani
-Maarifa hayamalizwi kwa kuturniwa na watu tofauti
-Maarifa hayagusiki
(b) Eleza sifa kuu za maarjfa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya va nane. (mandno 100- 110).
Majibu
-Maarifa huingiliana na maarifa mengine
-Huweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine
-Huweza kuwasilishwa kwa njia ya ishara
-Yana sifa ya uhusianaji
-Huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo
-Hayawezi kuzuiliwa yasisarnbae.

4.5 MAPENDEKEZO

Walimu waendelee kuwapa wanafunzi mazoezi ya rnaswali ya ufahamu na ufupisho na kusahihisha wakizingatia sarufi kwa sababujambo hili linazingatiwa wakati wa kusahihisha mtihani wa kitaifa.

Wanafunzi wasisitiziwe kwamba baadhi ya maswali ni ya stadi zajuu kama matumizi na tathtnini kwa hivyo maswali ambayo hayaonekani kuwa na niajibu ya kuinua moja kwa moja huulizwa pia.

Wanafimzi wapewe mazoezi ya muhtasari huku mtiririko ufaao ukisisitizwa mara kwa mara iii wapate kuzoea kutumia viunganishi kutiririsha hoja katika kujibu maswali ya rnuhtasari.

Walimu na wanafunzi watali maeneo yote ya sajili bila ya kujifunga kwa chache tu ambazo ni za kawaida.

*Masuala yote katika silabasi yafundishwe katika upana wake bila kubagua.

4.6 FASIHI (102/3)

Matokeo ya karatasi ya tatu (102/3) ya miaka ya 2007 hadi 2010.
 

 

 

Matokeo ya karatasi ya tam (102/3 ya mwaka wa 2010 yameimarika kutoka alarna ya wastani ya 32.72 mwaka wa 2009 hadi 39.22 mwaka wa 2010.
Tutachanganua swali la kwanza pekee katika karatasi hii kwa sababu lilikuwa la lazima. Pia ndilo lililoonekana kuwapa watahiniwa changarnoto kidogo.
Swali hili lilikuwa ni shairi kutoka diwani ya E. Kezilahabi

Sotna shatri hilt kisha ujibu maswali yanayofuara.
bhamiri yangu
Dhaniiri imenifunga shingoni.
Nami kama mbuzi nimefungwa
Kwenye mti wa urn. Kamba ni fupi
Na nimekwjshachora duara.
Majani niwezayo Icufikia yote nitnekula.
Ninaona majani mengi mbele yangu
Lakini siwezi kuyafilcia: kamba, kamba.
Oh! Nitnefungwa kama mbwa.
Nami kwa mbaya bahati, katika
Uhuru kupigania, sahani ya mbingu
Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
Kuifikia na hapa nilipofungwa
Nimekwishapachafua na kuhama siwezi.
Kainba isivoojiekana haikatiki.
Naini sasa sitaki ikatike, maana,
Mbuzi wa kamba alipofunguilwa, mashamba
Aliharibu na rnbwa aliuma warn.
Ninamshukuru aliyenifunga hapa
Lakini lazima nitamke kwa nguvu
"Hapa nilipo sina uhuru!"


(E. Kezilahabi)


(a) Taja mambo manne ambayo rnshairi analalanjikia.
(b) Kwa nini mshairi haoni baja ya yeye kuwa huru
(c) Eleza manna ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. "Kamba isiyoonekana haikatiki."
(d) Taja na utoe mifano ya ama mbili za tamathali zilizotumika katika shairi hii.
 

Majibu
(a) -Kufungwa
-Kunyimwa uhuru
-Alipofungwa pameharibika
-Angependa kuhama lakini hawezi
-Kuna majani mengi mbeie yake lakini hawezi kuyafikia
(b)
amekwisha zoea hail yaki
-Hapendi kuonekana tofauti. Hataki kuukosa uffi kwa sababu amefungwa katika kamba ya iflu.
majibu
(c) Ni dhamiri katika nafsi yake ambayo ameshikilia ambayo haionekani kwa macho ndiyo iliyomfunga


Majibu
(d) (i) Tashbihi -kama mbuzi
-Kama mbwa
(ii) Istiari/sitiari -Sahani ya mbingu, kamba isiyoonekana
(iii) Tasfida - Nimekwishapaehafua
Majibu
(e) Mishata: Mishororo ambayo maana yake inakamilika katika mshororo unaofuata
Mf: Nami kwa mbaya bahati, katika uhuru kupigania kamba ni fupi na nimekwishachora duara.
Nami kwa mbaya bahati, katika
Uhuru kupigania, Sahani ya mbingu
Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
Nami sasa sitaki ikatike maana
Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba Majibu
(1) Nimefungwa kama mbwa na kwa bahati mbaya katika kutaka kuondoka pale nimeipiga teke sahani ya mbingu ambayo imeenda mbele na siwezi kuifikia.
Na pale nllipofungwa ni pachafu ila siwezi kupatoka.
 

4.7 MAPENDEKEZO

- Walimu wafhndishe vitabu vilivyoteuliwa kwa ukamilifu wake huku wakizingatia
ploti,wahusika,maudhui,mbinu na lugha.
- Wanafunzi wahimizwe kutambua rnasuala muhimu yanayoj itokeza katika hadithi zote katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine

- Wanafunzi wawekewe misingi bora katika fasihi simulizi tangu kidato cha kwanza.
- Walimu wawafundishe wanafiinzi wao istilahi muhimu zinazohusiana na ushairi.
* Katika karatasi hii, swali lililohepwa na baadhi ya watahiniwa ni nambari tatu.
Swali hili lilihitaji watahiniwa waweze Icukumbuka ni wapi dondoo hilo linapopatikana kitabuni.
TANB. Ni dhahiri kwamba kwa jumla matokeo ya mtihani wa somo Ia Kiswahili yameimarika katika mwaka wa 2010 yakilinganishwa na mwaka wa 2009.

- Ni mataraj io yetu kuwa wahmu na wanafunzi watamakinika kuj ifaidi na mapendekezo tuliyoyatoa katika ripoti hii ili kuzidi kuboresha matokeo ya somo la Kiswahili katika siku za halath.

 

 

What it takes

xxx

Terms    |    About    |    Contacts         State of the art technology


Copyright ©  KCSE ONLINE 2017. All Rights Reserved.