KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kusikiliza na Kuzungumza - Kiswahili Kidato Cha 2

UTANGULIZI
Katika somo hili la matamshi, tutashughulikia vitate na vitanza ndimi.Vitate ni maneno yanayotatiza kimatamshi.Utatanishi huu unatokana na;
kukaribiana kimatamshi kwa sauti fulani.Mfano. posa poza.
Mtamkaji kuathiriwa na lugha ya kwanza au lugha nyingine;Mfano. mahali /mahariVitate


Vitanza ndimi


  Sikiliza vitanza ndimi vifuatavyo kisha uvitamke.

  1. Sitasitasita kusisitiza kuwa sita na sita si sita.


  2. Vazi alilovua alivaa baada ya kulifua likamfaa sana.


  3. Makoti Alikoti alipohukumiwa, alipiga magoti na kulivua koti kortini.


  4. Juzijuzi mjuzi jasusi alikutana na mjusi akienda kumuona mchuuzi akichuuza mchuzi.


  Himizo

  Muundo ni sura au namna kitu kinavyoonekana kwa nje .

  Soma mahojiano yafuatayo kati ya mwandishi wa habari na mwanariadha huku ukizingatia muundo wa mahojiano yenyewe.

  Mwandishi: Hujambo dada?

  Mwanariadha: Sijambo.

  Mwandishi: Mimi ni Philip Okelo mwanahabari wa Shirika
  Utangazaji la Mambo Leo.Ningependa
  Utangazaji la Mambo Leo.Ningependaa
  kukuhoji kuhusu kukuhoji kuhusu la ushindi
  wako.Waeleze wasikilizaji majina yako.

  Mwanariadha: Jina langu ni Janet Jelimo. Kwa jina la utani
  naitwa Risasi.

  Mwandishi: Kwa nini wanakuita Risasi?

  Mwanariadha: Kwa sababu ya kasi yangu katika mbio.

  Mwandishi: Hongera kwa kushinda medali ya dhahabu
  katika michezo ya Olimpiki.

  Mwanariadha: Asante!

  Mwandishi: Je, mipango yako ya siku za usoni ni ipi?

  Mwanariadha: Ningependa kupata medali nyingi zaidi za dhahabu na kuvunja rekodi nyingi zaidi kabla ya kustaafu.

  Mwandishi: Mbali na riadha, unashiriki mambo yepi mengine?

  Mwanariadha: Tayari nimejiunga na Chuo Kikuu cha Fujihama ili kujiendeleza kielimu.

  Mwandishi: Unasomea nini?

  Mwanariadha: Nasomea Uhandisi wa Tarakalishi.
  Mwandishi: Una ujumbe gani kwa vijana?
  Mwanariadha: Ningependa kuwahimiza vijana wajitolee na kukuza vipawa vyao. Kila mtu amebarikiwa na kipawa fulani. Lakini watu wengi hupuuza vipawa vyao na kukosa kuvikuza. Ni muhimu vijana kujipa muda na kutambua vipawa walivyo navyo. Baada ya kuvitambua, wapaswa kujitolea na kutia bidii ili waweze kunufaika kutokana na vipawa hivyo.


  Mwandishi:
  Asante kwa kutembelea Idhaa hii. Vijana wamepata kujifunza mengi kutoka kwako. Tunakutakia kila la heri.
  Mwanariadha: Asante sana.


  Tanbihi
  Inadhihirika kuwa mahojiano huwa na maswali elekezi ya kudadisi undani wa jambo fulani.
  Mahojiano yanaweza yakashirikisha mada mbalimbali kutegemea muktadha.

  Tanbihi
  Inadhihirika kuwa mahojiano huwa na maswali elekezi ya kudadisi undani wa jambo fulani.
  Mahojiano yanaweza yakashirikisha mada mbalimbali kutegemea muktadha.

  Shughuli

  Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uwe na uwezo wa:
  i) kueleza maana ya mazungumzo
  ii) kutambua muundo na sifa za mazungumzo
  iii) kubainisha miktadha mbalimbali ya mazungumzo
  iv) kutambua umuhimu wa mazungumzo


  Tazama na kusikiliza mazungumzo A na B katika video hii. Tambua matukio yote katika shughuli hizi mbili.

  Video A Marafiki wawili wamekutana mtaani baada ya muda mrefu. Haya ni mazungumzo ya kirafiki kuhusu maisha yao ya hapo awali na ambavyo yameendelea.

  Video B Kuna mazungumzo kati ya wakulima wawili wanaokutana katika kituo cha malipo. Wanazungumza juu ya mavuno haba na malipo duni waliyopata kutokana na hali mbaya ya anga.
  Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

  (Mwalimu na mwanafunzi wako nje ya sebule ya walimu)

  Mwanafunzi: Shikamoo mwalimu.
  Mwalimu : Marahaba! U hali gani ?
  Mwanafunzi: Sina neno mwalimu ila ningependa kuomba msaada wako kuhusu hotuba na mazungumzo.
  Mwalimu : Shida yenyewe ni ipi?
  Mwanafunzi: Aaa;Aa;nimeshindwa kubaini tofauti kati ya vipengele hivi viwili.
  Mwalimu : (Akionyesha kushangaa) Lo! Kwani jana hukuwepo darasani tukijadili mambo haya?
  Mwanafunzi: Samahani mwalimu nilikuwa hospitalini kwa matibabu.
  Mwalimu : Pole, Utapata nafuu.
  Mwanafunzi : Ahsante, nishapoa.
  Mwalimu : Tofauti kuu kati ya hotuba na mazungumzo ni kwamba hotuba huwasilishwa na mtu mmoja kwa hadhira fulani nayo mazungumzo ni maongezi kati ya watu wawili au zaidi. Hotuba huchukua umbo la maelezo kuhusu jambo fulani ilhali mazungumzo huchukua umbo la kitamthilia.
  Mwanafunzi : Ahsante mwalimu, kunazo tofauti zingine?
  Mwalimu : Ndiyo, lugha inayotumiwa katika hotuba huwa na urasmi fulani, mazungumzo hutegemea muktadha. Lugha inayotumika hotelini haina urasmi ilhali ile itumikayo ofisini huwa na urasimu. mazungumzo katika hoteli,hospitali,kituo cha polisi na kadhalika. Mwanafunzi : (Anatabasamu) Nashukuru sana Mwalimu. Hakika umenitoa gizani.
  Mwalimu : Karibu. Nenda darasani udurusu zaidi.  SIFA ZA MAZUNGUMZO

  Nyimbo

  Wimbo ni utungo ulioundwa kwa maneno au sauti zilizoteuliwa kisanii na zenye utaratibu wa kimuziki.Sauti hizo hupanda na kushuka na kuibusha hisia fulani kwa mwimbaji na msikilizaji. Nyimbo hazizingatii kaida zote za ushairi kama ilivyo katika mashairi halisi.

  WIMBO WA TAIFA

  Umesikia na kuona nini ?
  Huu ni wimbo wa Taifa la Kenya, unaoimbwa katika shughuli rasmi za kitaifa kama vile :
  -katika sherehe na shughuli za kitaifa na kimataifa
  -wakati wa kupandisha bendera katika shule, vyuo na taasisi mbalimbali

  umuhimu wa wimbo wa taifa la Kenya

  hutambulisha taifa letu
  huibua hisia za uzalendo
  hukuza umoja
  hukuza na kuendeleza utamaduni
  ni ombi kwa Maulana
  hufunza maadili
  huzindua wananchi

  AINA ZA NYIMBO
  Kuna aina mbalimbali za nyimbo kama vile:


  -nyiso
  - hodiya/vave/wawe
  - sifo
  - mbolezi
  - nyimbo za kidini
  - nyimbo za kisiasa
  - nyimbo za mapenzi
  - nyimbo za kizalendo na kadhalika

  Ni nyimbo ambazo huimbwa na mlezi wa mtoto kwa sauti nyororo na mahadhi taratibu ili kumtuliza mtoto,kumwongoa au kumfanya alale.

  Nyimbo hizi hudhihirisha hisia za mlezi kwa mtoto.


  BEMBEZI

  Soma wimbo huu.

  Ukimpenda mwanao
  Na wa mwenzio umpende
  Wako ukimpa chenga
  Wa mwenzio chenjegele
  Humjui akufaaye
  Akupaye maji mbele
  Kilengelenge cha boga
  Kuti nazi kunoga
  Roho yataka kunoga
  Mkono wafanya woga


  Nyamaa mama nyamaa
  Nyamaa usilie mno
  Ukilia waniliza
  Wanikumbusha ukiwa
  Ukiwa wa baba na mama
  (Kutoka Kiswahili Fasaha ; Oxford University Press Waititu Francis, Ipara Isaac, Okaalo Bilha, Amina Vuzo)
  Umejifunza nini kuhusu sifa za wimbo?

  Nyiso

  Ni nyimbo zinazoimbwa wakati wa tohara na shughuli zingine za jandoni.
  Umuhimu wa Nyiso
  -hujasirisha
  -hukuza ukakamavu
  -hukuza maadili na kusuta
  -hukuza na hudumisha utamaduni
  -hukuza umoja
  -huburudisha
  -huhamasisha
  -hufaharisha

  Hodiya
  Hodiya ni nyimbo zinazoimbwa wakati wa kazi kwa mfano wawe/ vave huimbwa na wakulima, kimai huimbwa na wavuvi.
  Umuhimu wa Hodiya
  -Humtia shime anayefanya kazi
  -hubeza wavivu-
  -huonyesha jinsi wahusika wanavyoonea fahari kazi
  - huonyesha mtazamo wa jamii kuhusu kazi

  Sifo huimbwa kwa lengo la kusifu wahusika kwa sababu ya umaarufu unaotokana na ushujaa, cheo, kipawa cha pekee na mambo ambayo wameweza kayatekeleza.Sifo huhimiza wanajamii kuiga matendo yanayosifiwa, kufunza maadili na amali za jamii.


  NYIMBO ZA KIZALENDO

  Nyimbo za kizalendo ni nyimbo zinazoimbwa kudhihirisha uzalendo wa wananchi kwa taifa lao.
  Nyimbo hizi huhimiza upendo kwa taifa lao na ombi kwa Maulana kubariki nchi.Huhimiza maadili na amali za kijamii

  Mbolezi
  Nyimbo zinazoimbwa wakati wa matanga au maombolezi.

  Umuhimu wa Mbolezi

  -kufariji/kuliwaza waliofiwa,
  -huwapa tumaini walioachwa,
  -huonyesha imani ya jamii husika kuhusu maisha na kifo,
  -kumsifu mwendazake,na kutoa ushauri.


  Nyimbo za mapenzi
  Ni nyimbo zinazohimiza mapenzi.Nyimbo hizi zinaweza kuchukua mikondo mbalimbali.

  • Wapendanao huimba ili kuimarisha na kudumisha penzi lao.
  • Hali kadhalika huwasilisha hisia za kimapenzi.
  • Fauka ya hayo, hutumika kuwasilisha matarajio aliyo nayo mpenzi mmoja kwa mwingine.
  • Zinaweza pia kutumiwa ili kumsifu mpenzi.
  • Mpenzi asiyeridhika na maisha ya kimapenz humlalamikia mpenziwe kwa mateso ya kimapenzi anayompa.
  • Hali kadhalika humrai arekebishe ili hali iwe jinsi ilivyokuwa hapo awali.
  • Wanaotengana ambao wameshindwa kabisa kuvumiliana kwa hivyo hawana budi kuwachana.
  • Aghalabu huelezea maisha yalivyokuwa na namna hali ilivyo sasa baada ya penzi kunyauka.

  Nyimbo za chekechea

  Nyimbo za chekechea ni nyimbo zinazoimbwa na watoto wanapocheza.
  Umuhimu
  kujiburudisha
  kuwaleta pamoja
  kufunza maadili
  kusaidia katika kunyoosha viungo na kuimarisha afya
  kukuza ukakamavu na uwezo wa kujieleza
  hufunza lugha


  NYIMBO ZA KIDINI

  Nyimbo za kidini huimbwa ili kumtukuza Mwenyezi Mungu.
  Umuhimu wa Nyimbo za Kidini

  • Hudhihirisha imani ya wahusika kutegemea muktadha
  • nyenzo muhimu za kupitisha amali za kidini.
  • Maadili
  • Hutoa mafunzo kuhusu dini husika/ huelimisha
  • Hukuza imani ya wahusika
  • Huhamasisha waumini/ Humpa mwumini tumaini
  • Huliwaza

  NYIMBO ZA HARUSI

  Nyimbo za harusi huimbwa wakati wa sherehe za harusi.


  Umuhimu wa nyimbo za harusi

  • Husifu maharusi
  • Huwahamasisha maharusi kuhusu majukumu ya unyumba
  • Huhimiza umoja wa jamii husika
  • Huburudisha
  • Huhimiza heshima kwa asasi ya ndoa

  NYIMBO ZA KISIASA

  Nyimbo za kisiasa huimbwa ili kushawishi watu kisiasa.

  Umuhimu wa Nyimbo za Kisiasa

  • Kusifu au kushtumu viongozi wa kisiasa
  • Kusambaza cheche au mwamko wa kisiasa na propaganda hivyo kushawishi watu kufuata mkondo Fulani
  • Kuonyesha utesi dhidi ya dhuluma na ukandamizwaji
  • Kuleta watu pamoja kwa misingi ya kisiasa
  • Kuzomea uongozi mbaya

  SIFA ZA NYIMBO

  Ni wazi kuwa nyimbo huwa na sifa mbalimbali kwa mfano :


  1. Kuwa na mapigo ya sauti( huchukua muundo wa ushairi) ambapo kuna beti, mishororo,vina, mizani
  2. Hutumia tamathali za usemi kama vile mafumbo, jazanda, ishara (taashira),takiriri kwa mfano nyamaa mama nyamaa
  3. Nyimbo huweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi
  4. Nyimbo huambatana na ala za muziki
  5. Waimbaji aghalabu huwa na maleba
  6. Huambatana na miondoko
  7. Nyimbo kutegemea umri, jinsia,mazingira na muktadha


  • Nyimbo hutumiwa kuburudisha na kufurahisha
  • Nyimbo hufunza maadili
  • Uhifadhi utamaduni
  • Nyimbo huelimisha
  • Huhifadhi historia ya jamii
  • Nyimbo huliwaza na kufariji
  • Nyimbo hukuza umoja
  • Nyimbo husifu na kukashifu matendo.

  TANBIHI
  Umejifunza kuwa nyimbo zina umuhimu katika jamii. Aina za nyimbo hugawika kulingana muktadha, jinsia,na lengo .Umuhimu wa nyimbo hutokana na ujumbe uliomo katika wimbo wenyewe.
  Endelea kufanya utafiti zaidi kuhusu nyimbo.

  Ni nyimbo ambazo huimbwa na mlezi wa mtoto kwa sauti nyororo na mahadhi taratibu ili kumtuliza mtoto,kumwongoa au kumfanya alale.

  Nyimbo hizi hudhihirisha hisia za mlezi kwa mtoto.


  SHABAHA:
  Kufikia mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uwezo wa:
  i) kubainisha aina za nomino
  ii) kueleza sifa za kila aina ya nomino
  iii) kutumia kila aina ya nomino katika sentensi ipasavyo.

  choma -katika kitenzi choma tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume chomoa

  komea- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume komoa

  shona- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume shonoa

  tia- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati o katika mzizi ili kupata kinyume toa

  fuma- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati u katika mzizi ili kupata kinyume fumua

  kunja- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati ukatika mzizi ili kupata kinyume kunjua

  hama- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati i katika mzizi ili kupata kinyume hamia

  fukia- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati ukatika mzizi ili kupata kinyume fukua

  nuka- katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati i katika mzizi ili kupata kinyume nukia

  funika-katika kitenzi tunaongezea kiambishi tamati u katika mzizi ili kupata kinyume funua


  Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uweze:
  i) kueleza maana ya vinyume
  ii) kubadilisha kitenzi hadi kinyume chake
  iii) kutumia vinyume ipasavyo katika sentensi.


  KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
  Kusikiliza na kuzungumza ni stadi zinazoshirikisha shughuli za kimawasiliano na kimaingiliano kwa sababu mbalimbali katika miktadha tofauti tofauti na mazingira halisi.Katika kusikiliza na kuzungumza, matamshi yafaayo ni muhimu.

  Ufunzaji na ujifunzaji wa stadi hizi humpa mwanafunzi nyenzo za kuwasiliana, kuingiliana na kutagusana ili kutimiza mahitaji mbalimbali.


  Kwa mfano:
  1. Kujuliana hali
  2. Kupasha ujumbe  3. Kuelimisha


  4. Kuelekeza

  5. Kuzindua/Kuhamasisha


  6. Kuonya/kutahadharisha
  7. Kuhimiza/kushawishi  8. Kuliwaza
  9. Kutatua mizozo katika jamii


  10. Kutumbuiza


  Hitimisho Imetambulika wazi kuwa stadi ya kusikiliza na kuzungumza itakufaa sana maishani!


  Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

  For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

  Sample Coursework e-Content CD

  Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

  Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

  Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

  Install ADOBE Flash Player for Best Results

  For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

  Search

  Subject Menu