KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kuandika - Kiswahili Kidato Cha 3KUANDIKA
Stadi hii humwezesha mwanafunzi kuandika hati nadhifu zinazosomeka na tahajia sahihi. Stadi hii humwezesha mwanafunzi kuandika maandishi yenye mantiki, mtiririko wa mawazo, miundo sahihi ya sentensi na kuzingatia kanuni za utungaji.

 


Mdahalishi/Barua pepe

Barua za mdahalishi ni barua ambazo huandikwa na kutumwa kwa njia ya mdahalishi au mtandao wa intaneti au wavuti.Ili kuandika barua hizi,ni sharti kuwe na tarakilishi.Mwandishi au mwandikiwa pia huhitaji anwani ya mdahalishi.

Tazama picha ifuatavyo.

Watu wasioweza kupata tarakilishi za kibinafsi,hupata huduma hiyo katika mikahawa ya mdahalishi kama ulivyoona katika picha uliyotazama.

Video

Jinsi ya kutuma barua ya mdahalishi

Tazama video ifuatayo:

Kutokana na maendeleo ya kiteknologia,siku hizi kunazo hata simu ambazo zinaweza kutumiwa ili kutuma na kupokea barua za mdahalishi.

 

Faida za barua za Mdahalishi

Nukulishi/Kipepesi/Faksi

Nukulishi ni njia moja ya kutuma ujumbe kwa kutumia mtambo maalum.Mtambo huu huwezesha ujumbe huo ambao huwa umeandikwa kwa karatasi kupokelewa jinsi ilivyo katika nakala asilia.Katika kutuma ujumbe wa nukulishi,karatasi iliyo na maandishi hutiwa katika mtambo wa kutumia ujumbe na nakala yenye ujumbe huo huo hutokea kwa mpokeaji.Kuwepo kwa huduma ya nukulishi kunategemea kuwepo kwa nguvu za umeme na simu.Barua inayotumwa njia hii pia huweza kuitwa kipepesi au faksi.

Hata hivyo unapotumia nukulishi kutuma barua,jaribu kufanya ujumbe wako kuwa mfupi kadri uwezavyo, kwani gharama hupanda ikiwa barua yako ni ndefu.

 

Ujumbe wa Rununu

Ujumbe pia unaweza kutumwa kupitia simu tamba.Hii huitwa huduma ya ujumbe mfupi.Ujumbe mfupi huandikwa kwa rununu au simu tamba na kutumwa hadi kwa mtu mwingine ambaye ana simu tamba pia.

Umuhimu wa ujumbe wa rununu.


1.Ujumbe huu huokoa muda.Hutumia muda mfupi kuandika na
kupokea.
2.Ujumbe huu pia huokoa gharama.Ni nafuu sana.
3.Mawasiliano kupitia ujumbe huu hutokea kimya kimya bila
kuwabughudhi waliokaribu.
4.Ujumbe huu pia unaweza kuhifadhiwa katika simu kwa
marejeleo.

Namna ya kutuma ujumbe huu.
Hitimisho

Kuibuka kwa teknolojia ya habari na mawasiliano kumerahisisha na kuimarisha njia za kutuma na kupelekea ujumbe. Awali tarishi walitumwa kuwasilisha ujumbe na jambo hili lilikuwa na gharama na pia kupoteza muhimu. Ni muhimu kukumbuka kwamba kadiri teknolojia inavyoendelea kupanuka ndivyo njia bora zaidi za mawasiliano zinavyoibuka.

Shabaha


Kufikia mwisho wa kipindi hiki unatarajiwa kuwa na uwezo wa,
i) Kufafanua maana ya wasifu.
ii) Kueleza umuhimu wa wasifu.
iii)Kuandika wasifu kwa kuzingatia mtiririko mzuri kwa njia ya
kuvutia.

UTANGULIZI

Maana ya wasifu

Wasifu ni maelezo yaliyoandikwa na mtu kumhusu mtu mwingine, kitu au jambo.Huwa habari halisi kuhusu umaarufu, matendo au tabia za mtu, kitu au jambo. Maelezo haya yanaweza kumhusu mtu aliye hai au aliyeaga dunia. Pia wasifu huzungumzia umuhimu wa mtu katika jamii. Aghalabu huonyesha maisha ya mtu kuanzia utotoni hadi uzimani. Huzungumzia kuzaliwa, elimu, kazi, ndoa na wakati mwingine kifo cha mtu huyo. Wasifu husomwa wakati wa sherehe mbali mbali au uzinduzi wa kazi fulani.

Muundo wa Wasifu

1. Wasifu husimulia sifa nzuri au bora.
2. Lugha inayotumika ni ya kuvutia.
3. Maneno ya chuku hutumiwa kwa wingi.
4. Mawazo huendeleza kwa mtindo wa nadharia.
5. Hurejelea nafsi ya tatu.
6. Hutoa taswira ya kinachozungumzia.

Umuhimu wa wasifu

 

Umetambua kuwa wasifu huelezea sifa bora za mtu au kitu.Katika hali hii msomaji hupata mwelekeo mzuri na himizo la kutenda mambo mazuri.
Wasifu humburudisha msomaji na humwezesha kumjua mtu vyema anayezungumziwa pia wasifu huchangia pakubwa katika kukuza na kuimarisha lugha.

 


Namna ya kuandika Wasifu

Uandishi wa wasifu unahitaji uangalifu. Ni vyema kufanya utafiti ili kupata habari kamili juu ya mtu au kitu.

Habari muhimu zinazozingatiwa lazima ziangazie kuzaliwa, maumbile, elimu, kazi,uraibu, umaarufu, falsafa na huduma zake kwa jamii.

Maelezo huandikwa kinatharia katika mpangilio wa kiaya. Matendo na sifa zake hubainishwa kwa njia ya kipekee ili kuonyesha upekee.

Ni muhimu kuteua msamiati unaohusika na taaluma ya mtu anayerejelewa.
Tamathali za usemi hutumiwa ili kumshawishi msomaji na kudumisha taharuki.

Kauli za mhusika hunukuliwa hapa na pale ili kuonyesha umaarufu wake.
Lugha ya heshima hutumiwa kwa kuwa hadhira hutaka kuiga waliosoma kuhusu mtu huyo.

MFANO WA WASIFUHitimisho


Umejifunza kuwa wasifu huandikwa na mtu kuhusu mwingine au kitu. Inaweza kusifia mji, mnyama, kazi au jambo.
Kuna utaratibu wa kihatua katika kuendeleza uandishi wa wasifu. Wasifu hutumika katika hafla muhimu au katika uzinduzi wa kazi.

Shabaha


Kufikia mwisho wa kipindi kikuu hiki unapaswa kuwa na uwezo wa:


1. Kueleza maana ya tawasifu
2. Kuandika tawasifu iliyo na mtiririko wa mawazo
3. Kuandika tawasifu kwa kuzingatia muundo maalum
4. Kueleza umuhimu wa tawasifu

 

Maana ya Tawasifu

Tawasifu ni hali ya mtu kutoa maelezo yanayomhusu binafsi kwa kuyaandika yeye mwenyewe. Habari hizi huhusu maisha yake tangu kuzaliwa kwake hadi wakati huo. Uandishi huu unaweza kuwa wa mpangilio wa kinathari au maelezo kwa ufupi ili kutoa taswira ya kijumla. Katika kipindi hiki tutashughulikia tawasifu inayoandikwa kwa kifupi na ambayo hutumiwa kwa madhumini ya kuomba kazi. Tawasifu ya aina hii huambatanishwa na barua fupi.

 

 

Ufafanuzi

Maelezo haya yanafafanua maana ya tawasifu.

Tawasifu ni hali ya mtu kutoa maelezo yanayomhusu binafsi kwakuyaandika yeye mwenyewe. Habari hizi huhusu maisha yake tangu kuzaliwa kwake hadi wakati huo. Uandishi huu unaweza kuwa wa mpangilio wa kinatharia au maelezo kwa ufupi ili kutoa taswira ya kijumla. Katika kipindi hiki tutashughulikia tawasifu inayo andikwa kwa kifupi na ambayo hutumiwa kwa madhumini ya kuaomba kazi. Tawasifu ya aina hii huambatanishwa na barua fupi.

 


Umuhimu wa tawasifu


1. Maelezo ya kijumla kumhusu mtu hutolewa kwa muhtasari
na kwa muda mfupi.
2. Humwezesha mwajiri kufanya uamuzi ufaao.
3. Humwezesha mtu kuajiriwa kwa kazi inayomfaa.
4. Hubainisha kiwango cha elimu na ujuzi wa kazi.
5. Hurahisisha kupata habari zinazohitajika.
6. Huonyesha uzoefu au tajriba ya mtu.
7. Mwajiri ana uwezo wa kupata habari zaidi kumhusu mtu kwa
siri kwa kurejelea majina na anwani za wadhamini.

Maana ya Tawasifu
Tawasifu ni hali ya mtu kutoa maelezo yanayomhusu binafsi kwa kuyaandika yeye mwenyewe. Habari hizi huhusu maisha yake tangu kuzaliwa kwake hadi wakati huo. Uandishi huu unaweza kuwa wa mpangilio wa kinathari au maelezo kwa ufupi ili kutoa taswira ya kijumla. Katika kipindi hiki tutashughulikia tawasifu inayoandikwa kwa kifupi na ambayo hutumiwa kwa madhumini ya kuomba kazi. Tawasifu ya aina hii huambatanishwa na barua fupi.

Muundo wa tawasifu

Tawasifu huwa na mpangilio rasmi. Utaratibu wake umegawanywa katika vipengele kama vifuatavyo


Uandishi wa Tawasifu

Hitimisho


Umetambua kuwa tawasifu ni maelezo unayoyatoa wewe mwenyewe kujihusu na kuna mtindo wa kuandika. Tawasifu huandikwa kwa ufupi lakini ina maelezo muhimu kwa mtu anayetaka kufahamu mengi kukuhusu.
Umuhimu wa kumbukumbu ni:
1) Kuwakumbusha wahusika mambo yaliyozungumzwa.
2) Kufuatilia utekelezaji wa yaliyoafikiwa.
3) Huhifadhi habari.


Ajenda

Miongoni mwa mambo yanayopatikana chini ya ajenda ni:
i) Kufunguliwa kwa mkutano kwa njia ya maombi kutoka kwa
yeyote katika mkutano.
ii) Makaribisho na hotuba ya mwenyekiti.
iii) Kila ajenda ya mkutano huwa kumbukumbu.
Kuna utaratibu maalum za kuandika kumbukumbu kwa mfano,
i)Kumb/15/05/2006


Kumbukumbu hii hunukuliwa kufuatia tarehe,mwezi na mwaka.
Pia kama ni mkutano na kumbukumbu zinazoendelea, huanzia pale walipoachia kwa mfano,
96/2006 au 96/06
1. Herufi kubwa -mada katika kumbukumbu huandikwa kwa herufi kubwa kwa mfano,

Kumb: 96/06 MAENDELEO YA SHULE
2. Mfuatano wa vipengele-Ni muhimu vipengele vinavyohusu mada kufuatana km
a) Kusomwa na kuthibitishwa kumbukumbu.
b) Yaliyotokana na kumbukumbu hizo.
c) Ajenda ya siku.
d) Shughuli nyinginezo.
3. Kufungua mkutano-Huja baada ya shughuli zote kumalizika na huonyesha saa ya kumalizika mkutano.Pia huonyesha siku ya mkutano mwingine.


4. Sehemu ya sahihi-Nafasi huachwa ili kutiwa sahihi na katibu na mwenyekiti.

 

Hitimisho
Uandishi wa kumbukumbu uhitaji uwe makini,umudu stadi za usikizi,ufupisho,uchanganuzi na uhariri.

Aina za Ripoti

Kuna aina mbili za ripoti

1) Ripoti za kawaida
2) Ripoti rasmi

Ripoti za kawaida
ni zile zinazohusu shughuli za kawaida. Kwa mfano, Shughuli za chama cha Kiswahili shuleni au chama cha sayansi pia ripoti kuhusu safari za wanafunzi kuvinjari mahali tofauti tofauti huwa ni ripoti ya kawaida.
Ripoti kuhusu yaliyotokea katika siku ya michezo pia ni ripoti ya kawaida.


Ripoti Rasmi

Hizi ni ripoti ambazo hufuata utaratibu wa kufanya utafiti kuhusu jambo fulani na kutoa mapendekezo.
Nyingi ya ripoti rasmi huwa zinatakiwa na serikali. Mifano ya ripoti rasmi huwa ni kama ripoti za tume za uchunguzi za Rais, ripoti za tume zinazotakiwa na mawaziri au maafisa wa juu serikalini.
Baadhi ya ripoti nchini Kenya ni,
1) Ripoti ya wizara ya elimu kuhusu migomo ya wanafunzi
shuleni
2) Tume kuhusu uabudu wa shetani shuleni.
3) Tume kuhusu mfumo wa elimu wa 8-4-4 na kadhalika


Sehemu za ripoti

Mfano wa ripoti ya kawaida

Ripoti ya shughuli za chama cha Kiswahili cha shule ya Mukameni


Utangulizi

Mwaka huu chama kilikuwa na shughuli nyingi na wanachama walijitolea, nao wanakamati walifanya kazi kwa hiari kubwa.
Waliokuwa wanakamati
1) Ayub Hassan - Mwenyekiti
2) Kesiah Mtaalamu - Naibu Mwenyekiti
3) Harriet Nyambura - Katibu
4) Boniface Onyango - Mweka hazina
5) Katee Mulwa - Katibu mtendaji
6) Yapande Bungei - Naibu wa katibu
7) Zodak Wafula - Mwanachama maalum.

Shughuli za Chama 2010
i) Kusajili wanachama wapya
Chama kiliwasajili wanachama wapya sitini. Hii ilikuwa ndiyo
idadi kubwa zaidi ya wanachama kusajiliwa mara moja tangu
chama kianzishwe.
ii) Safari ya Mombasa
Katika mwezi wa tatu wanachama walisafiri hadi Mombasa
kujionea maeneo yenye umuhimu wa kihistoria kwa Kiswahili
kama vile 'Ngome ya Fort Jesus'
iii) Kuigiza Mchezo wa kifo kisimani
Wanachama waliweza kuigiza mchezo wa kifo Kisimani katika
siku ya elimu ya wilaya.Mkuu wa wilaya alifurahishwa mno na
uigizaji wa wanachama wetu.
iv) Kuandika mchezo
Katika mwezi wa juni wanachama waliandika mchezo waliouita
'Tamaa'. Mchezo huu ulishinda katika kiwango cha tarafa
katika mashindao ya mchezo ya kuigiza.
v) Shindano la uandishi wa Insha
Katika mwezi wa Julai chama kiliandaa shindano la uandishi
kwa wanafunzi wote katika shule.Mshindi alituzwa tuzo.
vi) Karamu kwa wanachama
Wanachama waliweza kuwaandalia wanachama wanaoondoka
karamu murwa.

Hitimisho
Chama kiliweza kupata mafanikio makubwa mwaka huu. Wanachama walipata mshawashamkubwa na wana hiari kubwa ya kuendelea na shughuli mwaka wa 2011.
Ripoti imeandikwa na,

KEZIAH MTAALAMU
KATIBU
12-11-2010Mfano wa Ripoti rasmi

RIPOTI KWA MKUU WA AFYA WILAYANI CHAMBONI KUHUSU KUZUKA NA KUENEA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.

Utangulizi
Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa kipindundu katika wilaya ya chamboni mkuu wa afya wilayani aliunda kamati ya watu watano kuchunguza chanzo na kupendekeza njia za kudhibiti maenezi ya ugonjwa huo.

Waliohusika walikuwa
1) Kiprotichi Keter - Mwenyekiti
2) Dkt Maria Wekesa - Katibu
3) Paul Auma - Mwanachama
4) Siti Saidi - Mwanachama
5) Yui Kasangi - Mwanachama

Utaratibu uliofuatwa
Wanachama waliweza kutembelea mahali kadhaa na kujionea hali ilivyokuwa.Waliwahoji wakazi na kuwapa hojaji baadhi yao ili kuijaza.

Waliweza pia kurejelea kumbukumbu katika maktaba ya Mkuu wa Afya Wilayani.


Matokeo
a)
Maeneo ya sokoni
Wanakamati walitembelea masoko kadhaa na kujionea hali ilivyokuwa. Walitambua maeneo mengi ya masoko yalikuwa chafu sana.Panya na nzi walijazana kila mahali.

b) Mikahawa
Kamati ilitembelea maeneo ya mikahawa na kujionea hali ya uchafu uliokithiri katika maeneo hayo. Takataka zilitupwa ovyo ovyo nje. Katika mikahawa mingi vyakula vilikuwa vimetupwa ovyo ovyo. Nzi na kombamwiko walijazana mikahawani na wengine kutumbikia kwenye chakula kisichofunikwa.

c) Vyoo
Wanakamati walitambua kuwa mikahawa mingi na hata masoko mengi katika wilaya hayakuwa na vyoo. Pia wengi wa wakaazi walikuwa wakijisaidia kwenye misitu. Hali hii ilichangia sana kuenea kwa ugonjwa huu
.

d) Mabiwi ya takataka
Kamati ilitambua kuwa masoko mengi hayakuwa na mabiwi ya takataka nahivyo takataka zilitupwa ovyo ovyo sokoni.
Mabiwi machache yaliyoonekana yalikuwa yamejaa na yalikuwa yakito harufu mbaya sana.

e) Maji
Kamati ilitambua kuwa waaji walitumia maji yasiyo safi kutoka kwenye mabwawa. Wakaazi walitega maji na kuyanywa bila ya kuchemsha.

f) Kunawa mikono
Kamati ilitambua kuwa wakaazi wengi huwa hawanawi mikono wakati wanapotoka haja na kabla ya kula.

g) Vyakula vinavyopikiwa katika majengo wazi
Wanakamati walijionea chakula kikipikwa sehemu wazi. Hali ya usafi haikuwa ikizingatiwa.

Mapendekezo
Kufuatia utafiti wa kina wa kamati hii tunapendekeza yafuatayo

i) Maeneo ya soko yafungwe na yasafishwe.Wanyama na wadudu katika masoko wauliwe mara moja.
ii) Mikahawa
Mikahawa yote ifungwe mara moja hadi wenyewe wahakikishe usafi.
iii)Vyoo
Kila soko lijengwe vyoo kadhaa ili kudumisha hali ya usafi na kupunguza kasi ya maenezi. Kila mkahawa sharti uwer na vyoo viwili.
iv)Taka
Taka katika mabiwi ziondolewe kila siku pia baraza la mji lihakikishe kuwa kila soko lina mabiwi kadhaa.
v) Wakazi
Wakazi waelimishwe kuhusu kuchemsha au kuyatibu maji kabla ya kuyanywa. Pia baraza la mji lihakikishe kuwa limewapa wakaazi maji safi ya kunywa.
Wakazi pia waelimishwe kuhusu umuhimu wa kunawa mikono kila wakati wanapotoka haja na kabla ya kula.
vi) Uuzaji wa matunda masokoni na upikaji wa vyakula katika maeneo wazi upigwe marufuku mara moja hadi hali hii ya maenezi idhibitiwe.


Hitimisho

Kamati hii inaonelea kuwa iwapo hatua zilizopendekezwa zitazingatiwa hali ya maenezi ya ugonjwa wa kipindupindu itadhibitiwa.Hali hii pia itazuiwa kutokea tena. Kamati inaamini imefanya utafiti wa kina na inatoa shukrani kwa Mkuu wa Afya wilayani kwa kuipa nafasi ya kutekeleza jukumu hili.
Dkt Maria Wekesa Kiprotich Keter
Katibu Mwenyekiti.

Tarehe 17/08/2010


 

Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu