KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kusikiliza na kuzungumza - Kiswahili Kidato Cha 3

Kusikiliza na Kuzungumza

Ni stadi inayomwezesha mwanafunzi kustawisha mawasiliano kwa ufasaha kutegemea miktadha mbalimbali, kuimarisha usikilizaji, ufahamu, ubunifu, ukusanyaji, uchambuzi, na utendaji wa kazi mbali mbali za kisanaa. Baada ya kujifunza stadi hii mwanafunzi anatarajiwa kuzingatia maadili yafaayo katika jamii na kuona fahari kutumia lugha ya Kiswahili.

Tazama mifano ifuatayo.SHUGHULI

Katika sehemu hii,utapata maelezo zaidi juu ya somo husika. Bonyeza mada yoyote kati ya zilizoorodheshwa ili ufaidi!

Baada ya kipindi hiki unatarajiwa kuwa na uwezo wa
i) Kutambua sifa za sajili ya ofisini kwa mtawala na
mahamakani
ii) Kutumia lugha ipasavyo katika mazingira ya ofisi ya utawala
na mahakamani
iii) Kustawisha mawasiliano kwa kuzingatia lugha fasaha katika
mazingira mbalimbali.


Katika sehemu hii, unatakiwa kubonyeza mazoezi yaliyoorodheshwa ili uweze kujipima iwapo umeyapata yaliyofunzwa katika somo. Vilevile, unaweza kuupima uelewaji wako wa mada hata kabla hujashughulikia mafunzo ili uweze kujua unayopaswa kutilia mkazo zaidi.

MAAMKIZI NA MAZUNGUMZO

maamkizi ya heshima

Tazama video ifuatayo


Maamkizi ya heshima katika mazingira ya ofisini kwa mtawala

Utangulizi
Kusikiliza ni hali ya kuwa makini kwa linalosemwa au kuelezwa na msemaji. Kudadisi ni hali ya kutaka kujua undani wa jambo au hali fulani. Katika kudadisi unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchambua umuhimu wa fasihi simulizi ambao utashughulikiwa katika mada hii. Unatarajiwa kusikiliza na kuhoji aina tofauti za fasihi simulizi kwa mfano,methali,vitendawili,miundo, sifa, maana, mafunzo na maadili
Ni muhimu kwako kufahamu muainisho wa fasihi simulizi,miundo na majukumu ya kila mojawapo ya tanzu za fasihi simulizi.Inafaa utambue kuwa fasihi simulizi ina umuhimu katika maisha yako ya kila siku kwa jumla.


maamkizi ya heshima

Ofisini kwa MtawalaUmeona nini na kusikia nini?

Imebainika wazi kuwa hapa ni ofisini kwa mtawala.

Unaweza kutambua sifa za matumizi ya lugha baina ya watu hawa watatu?

Baadhi ya sifa ni:
i) Kuchanganya ndimi-kwa mfano...that is very serious
ii) Lugha ya kuamrisha kwa mfano...nataka hatua zichukuliwe
mara moja!
iii) Lugha ya vitisho (ukali)-;lini Bwana OCS?
iv) Lugha hisishi -;kwa mfano Oho!, Lo!
v) Lugha ya mdokezo kwa mfano, na...Mwalimu na mwanafunzi

Imedhihirika kuwa sajili ya ofisi kwa mtawala ina sifa zake. Baadhi ya sifa hizi ni:

 • Lugha yafaa iwe ya upole au unyenyekevu.
 • Lugha sharti ionyeshe heshima na staha.
 • Lugha iwe na msamiati maalum kutegemea mada.
 • Aghalabu huwa lugha ya  amri au ukali kutegemea jambo husika.
 • Mtawala anapaswa kuwa na ufasaha na usanifu wa lugha.
 • Lugha isiwe na mafumbo bali iwe ya wazi kuwezesha mawasiliano.
 • Lugha isiwe ya kiburi au dharau.
 • Mtawala anapaswa kutumia lugha ya ushawishi.
 • Lugha hii yaweza kuonyesha hisia.
 • Aghalabu kuna kuchanganya ndimi ili kusisitiza jambo.

Hitimisho

Imedhihirika kuwa sajili ya ofisi kwa mtawala ina sifa zake. Baadhi ya sifa hizi ni:

(Blink the following statements)

? Lugha yafaa iwe ya upole au unyenyekevu
? Lugha sharti ionyeshe heshima na staha
? Lugha iwe na msamiati maalum kutegemea mada
? Aghalabu huwa lugha ya amri au ukali kutegemea jambo husika
? Mtawala anapaswa kuwa na ufasaha na usanifu wa lugha
? Lugha isiwe na mafumbo bali iwe ya wazi kuwezesha mawasiliano
? Lugha isiwe ya kiburi au dharau
? Mtawala anapaswa kutumia lugha ya ushawishi

 

Mahakamani


Kortini

 

Maelezo


Sajili ya mahakamani ina sifa maalum. Baadhi ya sifa hizi ni:

i) Huwa na maelezo marefu naya kimzunguko ili kuhakikisha ukweli na ukamilifu wa jambo.
ii) Msamiati wake hurejelea vifungu vya sheria.
iii) Aidha msamiati huwa maalum kwa mfano, wakili, kiongozi wa mashtaka, karani, rufani, kukata kesi, kukata rufani, kuweka dhamana na kadhalika.
iv) Lugha huwa ya heshima, kwa mfano Mheshimiwa
v) Huwa na matumizi ya lugha ya kukopwa, kwa mfano, interparte, ex officio, amicus curie
vi) Huwa pia na unyenyekevu wa hali ya juu, kwa mfano, nakiri nilifanya kosa na naomba mahakama hii inisamehe.
vii) Lugha ya mafumbo huwa haitumiki
viii) Lugha huwa sanifu
ix) Lugha huwa rasmi na inapobidi lugha zingine hutumiwa na kukalimaniwa au kutafsiri
x) Misamiati ya kawaida wakati mwingine hufasiriwa kwa maana mpya kwa nyumba na nyumbani.


 

HITIMISHO
Ni muhimu kufahamu sajili mbali mbali za lugha kwa sababu zitakuwezesha kuwasiliana ipasavyo katika shughuli za kila siku. Vile vile, ufahamu wa sajili hukuza uelewano katika jamii na kuhimiza utangamano.

 

Shabaha:
Kufikia mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uwezo wa
i) Kubainisha maudhui ya mahojiano yanayoafiki muktadha
fulani.
ii) Kutambua sifa za sajili ya mahojiano baina ya wataalamu.
iii)Kushiriki kikamilifu katika mahojiano yanahusu taaluma
mbalimbalimahojiano baina ya wataalamu wawili


Mazungumzo haya ni baina ya nani na nani?

Hawa ni madaktari. Mmoja ni mtaalamu wa upasuaji na mwingine ni mtaalamu wa maswala ya filamu za uyoka.Kuna kuulizana maswali baina yao.

Tazama video na kusikiliza mazungumzo kwa makini


Mahojiano haya ni kati ya wataalamu wa aina gani?
Hawa ni wataalamu wa zaraa au kilimo. Wanazungumzia uimarishaji wa kilimo katika nchi yao.


 


SHABAHA:

Kufikia mwisho wa kipindi hiki unatarajiwa uweze :
1. Kubainisha maswala ibuka kupitia mada mbalimbali.
2. Kujadili kwa upana na urefu kuhusu mada hizo.
3. Kujieleza kwa ufasaha kuhusu mada hizo.
Hebu tazama video ifuatayo:Mijadala pia huweza kufanywa kwa kutoa na kufafanua hoja kuhusu mada Fulani ili kuonyesha msimamo linalozungumziwa bila ya kuwa na pande mbili. Tazama video ifuatayo:


Hitimisho
Mjadala ni muhimu zaidi kwa vile humsaidia msemaji kueleza kauli zake na kuzitetea ili aeleweke vyema na msikilizaji wake. Aidha mjadala huweza kupanua upeo wa kimawazo wa washiriki.

SHABAHA:
Kufikia mwisho wa kipindi hiki:
1) Uweze kusikiliza ufahamu kwa makini na kujibu maswali
2) Uweze kutambua ujumbe muhimu katika vifungu vya
ufahamu
3) Uweze kutambua miktadha katika taarifa za kusikilizwa


Tazama na kusikiliza yanayosemwa kisha ujibu maswali baadaye.


Hitimisho
Katika kipindi hiki tumeshughulikia ufahamu wa kusikiliza.
Inafahamika kwamba ufahamu ni kifungu unachopewa na ambacho huwa na maswali. Maswali haya hukusudiwa kuupima uwezo wako wa kuyaelewa yaliyosemwa, jinsi yanavyosemwa na mafunzo katika ufahamu wenyewe.
Kila mara, hakikisha kwamba;
i)Umelipata wazo kuu la taarifa kwa kuisikiliza kwa makini.
ii)Umeyachunguza maswali yaliyoulizwa kuhusu ufahamu.
iii)Umesikiliza tena taratibu na kwa makini ili kuelewa kwa
undani.
iv)Umejibu maswali kwa kikamilifu. Aghalabu, majibu ya maswali
haya hutokana na taarifa uliyopewa.


UTANGULIZI
Neno dhima lina maana ya wajibu mkubwa,madaraka au jukumu. Dhima ya fasihi simulizi inahusu majukumu au wajibu unaotekelezwa na fasihi simulizi kwa binadamu katika jamii; kama ilivyo kwamba fasihi ni kioo cha jamii. Miongoni mwa dhima katika fasihi simulizi ni kama zifuatazo:
Kuburudisha
kuelimisha
kuhifadhi na kukuza utamaduni
kukuza na kuendeleza stadi za lugha
kuipa jamii mwelekeo

Shabaha
Kufikia mwisho wa somo hili, mwanafunzi aweze:
1. Kufafanua maana ya Fasihi simulizi.
2. Kutaja na kueleza umuhimu wa fasihi simulizi katika jamii.


Kusikiliza na kudadisi


Umuhimu wa Fasihi simulizi


Ni muhimu kuelewa kuwa fasihi simulizi ilikuwapo tangu jadi kabla ya fasihi andishi.Fasihi hii hushughulikia masuala ya maisha ya binadamu kwa jumla na jinsi binadamu anavyoingiliana na mazingira yake. Binadamu alianza kueleza hisia na matamanio yake kwa njia mbalimbali. Katika kutekeleza haya, aliweza kupata burudani, kuelimika, kupata mwelekeo, kukuza lugha na mambo mengine mengi kuhusiana na utamaduni wake.


1. Kuburudisha

Fasihi simulizi huchangamsha wanajamii na kuwaondolea uchovu baada ya shughuli muhimu za siku. Burudani hii yaweza kupatikana kupitia kwa ngoma, ngano, vitendawili, vichekesho na michezo ya kuigiza.

Hebu tazama video ifuatayo.

Kama tunavyoona katika video, hadhira inaburudika kutokana na ngoma ndiposa wanashangilia kwa kupiga makofi. Aidha, nyuso zao zinaonyesha furaha.

Mbali na kupiga makofi, hadhira huweza hata kujumuika na watumbuizaji katika ngoma.

Hebu tazama video ifuatayo na jinsi hadhira inavyoburudika kiasi cha kujumuika na wachezaji.Katika burudani, watu pia huweza kusikiza muziki wakibarizi.

Hebu tazama kibonzo kifuatacho.Kama bwana huyu anavyoonekana,anaburudika kwa kusikiliza muziki baada ya kuogelea.Kuelimisha

Mbali na kuburudisha, fasihi simulizi ina dhima ya kuelimisha. Katika kuelimisha, fasihi simulizi huwajulisha wanajamii mambo ya usuli na utamaduni. Pia fasihi simulizi huijuza hadhira mambo ambayo kwayo ni mapya na hivyo kuwaongezea maarifa. Miongoni mwa tanzu zinazoelimisha ni pamoja na methali, vitendawili na masimulizi. Hebu tazama picha ifuatayo:Katika picha hii, wanafunzi wanajifunza kuwa yeyote anayeamka mapema na kufanya kazi fulani kwa bidii hupata kufanikiwa.Tazama video ifuatayo.Katika video hii, wanafunzi wanajifunzi kuhusu mazingira kwa vile wanaelimishwa kuhusu mazingira wanapojuzwa maumbile ya kobe anayepatikana katika mazingira.


 

Kuhifadhi na kukuza utamaduni
Fasihi simulizi pia ni njia ya kuhifadhi amali zote za kijamii. Amali hizi hupokewa kwa kizazi kipya kupitia hafla mbalimbali. Wanajamii hupata fursa ya kuelewa mambo ya kitamaduni na kihistoria. Miongoni mwa shughuli za kuhifadhi na kuendeleza utamaduni ni sherehe za jando, kuwapa watoto majina, harusi, mazishi na kadhalika. Tazama video ifuatayo:


Umeona na kusikia nini?
Katika jamii husika watoto walipewa majina kwa mujibu wa desturi za jamii hiyo. Lilikuwa ni jukumu la wazee kufanya hivyo . Endapo mtoto hakupewa jina kwa utaratibu huu alikuwa akilia lia kana kwamba ni mgonjwa.

 

Kukuza na kuendeleza stadi za lugha
Umuhimu mwingine wa fasihi simulizi ni kukuza na kustawisha stadi za lugha. Kwa kuwa lugha huwa kiungo muhimu cha kwasilishia kazi za fasihi. Stadi mbalimbali huibuliwa na kutumiwa na wasanii na hivyo ndivyo lugha huendelea kukua. Tamathali za usemi, vitanza ndimi, masimulizi na ukariri wa mashairi ni miongoni mwa njia zinazotumika kuimarisha lugha.

Sikiza vitanza ndimi vifuatavyo.
1. Upo upo papo hapo ulipo
2. Kikukasirishacho wewe ndicho kinikasirishacho mimi
3. Wavuvi walivua wavivu walifua wafu kwa wavuMisemo

Msemo Maana
1. Pekecha ugomvi - chochea ugomvi kati ya watu
2. Kuonea gere - kumwonea mtu wivu
3. Teka bakunja - teka fikira au akili ya mtu
4. Kaa doria - kuwa tayari kutekeleza wajibu
5. Tema umombo - kuzungumza kiingereza kwa ufasaha

Kuipa jamii mwelekeo
Kupitia tanzu mbalimbali za fasihi simulizi, jamii hupata kuelekezwa kwa njia mbalimbali kuhusu namna ya kuyatekeleza mambo fulani. Wanajamii hujifunza kaida za jamii, kwa mfano sherehe za jando, unyago, harusi na mazishi. Wao huelewa taratibu zote za kufanya jambo fulani na sababu za kufanya hivyo. Kwa mfano:
Katika jamii za waswahili wasichana walifunzwa mambo ya unyumba na nyanya zao kabla ya kuolewa. Utaratibu fulani ulifuatwa hatua hadi hatua.
Aidha,jamii ya waluo walifanya sherehe ya mazishi kwa njia ya kipekee.

Hitimisho

Umuhimu wa fasihi simulizi unaweza kuelezwa kwa mapana.Mbali na hoja zilizojadiliwa,zifuatazo zinaweza kujumuishwa.kwa mfano, kuhifadhi historia, kuunganisha watu,kukuza uzalendo na vipawa vya ubunifu,kuliwaza,kuhimiza na kuchangia katika fasihi andishi

Shabaha

Baada ya kipindi,unatarajiwa kuweza:
1.Kueleza maana ya malumbano ya utani.
2.kueleza sifa za malumbano ya utani.
3.Kufafanua umuhimu wa malumbano ya utani


 


Malumbano ya utani
Malumbano ya utani ni mazungumzo ya kujibizana baina ya watu wawili au zaidi yanayohusu kufanyiana mzaha na ambayo hukusudia kuleta ucheshi kwa wahusika.Soma mfano huu wa malumbano ya utani.
  Mjukuu: (Akibisha)Hodi , Hodi !huku;..wenyewe hawapo?
  Nyanya: (Akifikiria)karibu ndani,
  Mjukuu: (Akiiga sauti ya nyanya)karibu  ndani hutaki kunilaki?
  Nyanya: (Akicheka)Ah! mume wangu!Ni wewe,karibu
  Mjukuu: Bibi wee! Mwenyewe boma  hukaribishwa kwake?
  Nyanya: La hasha! Bwanangu hebu nikutue  mzigo  .
  Mjukuu:Mtu keshafika kwake hakuna haja ya  makaribisho zaidi
au vipi?
  Nyanya: Naam! Lakini rundo lote hili la vitabu litakukondesha
bure mume wangu He!
  Mjukuu: Wamaanisha nini haswa Bibiye?
  Nyanya:Mume wangu ukija nyumbani ni ule  ustarehe unone sio
masomo la sivyo (kinaya kifupi) nitarudi kwetu.
  Mjukuu: (Akicheka) urudi kwenu?mahari nayo  je?
  Nyanya: ukija nyumbani sio vitabu mchana kutwa  ,usiku kucha
nataka tukae tuzuungumze kama bibi na bwana.
  (wote wakicheka)


Mfano wa Pili
Utani kati ya makabila tofauti .
    Mutua: Vipi  mtani ?Bado mmekatalia milimani?
    Mwasi: Wacha  kuniita mtani maana mimi si mtani wako.
    Mutua :Kwa nini?kwani umesahau kuwa tuliwaita kisha
mkakataa kutufuata?
    Mwasi: Eh bwana we!ndiyo maana tunaitwa
wataita.Endeleeni kutuita ng'o hatutaitikia.
   Mutua: Haya basi tutaacha kuwaita bakini milimani.

Mfano wa tatu
Utani kati ya marafiki(Juma na Ali wakitaniana mjini gezaulole)
  Juma: Hujambo bwana Juma ?
  Ali: Sijambo Ali
  Juma: vipi Juma kwani bibi amekufungia kama  kuku siku hizi?
  Ali: kwa nini?
  Juma :Huonekani kabisa!
  Ali:Hunioni kwa kuwa umezima taa?
  Juma : Nitafanyaje basi hata nikuone?
  Ali: Washa taa utaniona.
  (Wanapeana  mikono huku wakicheka.Wanaendelea na mazungumzo yao)

Mfano wa Nne
  Malumbano ya utani kati ya mashemeji.
  Yohana: Habari za asubuhi?
  Maria : Bwana wee!utaziweza?
  Yohana:Mbona siku hizi,umeniacha njaa hivi?
  Maria: Tumbo lako limekuwa kama bahari  halijai.Labda litajaa ukipikiwa chakula chote hapa nyumbani.

  Yohana: Naona umeshindwa na kazi yako  nitakurudisha kwenu nioe mwingine.
  Maria: Hilo tu,utanipumzisha kazi ya  kujaza kiriba.
Katika mifano uliotazama,inabainika kuwa kuna aina mbali mbali za malumbano  ya utani.  Malumbano ya utani  pia huhusisha jamii, kwa  mfano Wataita na Wakamba.


Maana ya Ulumbi

Ulumbi ni mazungumzo yanayowasilishwa kwa hadhira kwa uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee.

SHABAHA
Baada ya kipindi,unatarajiwa kuweza:
1.Kueleza maana ya ulumbi.
2.Kueleza sifa za mlumbi mwema.
3.Kuweza kuzungumza kwa ufasaha kwa kuiga walumbi.

SHABAHA


Baada ya kipindi,unatarajiwa kuweza:
1.Kueleza maana ya ulumbi.
2.Kueleza sifa za ulumbi .
3.kufafanua umuhimu wa ulumbi.


Sifa za Ulumbi
1. Ni usemaji au uzungumzaji wa kifasaha
2. Hubainika katika utoaji wa hotuba
3. Hutumia chuku huku ukidumisha adabu
4. Huwa na urudiaji mwingi wa maneno ili kusisitiza
5. Huhitaji ufahamu mzuri wa jamii husika

 

Umuhimu wa ulumbi
a. Hukuza uwezo wa kujieleza hadharani
b. Hukuza ujuzi na ufasaha wa lugha
c. Ni kigezo cha kuteulia viongozi wa baadaye
d. Huhifadhi utamaduni wa jamii
e. Ni nyenzo ya kuburudisha wanajamii
f. Ni nyenzo ya kuwaelimisha bila ya kuchosha
g. Hukuza uzalendohauwezi kutumiwa kuwasilisha ujumbe
muhimu
h. Ni kitambulisho cha utabaka
i. Ni msingi wa kuheshimiwa katika jamii


Sifa za malumbano ya utani.


Hufanywa na watu wawili au makundi mawili ya watu.
Hutumia tamathali za usemi kwa mfano chuku
Huwa hayana mazimio kabisa
Huwa ni majibizano
Huwa na vichekesho
Waweza kujumuisha watu wa umri mbali mbali..

Umuhimu wa malumbano ya utani

Malumbano ya utani yana umuhimu hufuatayo,

Hukuza uhusiano mzuri kati ya watu .

Huburudisha kwa vile huwa yamejaa ucheshi.

Huelimisha watu.

Hukosoa,hukashifu,huonya.

Hukuza maadili katika jamii husika.

Hukuuza ukakamavu.

HITIMISHO
Malumbano ya utani hukuza utangamano kati ya watu.Pale ambapo malumbano haya yatazua mizozo huwa yamepotoka.Ni vyema kutaniana bila ya kukusidia kuumizana.

Kufikia mwisho wa somo unatarajiwa uweze,
1. Kueleza maana ya visasili.
2. Kueleza sifa na umuhimu wa visasili.
3. Kutoa mfano wa kisasili.

Maana
Visaasili ni visa vinavyosimulia asili au mianzo ya matendo fulani yasiyoeleweka katika hali ya kawaida. Huelezea imani na mtazamo wa jamii kuhusu historia,desturi,na matukio katika jamii hizi.
Visaasili hufafanua chanzo na maana ya mambo kutokea au kuwepo. Mathalani asili ya watu,kifo,matukio fulani katika jamii.


sifa za visa asili


i) Huwa na mianzo na miishio maalum,
kwa mfano, Hapo zamani za kale..
ii) Hueleza matukio ya jadi kwa mfano, asili ya watu, kitu,
kufanya kazi, kula na kadhalika.
iii) Hueleza imani pamoja na desturi za jamii. Huelezea misimu,
miungu yenye uwezo mkubwa wa kusababisha mambo na
uliopita wa binadamu.
iv) Huchukuliwa na jamii husika kuwa ni kweli.
v) Mandhari ya visa asili huwa si ya kawaida kwa mfano,
madhari ya milima
vi) Wahusika huwa na aina mbali mbali kwa mfano, binadamu
wanyama au hata miungu
vii) Wahusika huwa bapa; hawabadiliki

Umuhimu wa Visa Asili


i)Husaidia binadamu kuelezea matukio ya ajabu kwa mfano asili
ya kifo, kulala, mchana na usiku.
ii)Huhifadhi utamaduni wa jamii
iii) Visa asili huweza kuwaliwaza wanajamii Kwa mfano,
kunapotokea kifo kwa kuwa huelezea kuwa kifo ni jambo
linalozidi uwezo wa binadamu, au ni jambo la faradhi.
iv)Hueleza utaratibu wa kuitekeleza desturi kama vile jinsi ya
kutoa kafara.
v)Baadhi yake huwa ndio msingi wa kuhalalishwa kwa baadhi ya
mila na desturi za jamii kwa mfano,utoaji mahari, watoto
kunasibishwa na mzazi wa kike katika baadhi ya jamii na
kadhalika
vi) Husaidia kukita mizizi ya imani katika jamii

Hitimisho
Visaasili vinaweza kufungamana na historia ya jamii na kueleza dhana nzito katika jamii.kwa mfano Kifo.
Visaasili hutofautiana na ngano za usuli kwa kuwa zile za usuli huelezea mambo mepesi kama vile chanzo cha tabia fulani,maumbile ya vitu fulani kwa mfano, sungura kuwa na masikio marefu,wanyama fulani kuwa na ngozi laini au ngumu.

Kufikia mwisho wa somo uweze;

 1.  Kueleza maana ya ngano.
 2. Kufafanua sifa na umuhimu wa ngano.
 3. kutambua  na kufafanua aina za ngano.

Maana
Ngano ni hadithi za kubuni zisizokuwa na ukweli zenye kutoa mafunzo muhimu katika jamii.

 


Sifa za ngano

i. Hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya
mdomo
ii. Ni za kubuni
iii. Si za kweli
iv. Hushirikisha vipera vingine vya fasihi, kwa mfano nyimbo
v. Huhusisha hadhira, mfano makofi,kuimba,kucheka.
vi. Huwa na fomula maalum ya kuwasilisha.
vii. Hutumia tamathali nyingi za usemi.


Kuna aina zifuatazo za ngano
Hurafa au ngano za wanyama

Ni hadithi ambazo wahusika huwa wanyama au ndege ambao hupewa uwezo wa kutenda na kuzungumza kama binadamu.


Ngano za Hekaya/wafanya/kiayari


3. Ngano za mtanzikoNgano za mazimwi na Ngano za usuliUmuhimu wa ngano
Ngano huwa na umuhimu ufuatao,
Kuelimisha
kuburudisha
kukuza maadili
kuhifadhi utamaduni
kukuza ushirikiano
kuhimiza
kuliwaza
kuendeleza historia
kukuza stadi za lugha
kukuza vipawa
kukuza kumbukizi

Ngano za mazimwi
Ni hadithi ambao wahusika wake ni mazimwi. Mazimwi ni viumbe ambao wanaoaminika kudhuru na huwa na fikira za kibinadamu lakini huwa na uwezo uliokiuka wa binadamu.Ngano za usuli
Hizi hueleza asili ama usuli wa hulka au sifa za wanyama, wadudu ,ndege au samaki.kwa mfano,
1. Asili ya fisi kuwa na mguu mfupi.
2. Asili ya chura kuwa ngozi mbaya.
Ngano za usuli hutofautiana na visaasili kwa kuwa visaasili uhusisha vyauzo vya mambo yanayohusu imani za kijamii kwa mfano, kuhusu kuwepo ulimwengu, kifo na kadhalika.
Visasili huamimika kuwa ni kweli.
Ngano za usuli huelezea asili ya sifa na tabia za viumbe.

SHABAHA
Kufikia mwisho wa somo unatarajiwa
1. Kufafanua maana ya miviga.
2. Kutambua mifano ya miviga.
3. Kufafanua sifa za miviga, umuhimu na hasara za miviga

Miviga

Miviga ni sherehe mbalimbali za kitamaduni zinazofanyika katika jamii.


Mifano ya Miviga


1. Sherehe za ndoa au arusi


2. Kumpa mtoto jina3. Unyago na Jando
4. Kutawazwa kiongozi
5. Matanga na mazishi


MADHARA YA MIVIGA
Katika karne hii baadhi ya miviga inaweza kuwa haifai.Zifuatazo ni baadhi ya hasara za miviga kwa kuzingatia hali ya kileo.
1. Sherehe za ukeketaji kwa wanawake huwa na madhara kwa
maisha yao.
2. Huzua uhasama baina ya jamii tofauti
3. Katika baadhi ya miviga watu hukiuka maadili ..
4. Hudhalalisha jinsia ya kike.
5. Hueneza maradhi.
6. Imani za dini hukiukwa.

Hitimisho
Miviga hutangamanisha na kuburudisha jamii kwa namna mbalimbali. Ingawa hivyo baadhi ya miviga huathiri jamii kwa njia nyingi na haifai.

Maana ya Ushairi simulizi

Ushairi simulizi hujumuisha tungo zote zenye mapigo ya kimuziki. Ushairi simulizi huimbwa,hughaniwa au kukaririwa. Ushairi simulizi haundikwi na huzuka wakati wa shughuli fulani.Kwa mfano, watu wanapofanya kazi na wanapo omboleza.

 

Maghani

UTANGULIZI
Maghani ni aina ya ushairi simulizi ambao hutolewa kwa maneno bila ya kuimbwa. Kuna aina mbili kuu za maghani:
a)
Maghani ya kawaida.
Haya yanahusu ushujaa, kazi, mapenzi, kifo, dini na kadhalika. Mifano ya maghani ya kawaida ni sifo. Kuna vipera kadhaa vya sifo kama vile:
i)Majigambo au vivugo.
ii)Tondozi.
iii)Pembezi.
b)
Maghani ya masimulizi.
Haya yana lengo la kusimulia hadithi, historia au tukio fulani maishani. Mifano ya maghani ya masimulizi ni:
i) Rara.
ii) Tendi
iii) Ngano


 

SIFA ZA USHAIRI SIMULIZI

Huwasilishwa kwa njia ya mdomo mbele ya hadhira kwa kukaririwa,kughaniwa au kuimbwa.

Huzuka papo kwa hapo.

Hutegemea sauti kama kipengele muhimu.

Huwez kuwasilishwa na mtu mmoja au zaidi

Huweza kuandamana na vitendo kama ishara za mikono,uso na miondoko mingine tofauti.

Hufungamana na shughuli au muktadha maalumu.

Huwasilishwa mahali wazi na palipo na hadhira.

Huwa na mapigo ya kimuziki yanayofanya utungo huo uweze kuimbika.

Hutumia aina tofauti tofauti za tamathali za lugha.


Umuhimu wa ushairi simulizi
1.Huendeleza utamaduni wa jamii.
2.Hueneza na kukuza usanii wa lugha husika.
3.Huburudisha.
4.Hukuza maadili katika jamii.
5.Huhima umoja na uzalendo miongoni mwa jamii.
6.Hutoa mtazamo wa kijamii kuhusu matukio tofauti kama vile kifo,jando au unyago na kadhalika.
7.Huelimisha ,hukosoa na kurekebisha.
8.Hukuza ubunifu.


Aina za Ushairi Simulizi

Kuna aina mbili za Ushairi Simulizi,
1.Nyimbo
2.Maghani
Katika kidato cha Pili ulijifunza aina za nyimbo,sifa na umuhimu wake.

Katika somo hili tutafafanua aina ya pili ya ushairi simulizi yaani Maghani.Ewe ng'ombe wangu
Ng'ombe mweupe wa kupendeza
Utoaye maziwa pasi kuchoka
Maziwa meupe na matamu ja asali
Mwingine ulivyo hayupo.


Chako kinyesi mbolea
Mimea, mboga, mtama
Kukuza bila gharama
Wangu ng'ombe daima
Nashukuru kuwa ni wangu.

 

Sifa zake zilitangaa
Zilivuka mabonde na milima kuzagaa
Watu waliozisikia wakashangaa
Wakapigwa hata na butwaa.

Ni jasiri asiye mfano na imara mno jabali
aliyepambana na dhiki za baridi kali
kufanya kitendo kikubwa akawa
kama mwali
ulioangaza mwanga mkuu kila mahali.Mazungumzo

Mwanafunzi, sikiliza mazungumzo haya kati ya Chebet na Wario kisha ufanye zoezi litakalofuata.
Chebet: Sasa Wario?
Wario: Poa sana Chebet.
Chebet: Mbona unajisikia fiti?
Wario: Kwa sababu kesho tunakwenda hepi!
Chebet: Unabahati unazo jo!
Wario: Kwani wewe umesota kiaje?
Chebet: Ni kweli nimesota. Kwani huoni ninasafiri kwa matatu?
Nimewacha ndinga nyumbani.
Wario: Sawa lakini kwetu mahewa ni lazima siku kila wikendi.
wenzetu washafika 'Klab Kutwa'wanatusubiri.
Chebet: Ah! Nilikuwa nimesahau kuwa wasee wanakutana
wikendi. Ngoja kwanza nijichape vilivyo kisha
nitajumuika nanyi.

 

Hitimisho
Mradi lugha inakua kila kuchao misimu itazidi kuibuka na kutoweka. Itakuwa vyema kuwa macho kutambua misimu hii na kuitumia tu inapobidi.

SHABAHA:
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uweze,

 • kueleza maana ya ngomezi
 • Kutaja sifa za ngomezi
 • Kueleza umuhimu wa ngomezi
 • Kutaja mifano ya ngomezi..

MAANA YA NGOMEZI

Ngomezi ni istilahi inayotumiwa kwa maana ya fasihi ya ngoma. Katika jamii nyingi za kiafrika, ngoma zilitumiwa (au hutumiwa) kupitisha ujumbe fulani.
Katika lugha ya Kiswahili kuna msemo wa;Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo; ambao umejengwa kwenye utambuzi wa umuhimu wa njia hii ya mawasiliano.
Ngomezi huelezwa kama fasihi ya ngoma kwa sababu katika jamii inayohusika midundo fulani ya ngoma huwakilisha maneno au kauli fulani.

Mfano wa Ngomezi

Chifu awaambie wanakijiji mambo yafuatayo:

Wananchi wenzangu, karibuni kwa baraza yetu ya leo. Wahenga wamesema kwamba, Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo,tayari ya mgambo imelia na bila shaka pamezuka jambo hapa. Serikali imetambua kuwa wananchi hawakai kwa upendo kama hapo mbeleni. Uhasama umejitokeza kati ya majirani na serikali inahimiza kuwe na utangamano. Watu waishi kama ndugu huku wakikabili changamoto kwa pamoja. Ahsanteni kwa kuhudhuria na kunisikiliza. Hadi siku nyingine, kwaheri ya kuonana.

SIFA ZA NGOMEZI
a) Kuwepo kwa ngoma au ala nyingine.
b) Kila mdundo wa ngoma huwa na ujumbe mahususi.
c) Maana ya mdundo hujikita kutokana na jamii husika.
d) Mapigo ya ngoma yafuate toni au ridhimu ambayo
huwakilisha maneno fulani.
e) Hadhira ya kutafsiri ujumbe iwepo.

UMUHIMU WA NGOMEZI
i. Hupitisha ujumbe kwa dharura
ii. Huitambulisha jamii
iii. Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii
iv. Hukuza uzalendo
v. Hukuza ubunifu
vi. Ni njia rahisi ya kuwasilisha ujumbe bila sauti ya mtu
vii. Huhifadhi siri za jamii husika.


 

Kiswahili kwa Kidato cha Tatu


Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu