KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kusoma - Kiswahili Kidato Cha 3

Utangulizi
Somo hili limenuiwa kumpa mwanafunzi ari ya kujisomea ili kustawisha msamiati wake wa Kiswahili. Stadi ya kusoma humpa mwanafunzi nafasi ya kuimarisha ukakamavu katika mazungumzo na kumsaidia katika somo la sarufi vilevile.
Mfano

Tazama video hii na kusikiliza kwa makini taarifa inayosomwa.


Taarifa

Nchi zinazoendelea hukumbwa na matatizo mengi mathalan umaskini, kutokuwepo kwa miundombinu ifaayo, uongozi potofu, sera ambazo hazifai na kadhalika. Tatizo mojawapo ambalo limekuwa sugu katika mataifa mengi ni lile la mrundiko wa mahabusu. Mahabusu hawa ni wengi kutokana na sababu mbili kuu.
Kwanza, kuwepo kwa nafasi ndogo katika magereza yaliyomo katika nchi fulani. Pili, suala la kuwepo kwa mahabusu wengi huweza kwenda sambamba na mrundikano wa kesi. Hii ina maana kuwa baadhi ya hao waliomo magerezani hawajahukumiwa rasmi kwa kuwa kesi zao hazijasikilizwa. Baadhi ya kesi huchukua muda mrefu kusikilizwa kutokana na muda wa kufanywa upelelezi na uchunguzi unaohusika hasa katika kesi za jinai.

Chemichemi za Kiswahili Kidato cha 3 by G. Waihiga and Wamitila, Longhorn Publishers.

Hitimisho

Katika kipindi hiki tumeshughulikia kusoma kwa ufahamu. Inafahamika kwamba ufahamu ni kifungu unachopewa na ambacho huwa na maswali. Maswali haya hukusudiwa kuupima uwezo wako wa kuyaelewa yanayozungumziwa, jinsi yanavyozungumziwa na mafunzo katika ufahamu wenyewe.
Kila mara, hakikisha kwamba, umelipata wazo kuu la taarifa kwa kuisoma tena na tena. Hakikisha kwamba unayachunguza maswali yaliyoulizwa kwa undani kujua kiini. Jaribu kumesoma taratibu na kwa makini ili kuelewa kwa undani wazo kuu katika kifungu. Jibu maswali kwa sentensi fupi na zilizokamilika. Kwa kawaida, majibu ya maswali hutokana na kifungu cha taarifa uliyosoma

Shabaha

Kufikia mwisho wa kipindi uweze:

i) Kubainisha vipengele muhimu katika uchambuzi wa kazi za fasihi na kutetea maoni yako kimantiki na inavyostahiki.
ii) Kupenda kusoma maandishi ya kiswahili kwa undani na kuyachambua.

iii) Kufafanua vipengele muhimu katika uchambuzi wa hadithi fupi.

 

Kusoma kwa kina

Stadi ya kusoma imenuiwa kumpa mwanafunzi ari ya kusoma na kukuza uwezo wa kupenda kusoma kazi mbalimbali za Kiswahili vikiwemo vitabu viteule vya Fasihi. Hii itamsaidia kustawisha umilisi wa matumizi ya msamiati kutegemea muktadha na kaida za jamii.
Kusoma huku aidha kunamsaidia mwanafunzi kusoma kwa jicho la ndani na kufasiri kazi za fasihi kama anavyoziona na kuelewa. Mwanafunzi anafaidi kwani mawazo na mtazamo wake wa masuala hupanuka. Fasihi itamfunza kuwa mwadilifu katika maisha na kutoa maamuzi yasiyotatanisha.

Utangulizi

Fasihi ni somo pana kwa vile linashirikisha fasihi simulizi na fasihi andishi.
Umejifunza mengi kuhusu fasihi simulizi katika stadi ya kusikiliza na kuzungumza kutoka kidato cha kwanza mpaka sasa.

Fasihi andishi inashirikisha:
i) Riwaya
ii) Tamthilia
iii)Ushairi-Mashairi yamegawanywa katika makundi mawili
- Mashairi ya arudhi
- Mashairi huru
iii) Hadithi fupi.

Ni vyema kusoma na kuelewa kila utanzu wa fasihi andishi. Katika kipindi hiki tutaangazia Hadithi fupi.

 Hitimisho
Hadithi fupi ni kigezo mwafaka cha kuimarisha lugha,kipawa cha uandishi na pia maadili katika jamii. Malengo yake huwa ni kukufahamisha masuala ibuka katika jamii mara kwa mara.

Shabaha

Baada ya somo hili unatarajiwa kuweza:
1.Kutambulisha aina mbalimbali za ushairi.
2.Kueleza ujumbe unaotokana na mashairi unayosoma.
3.Kusoma mashairi kwa ufasaha.

Ushairi

Ushairi ni kitengo cha fasihi kinachojishughulisha na mashairi.Mashairi nayo ni mitungo ya kisanaa yenye ujumbe unaowasilishwa kwa kuimbwa au kukaririwa.Hivyo basi mitungo hii huwa na mpangilio maalum wa maneno ili kuleta mahadhi katika uwasilishaji wake.Hebu soma mfano ufuatao:
1.Busara nina uwezo
Mfalme duniani
Ni mtukufu wa mawazo
Na maarufu mwishoni.
2.Palipo matengenezo,
Nikiwapo mimi ndani
Watu wanapata tuzo
Hawakosi abadani.
(Shaaban Bin Robert:sanaa ya ushairi)


Ujumbe kuhusu busara unawasilishwa kwa njia yenye umbo maalum inayoweza kukaririwa kama ulivyosikia.Kuna aina mbili kuu za mashairi:
1.Mashairi ya arudhi au jadi au ya kimapokeo.
2.Mashairi huru.

 

Mashairi ya arudhi
Haya hufuata kanuni za utunzi wa mashairi ya Kiswahili hivyo basi huchukua muundo fulani maalum.kwa mfano huwa na idadi maalum ya mishororo katika kila ubeti.

Sikiliza kwa makini shairi lifuatalo:
Mama nakupa pongezi,kwa yako mengi mapenzi
Mama wewe wanienzi,tokea zama za enzi
Mama tumbo lako zizi,miezi tisa ni kazi
Mama wanipa malezi,kufuta yangu machozi
Mama ndio la azizi,kwako kuna mapokezi
Mama huna ubaguzi,wote kwako wana mbuzi
Mama wewe u mjuzi,watupa pia mchuzi
Mama hutaki upuzi,watunyosha kama mhunzi
Mama huna msaidizi,wewe ndiye muuguzi
Mama jikoni ndo kazi,chakula mkurugenzi
Mama unanipa ndizi,ugali kwako si kazi
Mama waniosha ngozi,sabuni wanipakazi
Mama hutaki mapozi,wataka ufafanuzi
Mama umshikilizi,familia ndio ngazi

(Swaleh Mdoe:Nachora kwa maneno)


Shairi hili linasikika kutoa sauti fulani kwa sababu ya muundo wake maalum.Kuna aina nyingi za mashairi ya arudhi zinazotokana na tofauti za kimuundo au hata kimaana.Aina hizi pia huitwa Bahari au Mikondo ya ushairi.


Mfano wa shairi

Soma mfano mwingine wa shairi.
Binti: Nataka kuenda shuleni,nina haki ya kusoma
Nipate kuelimika,kuandika na kusoma.
Mama: Kwa nini shuleni wende,wewe mtoto wa kike?
Kaa nyumbani ucheze,ya kupika ndo ya uke!
Binti: Nataka jua sayansi,hesabu tena ya juu
Nihitimu mitihani, mpaka chuo kikuu

 


Hili ni shairi la beti mbili katika kila ubeti.Yaani tathnia au uwili.
Vilevile ni ngonjera kwa kuwa lina majibizano.

Kuna mashairi mengine ambayo huainishwa ifuatavyo:
Mishororo mitatu___tathlitha/utatu
Mishororo minne____tarbia/unne
Mishororo mitano___takhmisa/utano


Mashairi huru
Mashairi haya hayazingatii kanuni za utunzi wa mashairi ya Kiswahili.Hivyo basi hayana muundo maalum.
Sikiliza shairi lifuatalo kwa makini:

Shairi ulilosoma lina idadi sawa ya mishororo katika kila ubeti.Vile vile,idadi ya mizani inatofautiana katika kila mstari au mshororo.Shairi pia halina urari wa vina.Hii ni kawaida ya mashairi huru.

Maudhui ya Mashairi

Mashairi, mbali na muundo huwa na ujumbe.


Soma shairi lifuatalo ukizingatia maana yake.
Shairi la kwanza

Michezo huwa muhimu,kukuza bongo na mwili
Maungo huchangamka,na kuleta urafiki
Huleta nyingi shauku,mashabiki pande mbili


Kandanda au kabumbu,mchezo wa kupendeza
Timu mbili hupambana,mpira kukimbilia
Golini wafunga bao,kombe hujichukulia


Timu pia zimejaa,Livapuli mojawapo
Manichesta shujaa,Chelisi pia imo
Arsenali wasifika,Thieri kufunga bao


Kuna pia na masumbwi,ndondi jina lake pia
Conjestina awika,ngumi zake nzito nzito
Awachapa mabondia,ushindi ajipatia


Raga mpira wa nguvu,mibabe wanamenyana
Hushikwa kwenye mkono,wote wakakimbilia
Ni mwenye nguvu mpishe,mnyonge hana nafasi


Kuna pia na riadha,wakenya wanasifika
Terigati namba moja,duniani atajika
Katerina Wa Ndereba,yupo mbioni kukicha


Bakee pia tenisi,voliboli kiwanjani
Kuogelea majini,mitindo huku na huku
Kiriketi wanacheza,vijana wenye bidii.
Swaleh Mdoe ( Nachora kwa maneno publisher)

 


Shairi la pili

Sikiliza msomaji wa shairi la pili makini.
Mti ukingoni mwa mto
Katika bonde lenye rutuba
Na anga lisilohini mwanga
Hauhisi machungu
Kama miti ya kando
Ambayo huhangaishwa
Na hasira za kiangazi
Bali mfugaji mawingu
Apigapo filimbi
Na kumetameta umeme
Na kushuka gharika
Huo mti
Kuporomoka kwa kasi
Si kitu cha kuajabiwa
Na hilo
Historia yajua!
(Kithaka Wa Mberia:Mchezo wa karata:1997)
Kama ulivyoona shairi linazungumzia mti ulio ukingoni mwa mto na minigine katika kiangazi kikali. Miti hii inaweza kulinganishwa na watu katika hali mbalimbali za maisha.


Shabaha

Kufikia mwisho wa somo hili utaweza
1. Kueleza chimbuko la Kiswahili.
2. Kufafanua maelezi na usanifishaji wa lugha ya Kiswahili
nchini Kenya.

KUSOMA KWA KINA

HISTORIA NA MAENDELEO YA KISWAHILI

Provide an animation of a multiple of cartoons interchangeably saying the following
refer to the script

 

Maenezi

Maenezi ya lugha ya Kiswahili katika Afrika Mashariki


Hitimisho
Ni dhahiri kuwa lugha ya Kiswahili ina msingi wa mchanganyiko wa lugha za kiafrika (kibantu) na za kigeni. Lugha hii inaendelea kukua na matumizi yake kutandaa kuanzia kiwango cha mashinani hadi kimataifa.

Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu