KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Sarufi na Matumizi ya Lugha - Kiswahili Kidato Cha 3

Sarufi na matumizi ya lugha

Utangulizi

Sarufi ndio uti wa mgongo wa lugha yoyote ile. Sarufi huhusisha kanuni zinazotawala matumizi ya lugha ili kuepusha utata katika mawasiliano. Matumizi ya maneno kisahihi huleta maana iliyokusudiwa.
Sarufi ya lugha huwa uwanja mpana ambao unashirikisha mada mbali mbali.

Sarufi na matumizi ya lugha hushirikisha shughuli za kimawasiliano na kimaingiliano kwa sababu mbalimbali katika miktadha tofauti tofauti na mazingira halisi.
Ufunzaji na ujifunzaji wa sarufi na matumizi ya lugha humpa mwanafunzi nyenzo za kuwasiliana kikamilifu.
Katika kidato cha tatu unapaswa kujifunza umoja na wingi wa sentensi,vielezi,viwakilishi,mwingiliano wa maneno, vitenzi, uundaji wa nomino, sentensi za Kiswahili, nyakati na hali, ukanushaji, uakifishaji na mnyambuliko wa vitenzi. Katika mafunzo yetu haya, ni baadhi tu ya mada zitakazoshughulikiwa.

Vielezi

Vielezi ni maneno yanayotumika kufafanua vitenzi , vivumishi au vielezi vingine.

Maelezo

1. Mkulima aliondoka jana.
2. Daktari atamtibu sasa.
3. Zahra ni mrembo ajabu
4. Gari lilipita mbio sana
5. Alifanya kazi yake vizuri sana.
Kutokana na sentensi hizi tunatambua kuwa vielezi hufafanua zaidi vitenzi, vivumishi na vielezi vingine.kwa mfano.katika sentensi ya kwanza kielezi ni
jana. Kielezi jana kinafafanua zaidi kitenzi aliondoka.Katika sentensi ya pili kielezi ni sasa. Kielezi sasa kinatuelezea zaidi kitenzi atamtibu.Katika sentensi ya tatu ajabu ni kielezi. Kielezi ajabu kinafafanua zaidi kivumishi mrembo.Katika sentensi ya tano vizuri sana ni vielezi. Kielezi sana kinafafanua zaidi kielezi vizuri.

Aina za Vielezi
Kuna aina nne za vielezi kama ifuatavyo,
i. Vielezi vya namna kwa mfano asteaste, kasi
ii. Vielezi vya wakati kwa mfano leo ,alasiri,mwaka ujao
iii. Vielezi vya mahali kwa mfano darasani,mtini, Kisumu
iv. Vielezi vya idadi/kiasi kwa mfano mara mbili, daima, moja

Mifano katika sentensi
1. Kinyonga alitembea asteaste.
2. Kura ya maoni ilipigwa Agosti.
3. Alienda Kisumu kwa michezo ya kitaifa.
4. Alibwia vidonge mara mbili.
Maneno yaliyokolezwa wino ndiyo vielezi.Vielezi vya Namna

Zitazame picha zifuatazo na kusikiliza maelezo yanayotolewa.
1) Kinyonga alitembea aste aste kwenye tawi la mti.2) Cherono alikimbia kwa kasi3) Skauti mkuu alitembea kijeshi


Katika picha ulizotazama, vielezi vivliyotumiwa ni vielezi namna. Aina hii ya vielezi huonyesha jinsi kitendo kilitendeka. Kuna aina sita za vielezi namna /jinsi.


1. Mwalimu alisoma kitabu taratibu.(taratibu ni kielezi namna
halisi)
2. Mchezaji aliuacha mpira ukadundunda.(dundadunda ni kielezi
namna kiariri
)
3. Bibi Yule alifanya kazi yake kistadi.(kistadi ni kielezi namna
hali
4. Mgeni alisimama wima na kuimba.(wima ni kielezi namna
hali
)
5. Aliukomelea msumari kwa nyundo.(kwa nyundo ni kielezi
namna kitumizi(ala
)
6. Mvulana yule alicheka kwe! kwe! kwe! alipopewa
zawadi.(kwe!kwe!kwe!
ni kielezi namna kiigizi)Vielezi vya wakatiKatika mfano huu, leo jioni, mwaka ujao, zamani na jumamosi ni mifano ya vielezi vya wakati. Vielezi hivi hueleza vitenzi vilitendeka wakati gani au lini.

Vielezi vya mahali

Huonyesha vitendo vilitendekea wapi. Aghalabu huwa maneno kamili aidha viambishi.Mifano tuliyopewa inaonyesha aina mbili kuu za vielezi mahali. Kwa mfano, sentensi ya kwanza na ya nne,mtini na darasani ni vielezi ambavyo hutumia kiambishi tamati-ni ilhali katika sentensi ya pili na tatu, nje na juu ni maneno kamili ambayo ni vielezi.Vielezi vya Idadi au Kiasi

Hutuonyesha tendo husika limetokea au kutendeka mara ngapi.

Mara sita ,kila siku,mara kwa mara, na mara chache ni mifano ya vielezi idadi katika sentensi tulizopewa.

Hitimisho

Imebainika kuwa vielezi ni maneno yanayotumiwa kutoa habari zaidi kuhusu kitenzi.Aghalabu hutokea baada ya kitenzi, kivumishi au kielezi kingine. Pia imejitokeza kuwa baadhi ya nomino hutumika kama kielezi kulingana na jinsi ilivyotumika katika sentensi. Pia baadhi ya nomino za kawaida zinapochukua kiambishi tamati -ni huwa vielezi vya mahali. Unashauriwa uzame zaidi katika vielezi namna.
Aidha tafiti zaidi kuhusu vielezi vya vivumishi ,vya vielezi
na viambishi vielezi vya wakati.


Maana ya viwakilishi
Viwakilishi ni maneno (au hata viambishi) yanayotumiwa badala ya nomino. Msemaji anapozungumza, aweza kulazimika kurejelea nomino fulani mara kadha. Ili isitokee kuwa anajirudia, mzungumzaji anaweza kutumia neno badala ya nomino husika. Neno hilo ambalo litatumiwa badala ya nomino ndilo kiwakilishi. Kwa mfano:
1.
Huyu amepita mtihani.
2.
Mwenyewe hayupo.
3.
Changu kimepatikana.
4.
Za watoto zimenunuliwa.
5.
Wangapi wamefika?

Aina za viwakilishi
Kuna aina kumi za viwakilishi kama zifuatazo:
1. Viwakilishi vionyeshi
2. Viwakilishi vimilikishi
3. Viwakilishi viulizi
4. Viwakilishi virejeshi
5. Viwakilishi vya A-Unganifu
6. Viwakilishi vya sifa
7. Viwakilishi vya nafsi
8. Viwakilishi vya ngeli
9. Viwakilishi vya pekee
10. Viwakilishi vya idadi

VIWAKILISHI VIONYESHI
Hivi ni viwakilishi ambavyo huonyesha vitu visivyotajwa.Huonyesha kama kitu fulani ki karibu,mbali kidogo au mbali sana na mzungumzaji.Tazama vibonzo vifuatavyo:


Maneno
huu, huo na ule ni viwakilishi vya nomino ufagio kutegemea ujirani na msemaji.
Tazama mifano katika sentensi zifuatazo:
1.
Huu ni mweusi.


2.
Huo ni mweupe.

3. Ule ni mwekundu


Hebu tuone mifano kutoka ngeli mbali mbali.

Viwakilishi Vimilikishi

Kumiliki ni hali ya kuwa na kitu au hali ya kitu kuwa cha mtu.kwa mfano mwanafunzi humiliki kalamu,kitabu na sare. Viwakilishi vimilikishi hutumiwa badala ya nomino kuonyesha umiliki. Viwakilishi vimilikishi vinajitokeza katika nafsi tatu yaani ya kwanza, ya pili na ya tatu. Mizizi ya viwakilishi hivi ni -angu; -ako na -ake katika umoja na -etu; -enu na -ao katika wingi.
Tazama mifano ya sentensi:
1. Changu kimepigwa chapa vizuri.
2. Lake linaletwa leo.
3. Yako inapendeza.
4. Kwetu kunavutia watalii.
5. Vyao ni vitamu mno.
6. Zenu zimepatikana.


Viwakilishi vimilikishi vinategemea upatanisho wa kisarufi kuambatana na ngeli mbalimbali. Hebu tazama jedwali lifuatalo:


VIWAKILISHI VIULIZI

Ni maneno yanayowakilisha nomino kwa kuuliza. Kuna aina tatu za viwakilishi hivi yaani: -pi,-ngapi na gani.
Tazama mifano ya sentensi hizi:
1.Upi umepandwa leo?
2.Wangapi wamefika hapa?
3.Gani limeharibika?
Viwakilishi -pi na -ngapi huweza kupatanishwa kisarufi kuambatana na ngeli mbalimbali.Tazama jedwali lifuatalo:Kiwakilishi gani hakibadiliki,yaani,hubakia kilivyo katika ngeli zote.Tazama jedwali:VIWAKILISHI VIREJESHI

Ni maneno yanayowakilisha nomino kwa kurejesha.Vipo vya aina mbili:


1.O-rejeshi
2.Amba rejeshi

O-rejeshi
Tazama mifano ifuatayo:
1.Kilichohifadhiwa vizuri kimerudishwa.


2.Aliyetuhutubia mwaka jana atatutembelea.
3.Uliomwagika umekusanywa.


4.Zilizotumwa zilikuwa na ujumbe mzuri

Amba rejeshi
1.Ambacho kilihifadhiwa vizuri kimerudishwa.
2.Ambaye alituhutubia mwaka jana atatutembelea.
3.Ambao ulimwagika umekusanywa.
4.Ambazo zilitumwa zilikuwa na ujumbe mzuri.

Ukitazama makundi hayo mawili ya sentensi,utaona kuwa O-rejeshi na Amba rejeshi zina matumizi sawa katika sentensi.Epuka kutumia O-rejeshi na Amba rejeshi katika sentensi moja.

Viwakilishi vya -A unganifu

Viwakilishi vya a-unganifu huwakilisha vitu ambavyo humilikiwa.Viambishi vya ngeli hutumiwa katika kuunda viwakilishi hivi.


Viambishi hubadilika kulingana na ngeli kama inavyoonekana katika jedwali.Viwakilishi vya Sifa

Hivi huwakilisha kwa kutumia sifa za nomino ambazo kwa wakati huo hazipo.Kwa mfano:


1.Mkubwa utajengwa.
2.Kifupi kimewekwa jukwani.
3.Mzuri amepewa zawadi.
4.Hodari amepongezwa.
5.Zuri litanunuliwa.

Viwakilishi vya Nafsi

Viwakilishi nafsi huwakilisha nomino kwa kurejelea nafsi tatu yaani, ya kwanza,ya pili na ya tatu,katika umoja na wingi.Kwa mfano;
1.Mimi ninafanya kazi Nairobi.
2.Sisi ni wafanyikazi wa shirika la reli.
3.Wewe utakwenda Eldoret leo.
4.Ninyi mtaanza kazi mapema kesho.
5.Yeye atakwenda Mombasa kesho.
6.Wao wanalipwa mishahara mizuri.

VIWAKILISHI VYA PEKEE

Hivi ni viwakilishi vya -ote,-o-ote,-enye,-enyewe,-ingine,na -ingineo.Hebu tazama jedwali lifuatalo:
JEDWALI IJEDWALI II


VIWAKILISHI VYA IDADI

Hivi huwakilisha nomino kwa kuonyesha idadi kama vile moja, wanne,ishirini.Hata hivyo idadi hii wakati mwingine si bainifu na maneno kama vile wengi,wachache, hutumiwa.

 


1.Wawili wamechinjwa.
2.Vinne vimeletwa.
3.Wachache wamefika.
4.Nyingi zimenunuliwa ili zitumiwe katika warsha.

Viwakilishi vya Ngeli

Hivi ni viwakilishi vinavyowakilisha ngeli ya nomino katika sentensi.Hujitokeza kama viambishi.Hebu tazama jedwali lifuatalo.


 

Hitimisho
Kila wakati unapotumia viwakilishi usitaje nomino. Vilevile kumbuka kuwa viwakilishi vingi hutumiwa kulingana na ngeli.


Shabaha
Kufikia mwisho wa somo unatarajiwa;
1. kufafanua maana ya mwiingiliano wa maneno.
2. Kutambua mwiingiliano wa maneno katika sentensi.
3. Kutofautisha matumizi tofauti ya neno moja katika sentensi.

Utangulizi

Maneno katika lugha huweza kutumika kwa njia tofauti kuleta maana tofauti kwa kuzingatia uamilifu wake katika muktadha unaohusika kwa mfano,
1. Nairobi ni mji mzuri.
2. Nitamtembelea Nairobi kesho.
Katika mfano wa kwanza neno Nairobi limetumika kama nomino na katika mfano wa pili linatumika kama kielezi.

Huu ndio mwingiliano wa maneno.

Maelezo

Maneno yanaweza kuingiliana kwa njia ifuatayo.

1.Kitenzi (T) kuwa nomino (N)

a. i)Mwihaki anapenda kuimba(T)

ii)Kuimba kwa Mwihaki kunapendeza(N)

b. i)Mwanafunzi anajua kuandika vizuri (T)

ii)Kuandika vizuri hufurahisha walimu (N)

c. i) Meza dawa mara mbili kwa siku.(T)

ii)Meza nzuri imenunuliwa.(N)


2.Nomino(N) kuwa kivumishi(V)

Nomino hubadilika na kuwa kivumishi, ikiwa nomino hiyo inatumika kuelezea sifa za nomino nyingine. Nomino ikitumika hivi huwa kivumishi cha nomino kwa mfano,

a.(i) Mkulima amepata mazao mengi(N)

(ii)Mwalimu mkulima amepata mazao mengi (V)

b. (i) Mrembo yule ni nani? (N)

(ii) Faizali ni msichana mrembo.(V)
3.Vivumishi (V) kuwa viwakilishi (W)

a. (i)Mchezaji hodari amesifiwa.(V)

(ii)Hodari amesifiwa.(V)

b. (i)Ua hilo ni maridadi sana.(V)

(ii)Hilo ni maridadi sana.(W)4.Nomino (N) kuwa vielezi (E)

Baadhi ya nomino huweza kutumiwa kama vielezi.

a. (i)Haraka ya mwanafunzi huyu imemfaa.(N)

(ii)Mwanafunzi alitembea haraka.(E)

b. (i)Pupa ya fisi ilimtia mashakani.(N)

(ii) Alitafuta mfupa kwa pupa.(E)

c. (i) Kasi ya gari lile imesababisha ajali.(N)

(ii)Gari liliendeshwa kwa kasi.(E)

d. (i) Mombasa ni mji unaopendeza.(N)

(ii)Watalii huenda Mombasa kujivinjari.(E)


5.Kiunganishi(U) kuwa Nomino (N)

a. (i)Nilitakikana kumwona ila sikuweza.(U)

(ii)Ila yake kubwa ni wizi.(N)

b. (i)Sina neno mradi nawe huna neno.(U)

(ii)Mradi wa kazi kwa vijana haujafaulu.(N)6.Kitenzi(T) kuwa kivumishi (V)

a. (i)Tosa mkate ndani ya chai uule,'Mama alimshauri'. (T)

(ii)Embe tosa haliliki. (V)Hitimisho
Maneno ya Kiswahili huwa yanaingiliana. Ni muhimu kutambua aina za maneno na jinsi yanavyotumiwa ili uwe na uwezo wa kuyatumia kistahiki bila ya kuvuruga maana au sarufi.

UTANGULIZI

Katika kidato cha pili ulijifunza vinyume vya vitenzi. Uliona kuwa vinyume vya vitenzi ni vitenzi vilivyo na maana inayokinzana na kitenzi kilichotolewa.

Ilidhihirika pia kuwa baadhi ya vinyume vya vitenzi huundwa kwa kutumia viambishi tamati.Kwa mfano,
choma -chom
oa
komea- kom
oa
shona- shon
oa
tia- t
oa
fuma- fum
ua
kunja- kunj
ua
hama- ham
ia
fukia- fuk
ua

Vivyo hivyo katika kidato cha pili uliweza kujifunza mnyambuliko wa vitenzi katika kauli zifuatazo.


i) Kutendwa -anapigwa
ii) Kutendewa -anasomewa
iii) Kutendeka -umefungika
iv) Kutendana -wanapigana
v) Kutedeana -wanasomeana
vi) Kutendeshwa -anabebeshwa
vii) Kutendeteshana -wanalishana
viii) Kutendeshea -anaendeshea
Katika kipindi hiki utajifunza maana ya mzizi wa kitenzi, viambishi awali katika vitenzi, viambishi tamati katika vitenzi, na hali ya kuamrisha.MZIZI WA KITENZI

1. Sahau
2. Rudi
3. Amini
4. Dharau
5. Samehe
1.
Sem-a, sem-eana, sem-wa
2.
Pig-a, pig-sha, pig-lia
3.
L-a, l-iwa, l-isha
4.
F-a, f-iwa, f-iliwa
5.
Som-a som-eka som-eka
Sehemu za maneno unazoona ni mizizi. Umeona kuwa mzizi waweza kuwa neno kamili au sehemu ya neno?
Ikiwa mzizi ni neno kamili linalojisimamia kimaana na haliwezi kugawika katika visehemu, basi huwa ni
mzizi huru.
Kwa mfano:
Barizi
Balehe
Laki
Hukumu
Kabili
Dadisi

Ikiwa mzizi ni sehemu tu ya neno na sehemu yenyewe haiwezi kujisimamia kimaana basi huwa ni mzizi tegemezi.

Kwa mfano:

Kumkaribisha
Nitasoma
Mlielewa
Hawachezi
Mnacheza
Limeni

Kitenzi,katika kauli yake ya awali huwa ni shina.

Tazama mifano hii:
i. Imba
ii. Cheka
iii. Andika
iv. Enda
v. Soma
Vitenzi hivi vina toa maana kamili na vina irabu 'a' kama kimalizio. Katika hali hii kitenzi huwa ni shina.

 

Viambishi awali katika vitenzi

Hivi ni viambishi ambavyo huja kabla ya mzizi.
Mifano:
i) wa-li-o-imba
ii) wa-me-ji-pendekeza
iii) ha-wa-ku-m-sikiliza
iv) u-na-ji-funza
v) a- me-m-thibitisha

Viambishi awali katika vitenzi huwa na majukumu maalum.

Viambishi awali nafsi katika vitenzi

Hivi ni viambishi viavyowekwa kabla ya mzizi wa kitenzi na huonyesha mtenda au mtendewa wa kitenzi.


Kwa mfano:
1. a)Mimi nitamwelekeza.
b)Sisi tutawaekeleza.


2. a)Wewe umenyamaza sana.
b)Ninyi mmenyamaza sana.
3. a)Yeye amepika wali.
b)Wao wamepika wali.

Viambishi vya kuwakilisha njeo (wakati) na hali

Viambishi hivi huambikwa kabla ya mzizi kuonyesha wakati kitendo kilitendeka au kuonyesha hali mbalimbali za kitenzi hicho.
Kwa mfano:

1. a)Rose anasoma.

b)Rose asoma.


2.Kiti kitanunuliwa.


3.Wageni walifika mapema.


4.Amemaliza kula.


5. Mwalimu akija tutaondoka.

6. Mimi hupenda Kiswahili.

7. Mtoto alikuja akatusalimu akatoroka.

8. Ningesoma ningeelewa makala hayo.

Viambishi vya Ukanushi

Viambishi hivi huambikwa mbele ya mzizi wa kitenzi na huonyesha ukanusho wa kitenzi.

Kwa mfano:


1.Hajaandika insha yake.


2.Hamtavua samaki wengi.


3.Usingesoma usingeelewa.


4.Hamwimbi.


5.Sili.

6.Huandiki.

7.Hataenda.

8.Msicheze.

Viambishi vya yambwa

Yambwa huwa ni kitendwa au kitendewa. Yambwa ni nomino ambayo hupokea athari ya kitendo. Huitwa pia shamirisho.
Viambishi vya yambwa au yambiwa huambikwa mbele ya mzizi wa kitenzi kama tu viambishi vya nafsi au njeo.

Mifano:
(Highlight the syllable)

Wamekivunja

Umemsaidia

Atawalipia
Nitaila

Mnamwimbia

Tungekupa

Viambishi Virejeshi

Viambishi hivi huambikwa katika kitenzi kuturejesha kwa nomino iliyotajwa awali.

Mifano:

 


1. Lililochimbwa
2. Waliofundisha
3. Ninayokula
4. Uliposimama
5. Alichokalia
6. Mtakayolipa
7. Wanayopalilia
8. Yanayomwagika
9. Iliyooza
10. Vilivyonunuliwa

Viambishi tamati
Viambishi tamati hutokea baada ya mzizi wa vitenzi.
Mifano
Sem-ea
Som-ew-a
Chuku-lik-a
Chez-eni
Andik-a


Kutokana na mifano uliyosoma utaona kuwa viambishi tamati huonyesha dhana mbalimbali.
a)Kiishio cha kitenzi
Som-a
Jib-u
b)Mnyambuliko wa vitenzi
Som-ew-a (tendewa)
Andik-ish-a (tendesha)
Chom-o-a (tendua)

c)Kirejeshi'O'
Afundisha-ye
Usomeka-o
Kijaa-cho

d)Hueleza mahali
Aendako
Aingiamo

e)Hali ya kuamrisha
Someni!
Andikeni!

Hali ya Kuamrisha

Vitenzi katika hali ya kuamuru hubainika kutokana na toni inayosikika. Toni hii huwa na ukali na anayeambiwa hutarajiwa kutenda anavyoamriwa.Vitenzi katika hali ya kuamuru vinapoandikwa alama hisi ! hutumiwa ili kubainisha kiimbo au toni.Kiambishi 'ni' huambikwa mwishoni mwa kitenzi kubainisha kuwa wanaotolewa amri ni wengi.
Kwa mfano:
a) Jengeni!
b) Pikeni!
c) Vuteni!
d) Lipeni!
e) Sukeni!

Baadhi ya vitenzi huishia na 'e'

a) Tule!
b) Turauke!
c) Usile!
d) Msitukanane!

 

Hitimisho
Ni muhimu kukumbuka ya kwamba vitenzi katika hali ya kuamrishwa huonyeshwa kwa matumizi ya alama hisi.!

Viambishi

Kiambishi ni sehemu ambayo huambikwa kwenye mzizi wa neno ili kulipa maana ya ziada.Kiambishi huweza kubadilisha kitenzi kikawa nomino au kukifanya kitenzi kupata maana mpya

Kuna aina kuu mbili ya viambishi
(i) viambishi awali na
(ii) viambishi tamati

 

Viambishi awali katika vitenzi

Hivi ni viambishi ambavyo huja kabla ya mzizi.
Mifano:
(Highlight the syllables by blinging or the most effective and attractive highlight)
i) wa-li-o-imba
ii) wa-me-ji-pendekeza
iii) ha-wa-ku-m-sikiliza
iv) u-na-ji-funza
v) a- me-m-thibitisha


1. Viambishi awali nafsi katika vitenzi

Hivi ni viambishi viavyowekwa kabla ya mzizi wa kitenzi na huonyesha mtenda au mtendewa wa kitenzi.

(as the text is read, highlight with a bling)

Kwa mfano:
(Highlight the syllable)

Mimi nitamwelekeza
Sisi tutawaekeleza

Wewe umenyamaza sana
Ninyi mmenyamaza sana
Yeye amepika wali
Wao wamepika wali


2. Huwakilisha njeo (wakati) na hali

Viambishi hivi huambika kabla ya mzizi kuonyesha wakati kitendo kilitenda au kuonyesha hali mbalimbali za kitenzi hicho.
Kwa mfano:
(Highlight the syllable)

Rose anasoma

Rose asoma

Kiti kitanunuliwa

Wageni walifika mapema

Amemaliza kula

Mwalimu akija tutaondoka

Mimi hupenda Kiswahili

Mtoto alikuja akatusalimu akatoroka

Ningesoma ningeelewa makala hayo.


3. Viambishi vya ukanushi

Viambishi hivi huambikwa mbele ya mzizi wa kitenzi na huonyesha ukanusho wa kitenzi.

Kwa mfano:

(Highlight the syllable)

Hajaandika insha yake

Hamtavua samaki wengi

Usingesoma usingeelewa

Hamwimbi

Sili

Huandiki

Hataenda

Msicheze

Viambishi vya yambwa

Yambwa huwa ni kitendwa au kitendewa. Yambwa ni nomino ambayo hupokea athari ya kitendo. Huitwa pia shamirisho.
Viambishi vya yambwa au yambiwa huambikwa mbele ya mzizi wa kitenzi kama tu viambishi vya nafsi au njeo.

Mifano:
(Highlight the syllable)

Wamekivunja

Umemsaidia

Atawalipia
Nitaila

Mnamwimbia

Tungekupa


5. Viambishi virejeshi

Viambishi hivi huambikwa katika kitenzi kuturejesha kwa nomino iliyotajwa awali.

Mifano:

(Highlight the syllable)


1. Lililochimbwa
2. Waliofundisha
3. Ninayokula
4. Uliposimama
5. Alichokalia
6. Mtakayolipa
7. Wanayopalilia
8. Yanayomwagika
9. Iliyooza
10. Vilivyonunuliwa

B: Viambishi tamati katika vitenzi
Viambishi tamati huambikwa baada ya mzizi katika kitenzi

Mifano:
(Highlight the syllable)


1. Semea
2. Somewa
3. Alimayo
4. Chukulika
5. Ukupigao
6. Liliwalo
7. Tegwa
8. Andikiana
9. Bebeshwa
10. Legezeka
Viambishi tamati huonyesha kauli mbalimbali za vitenzi. Pia huonyesha kirejeshi O katika kitenzi.

Kirejeshi O kikiambikwa katika kitenzi kama kiambishi tamati, hutoa dhana ya hali ya mazoea.

Ta
zama vibonzo vivyatavyo kwa makini


1. Provide an animation of policemen on a parade responding to orders with a voice over
Thus; attention! Right turn!
By your left, forward match!


2. Provide another animation of four students in inform in class on their desks responding to these orders:
Simama!
Kaeni!
Simameni!
Kaeni!

The students should do the actions ordered.

Umeona na kusikia nini?

Bonyeza kupata jibu kamili.

Vitenzi katika hali ya kuamuru hubainika kutokana na toni inayosikika. Toni hii huwa na ukali na anayeambiwa hutarajiwa kutenda anavyoamriwa.

Vitenzi katika hali ya kuamuru vinapoandikwa alama hisi ! hutumiwa ili kubainisha kiimbo au toni.

Provide photograghs of the following with a voice over.

i) Students writing with a voice over Andikeni!
ii) Little children in bed with a voice over laleni!
iii) Children on a table with food ready to eat with a voice over kuleni

Kiambishi ni huambikwa mwishoni mwa kitenzi kubainisha kuwa wanaotolewa amri ni wengi.
Kwa mfano:
a) Jengeni
b) Pikeni
c) Vuteni
d) Lipeni
e) Sukeni

Baadhi ya vitenzi huishia na e

a) Tule
b) Turauke
c) Usile
d) Msitukanane.

Shabaha

Kufikia mwisho wa kipindi hiki,unafaa uweze

i) Kueleza maana ya mnyambuliko wa vitenzi
ii) Kunyambua vitenzi katika kauli za
a) Kutendeshewa
b) Kutendesheana
c) Kutendesheka
d) Kutendama
e) Kutendata
f) Kutendua
g) Kutenduka

 

Kauli ya kutendeshewa


Vitenzi katika kauli hii hutokana na vitenzi vilivyo katika kauli ya kutendesha.
Vitenzi hivi huongezewa kiambishi tamati
-iw au-ew

Mifano:
1. Ogeshewa
2. Limishiwa
3. Dundishiwa
4. Pangishiwa
5. Rembeshewa

Kauli ya Kutendesheana

Tazama kwa makini Kibonzo hiki.

Katika kibonzo hiki dhana ya kutendesheana inajitokeza. Dhana inayojitokeza hapa ni kwamba walimu hawa wana majukumu ya kusababisha mambo yatendeke kwa niaba yao. Wanabadilishana majukumu.
Mifano


1. Endesheana
2. Ketishiana
3. Andikishiana
4. Zamishiana
5. Bakishiana

Kauli ya kutendesheka

Tazama na kusikiliza kwa makini vibonzo hivi.

 

Mbio za mita mia moja zimeanzilika bila tatizo.

Katika vibonzo hivi tendo lililisababishwa na kitu au mtu limetokea kikamilifu au vizuri.
Mifano:
1. Kisaka alisalimishika na Hirmoge.
2. Mifugo walilishika kwa nyasi zilizonawiri.
3. Bogi lililoanguka barabarani lilisongezeka.
4. Wezi waliotoroka watashikika.
5. Ngazi inaporomosheka.

Kauli ya kutendamaDhana inayodhihirika ni kuwa kitendo kilifanyika na hali hiyo ikadumishwa. Kauli hii hubainika kwa kitenzi kuongezewa kiambishi 'm' ili kutoa dhana ya kutendana na kubaki katika hali hiyo.

Mifano:


1. Fichama
2. Anadama
3. Sakama
4. Chutama
5. Lalama

Kauli ya Kutendata

Fumbata


Kokota


Hali inayojitokeza ni ya vitu viwili kugusa na kuendelea kuwa katika hali hiyo.
Kauli hii hutumia viambishi tamati 'ta'

Mifano.
1. Kamata
2. Pakata
3. Sokota
4. Okota
5. Fumbata

Kauli ya Kutendua

Kutendua ni kauli inayoonyesha kinyume cha tendo lililotajwa awali. Vitenzi hivi hunyambuliwa kwa kuongezewa kiambishi tamati 'u'au'o'.

Mifano:

Ziba -zibua
Komea -komoa
Kosa -kosoa
Chimba -chimbua
Angika -angua

kauli ya kutenduka

Kauli ya kutendua na ya kutenduka huonyesha dhana sawa, yaani hutoa maana ya kinyume. Kauli ya kutendua husababishwa na mtu lakini kauli ya kutenduka hutokea tu yenyewe.
koti limeanguka.
'bango limebanduka'.


Umeona kuwa koti na bango vyenyewe vinasababisha vitendo kutokea.Hitimisho
Ni vyema kuelewa kunyambua vitenzi katika kauli mbalimbali ili uweze kujieleza kwa urahisi. Aidha hakikisha vitenzi unavyonyambua vinatoa maana inayokusudiwa. Baadhi ya vitenzi vikinyambuliwa katika kauli fulani hukosa mantiki.

SHABAHA
Kufikia mwisho wa kipindi, unafaa uweze
a) Kubaini vitenzi vya silabi moja
b) Kunyambua vitenzi vya silabi moja katika kauli mbalimbali
c) Kubainisha vitenzi vya asili ya kigeni
d) Kunyambua vitenzi vya asili ya kigeni katika kauli
mbalimbali.

Mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja na vya asili ya kigeni katika kauli mbalimbali


Utangulizi
Kama ulivyojifunza katika kidato cha pili, mnyambuliko wa vitenzi ni kukiongezea kitenzi kiambishi ili kukipa maana mpya.

Katika kipindi tutashughulikia vitenzi vya silabi moja. Vitenzi vya silabi moja huwa si vingi.

 

Mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja

Vitenzi vya silabi moja vinapotumika katika sentensi huchukua kiambishi 'ku' mwanzoni ili kukipa maana inayoeleweka.

Kiambishi hicho 'ku' hudondoshwa vinaponyambuliwa.

Tazama mchoro huu kwa makini.
Kuna vitenzi kumi vya silabi moja. ili kiweze kukubalika,unapokinyambua katika kauli fulani, lazima kitenzi hicho kitoe maana yenye maantiki.Hii inafanya baadhi ya sehemu kuachwa wazi.


Mnyambuliko wa vitenzi vya asili ya kigeni

Sifa kuu ya vitenzi vya asili ya kigeni ni kuwa huwa haviishii na irabu 'a' kama ilivyo na vitenzi vya asili ya kibantu. Vitenzi vya kigeni huishia irabu 'e', 'i', na 'u'.

Kwa mfano
1. Samehe
2. Tubu
3. Sahau
4. Fadhili
5. Fariji
6. Dhulumu
7. Balehe
8. Hitimu
9. Dadisi
10. Dhuru
Vitenzi hivi hunyambuliwa kwa kuzingatia maana inayokusudiwa. Baadhi ya vitenzi hivi havinyambuliki katika kauli fulani na haiwezekani kuvinyambua katika kauli zingine.
Aghalabu mizizi ya baadhi ya vitenzi hivi husalia na kuchukua tu kiambishi cha kauli.

Tazama jedwali hili kwa makini.

Hitimisho
Mwanafunzi ufahamu kuwa vitenzi vya asili ya kigeni havionyeshi tofauti vikinyambuliwa katika kauli za kutendwa na kutendewa. Hii hubainika katika sentensi tu. Kwa mfano,
1. Swali lilijibiwa vizuri(kutendwa)
2. Mwalimu alijibiwa swali lake vizuri.(kutendewa)

Vitenzi vya asili ya kigeni.

Vitenzi vya asili ya kigeni ni vinavyotokana na maneno ya lugha nyingine yaliyoingizwa katika Kiswahili.Lugha hizi ni kama Kiarabu,Kihindi,Kireno na Kingereza.Aghalabu vitenzi vya asili ya kigeni huishia kwa irabu i,u na e tofauti na vile vya asili ya kibantu ambavyo huishia kwa irabu a.
Mifano ya vitenzi vya asili ya kigeni ni kama:
Sahau
Adhibu
Udhi
Talii
Samehe
Starehe.

 

Uundaji wa Nomino

Nomino zinaweza kuundwa kutokana na vitenzi vya asili ya kigeni.Tazama jedwali lifuatalo.Hebu tuangalie mifano zaidi katika jedwali lingine.


Hebu tuangalie mifano ya nomino hizo katika sentensi.


1.Msafiri alichoshwa na safari ndefu.


2.Maneno ya Salome yaliniletea faraja.


3.Nilijibu maswali machache tu katika hojaji hiyo.


4.Kuwepo kwa uchafu mwingi kunaleta madhara.


 Mifano ya sentensi


1. Mchezaji amefunga bao.
2. Mama anasonga ugali na baba anapalilia mahindi.
3. Mwanafunzi aliyeumia alipelekwa hospitalini.


Aina za Virai


Kuna aina nne za virai
1. Virai nomino
2. Virai vivumishi
3. Virai vielezi
4. Virai vihusishi

Aina za Virai

Kuna aina nne za virai
1. Virai nomino
2. Virai vivumishi
3. Virai vielezi
4. Virai vihusishi


Virai Nomino (KN/RN)

Kirai nomino ni kipashio ambacho hufanya kazi ya nomino. Neno lake kuu huwa ni nomino ama kiwakiliishi chake.
Mifano katika sentensi
1.
Baba na mama wanalima.
2.
Ukuta uliobomoka unajengwa upya.
3.
Gari hilo linaendeshwa mbio.
4.
Wafungwa wanne wametoroka gerezani.
5.
Embe tamu limeliwa.

 

Virai vivumishi (RV/KV)
Huwa ni kundi la maneno ambalo neno lake kuu ni kivumishi. Fungu hili la maneno huvumisha nomino aina kiwakilishi chake.
Mifano
1. Nguo
maridadi sana imenunuliwa.
2. Tumbo
lenye maumivu husumbua sana.
3. Kiti
chake kizuri kimevunjika.
4. Sungura
huyu mjanja alilaghai fisi.
5. Mtoto
mwerevu wa shangazi amepita mtihani.

Kirai Kielezi
Kirai kielezi ni kundi la maneno ambalo lina uamilifu wa kielezi.
Kirai kielezi hivyo basi ni mfuatano wa vielezi viwili au zaidi.
Mifano ya virai elezi
1. Rais wa marekani atawasili Kenya
kesho jioni.
2.
Sasa hivi tutaanza shughuli yetu.
3. Mkutano wa siasa utafanyika
katika bustani ya uhuru.
4. Wanafunzi walizunguka
uwanjani mara tatu.
5. Mama hututembelea
mara kwa mara.

Virai Vihushi

Maana
Ni kundi la maneno ambalo neno lake kuu ni kihusishi. Muundo wake umejengeka katika mahusiano baina ya kihusishi na fungu la maneno liloko katika sentensi. Kirai kihusishi huundwa kwa kihusishi na hufuatwa na kikundi nomino.

Mifano ya Virai vihusishi
1. Mtoto amelala
ubavuni mwa mamake.
2. Kitabu kimewekwa
juu ya meza.
3. Usilime
kando ya barabara.
4. Uongozi wa mkuu huyu wa wilaya ni
wa kupigiwa mfano.
5. Umeweka saa yangu
ndani ya sanduku?


Vishazi

Maana ya Kishazi:
Ni kundi la maneno ambalo lina kiima kimoja na kiarifu kimoja. Kishazi huwa ndani ya sentensi kuu. Baadhi ya vishazi huweza kusimama peke yake na kikatoa maana kamili au kikawa sehemu ya sentensi kwa mfano,
1) Bei ya mahindi imeshuka ingawa mvua haijanyesha.
2) Kitabu kilicholoa maji kimepasuka.
Vishazi ni:
a) Kitabu kimepasuka.
b) Kilicholoa maji.
c) Bei ya mahindi imeshuka.
d) Mvua haijanyesha.


Aina za Vishazi

Kuna aina mbili ya vishazi:
a) Vishazi huru
b) Vishazi tegemezi


Vishazi huru
Vishazi huru ni vile ambavyo hata vikiondolewa katika sentensi kuu huweza kutoa maana kikamilifu. Kwa mfano;
1) Walimu wanasoma gazeti na wanafunzi wanacheza.
2) Jumba lililoanguka limejengwa upya.
Kishazi huru ni -
1.Jumba limejengwa upya.
2.Walimu wanasoma gazeti.
3.Wanafunzi wanacheza.
Njia rahisi ya kutambua kishazi huru ni kutafuta sentensi sahili ndani ya ile sentensi kuu.Vishazi tegemezi
Hivi ni vishazi ambavyo vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu haviwezi kusimama peke yake na kuleta maana iliyokamilika. Vishazi tegemezi hutegemea vishazi huru au vishazi vingine tegemezi ili kuleta maana.Kwa mfano,

1) Kenya iliposhinda mashindano ya riadha ya bara la Afrika, watu wengi walifurahi.
Fungu la maneno lililokolezwa wino ni kishazi tegemezi kwa kuwa linategemea sehemu ambayo haijakolezwa (kishazi huru) ili kuleta maana.
2)
Ikiwa hunyamazi nitakuacha.
Katika sentensi hii, sehemu iliyokolezwa ni kishazi tegemezi. Sehemu hiyo haiwezi kutoa maana kamili, hivyo inahitaji kuungana na kishazi huru'
nitakuacha' ili kuleta maana.

Utambuzi wa kishazi tegemezi

Njia za kutambua kishazi tegemezi katika sentensi
1) Tambua sehemu ambayo hata ikiondolewa katika sentensi hiyo itabaki kuwa na maana. Kwa mfano,
Wafanyikazi wa serikali waliohusika katika ufisadi wameshtakiwa.
2) Tafuta palipotumiwa viambishi vya masharti kama nge, ngeli, ngali na ki. Kwa mfano,
a) Ungesoma kwa bidii, ungepita mtihani.
b) Mvua ikinyesha, tutapanda miti.
c) Ungalipata kazi hiyo, maisha yako yangaliimarika zaidi.
Sehemu zote zilizokolezwa wino ni vishazi tegemezi kwa kuwa kuna matumizi ya viambishi vya masharti.
3) Njia ya tatu ya kutambua kilipo kishazi tegemezi ni kutafuta palipotumiwa 'o' rejeshi au kirejeshi 'amba'. Kwa mfano,
a) Tarakilishi iliyoharibika imekarabatiwa.
b) Wanafunzi ambao watajifunza mafunzo meme watanufaika
sana.
c) Gari ambalo liliibwa limepatikana.
Sehemu zote zilizokolezwa ni vishazi tegemezi kwa kuwa kuna matumizi ya virejeshi.
4) Iwapo kuna matumizi ya baadhi ya viunganisha vya kinyume kama vile; ijapokuwa, ingawa, ijapo kwa mfano,
a) Ingawa Khadija hafanyi vyema masomoni, ana bidii nyingi.
b) Ijapokuwa watoto walihadithiwa hadithi za mazimwi,
hawakuogopa.
Sehemu zote zilizokolezwa wino ni vishazi tegemezi.


Hitimisho
Mwanafunzi umetambua kuwa vishazi huru huweza kujisimamia,kimaana,ilhali vishazi tegemezi huhitaji vishazi vingine ili maana ikamilike.


Yambwa/Shamrisho
Maana ya yambwa/shamirisho
Yambwa ni neno linaloonyesha kitendwa au kitendewa. Aghgalabu yambwa hupatikana katika kikundi kitenzi. Yambwa huwa nomino au kiwakilishi chake ambacho hupokea kitendo katika sentensi. Kwa mfano, Mama amepika
chakula. Chakula ni yambwa kwa sababu ndiyo nomino inayopokea kitendo katika sentensi.

Aina za yambwa au shamirisho

Kuna aina tatu za yambwa:
a) Yambwa tendwa/shamirisho kipozi
b) Yambwa tendewa/shamirisho kitondo
c) Yambwa ala/kitumizi/shamirisho ala/kitumizi
Yambwa tendwa / shamirisho kipozi
Yambwa tendwa/shamirisho kipozi ni nomino ambayo hupokea athari ya kitendo cha kiima moja kwa moja katika sentensi.
Mariga ameupiga mpira.
Mpira ndio yambwa tendwa/shamirisho kipozi kwa kuwa mpira ndio unaopokea athari ya kitendo cha Mariga yaani kule kupigwa.

Yambwa tendewa/ Shamirisho kitondo
Yambwa tendewa/ Shamirisho kitondo ni kitendewa katika sentensi. Kitondo ni nomino ambayo hunufaika au huhasirika na vitendo vya kiima/ mtenda katika sentensi.
Kwa mfano,
a) Mwalimu alimsahihishia
mwanafunzi insha.
b) Mengo alimfundisha kazi
Kazo.
Katika mfano wa kwanza, mwanafunzi ndiye anayenufaika na kitendo cha mwalimu (yaani kusahishiwa insha) huyo ndiye kitondo/yambwa tendewa.
Katika mfano wa pili, Kazo ndiye kitondo kwani ndiye anayenufaika na vitendo vya Mengo (mtenda).
Kitondo huweza kutokea kama kiwakilishi cha nomino, kwa mfano,
a) Salome ame
niandikia insha nzuri.
b) Jedida ame
kuletea embe tamu.
c) Wanafunzi wata
walimia mashamba.
Katika mifano hii,
ni, ku na wa ni viwakilishi nafsi viambata vinavyosimamia nomino inayonufaika katika sentensi, hivyo ni kitondo/yambwa tendewa.


Shamirisho ala/yambwa ala/kitumizi

Shamirisho ala/kitumizi/yambwa ala huwa ni kile kifaa au kitu ambacho hutumiwa kufanikisha kitendo fulani katika sentensi. kwa mfano,
1) Wanafunzi walisoma kwa bidii.
2) Wanafunzi waliimba kwa furaha.
Mifano hii inaonyesha matumizi ya vifaa/ dhana za kufikirika tu.
Mifano ya ala/vitumizi halisi ni kama - gari la moshi na kalamu katika sentensi zifuatazo;
1) Watalii walisafiri kwa gari la moshi.
2) Mwalimu anaandika kwa kalamu ya wino.

Hitimisho
Mwanafunzi umetambua kwamba yambwa ni sawa na shamirisho na kuwa shamirisho kipozi ni yambwa tendwa. Vilevile shamirisho kitondo ni sawa na yambwa tendewa. Pia shamirisho ala\ kitumizi ni sawa na yambwa ala /kitumizi

Shabaha

Kufikia mwisho wa kipindi uweze,
1. Kutaja aina tatu za sentensi.
2. Kutofautisha sentensi sahihi, ambatano na changamano.
3. Kuandika mfano wa sentensi sahili, ambatano na
changamano.

Aina za sentensi
Kwa kuzingatia muundo kuna aina tatu za sentensi
1. Sahili
2. Ambatano
3. Changamano

Sentensi sahili
1. Huwa ni kiima na kiarifa kimoja.
kwa mfano,
a) Mvua
inanyesha.

b) Juma anacheza.
c) Mwandishi stadi ameandika riwaya nzuri.
2. Huwa sentensi ya neno moja au fungu tenzi.
kwa mfano,
a) Ananitafutia.
b) Wametahadharisha.
3. Baadhi ya sentensi za kuamrisha huwa sentensi sahili.
Kwa mfano,
i. Imbeni!
ii. Chezeni!
iii. Tulizeni !
iv. Inameni !

Sentensi ambatano
1. Sentensi ambatano huwa na vishazi huru viwili au zaidi vilivyounganishwa kwa viunganishi.
Sentensi ambatano huwa na kiima na viarifu viwili au zaidi.
Umbo la sentensi ambatano huwa kama ifuatavyo,
S--------
S1 + U + S2 ----Sentensi huwa na sentensi mbili zilizounganishwa kwa kiunganishi.
Kwa kuzingatia umbo hili ni wazi kuwa sentensi ambatano huwa na sentensi sahili au zaidi zilizounganishwa
Kwa mfano,
a) Nimefika sokoni lakini sijamwona.
b) Mtampei anajivunia utamaduni wake ingawa alikaa uzunguni kwa miaka kumi.


Chagizo(CH)
Hii ni sehemu ambayo huja baada ya kitenzi. Chagizo huwa ni kielezi au kirai elezi au kirai husishi ambacho hufanya kazi kama kielezi.
Chagizo huwa si lazima kuwepo katika sentensi.
Kwa mfano,
Ukikawia utaachwa
hapa tu.
Hapa tu ni chagizo. Hata hivyo si lazima iwepo ili sentensi hii iweze kujisimamia. kwa mfano,
a) Juma atamtembelea nyanya
kesho jioni.
b) Tutakula chajio
kabla ya saa moja.
Ni muhimu kukumbuka kwamba chagizo hutokea baada ya yambwa au shamirisho. Ikitokea kabla ya shamirisho huwa kielezi.kwa mfano,
Mwanafunzi alisoma
kwa bidii na kupita mtihani vizuri.
Kwa bidii- ni kielezi cha kawaida.
vizuri - ni chagizo.

Sentensi changamano
Sentensi changamano huwa na kishazi kimoja huru na kingine kishazi tegemezi.
Kwa mfano,
Mama aliyatupilia mbali matunda yaliyooza.
Pia sentensi changamano huweza kuundwa kwa vishazi viwili tegemezi.
kwa mfano,
Wangalisikiliza ushauri wangaliepuka matata.

Sentensi ambazo huwa na 'o' rejeshi au kirejeshi 'amba' huwa ni sentensi changamano.
kwa mfano,
1. Mfumo wa kisiasa ambao umependekezwa katika katiba mpya ni ugatuzi.
2. Mwalimu aliyejitolea kazini amepandishwa cheo.

Shabaha

Kufikia mwisho wa somo hili,unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
1.Kufafanua maana ya uchanganuzi wa sentensi.
2.Kuchanganua sentensi kwa vielezo vifuatavyo,
a. Matawi
b. Vistari
c. Jedwali


Uchanganuzi wa sentensi

Hii ni hali ya kuigawa sentensi katika vijenzi vyake kimuundo kutoka kwa sehemu kubwa hadi ndogo.
Uchanganuzi wa sentensi sahili kwa mchoro wa matawi
Uchanganuzi wa sentensi sahili kwa njia ya mstari.


Sentensi Ambatano
Uchanganuzi wa sentensi ambatano kwa mchoro wa matawi.Uchanganuzi wa sentensi ambatano kwa mtindo wa Jedwali.Sentensi Changamano

Uchanganuzi wa sentensi changamano kwa mchoro wa matawi
Uchanganuzi wa sentensi changamano kwa mtindo wa mstari.
1.Haki za watoto zilizopuuzwa zamani zinazingatiwa sasa.
S- KN+KT
KN- N+V+N
N- Haki
V- za
N- watoto
S- zilipuuziliwa zamani
KT- T+E
T- zinazingatiwa
E- sasa


SHABAHA

Kufikia mwisho wa kipindi,utaweza:
1. Kufafanua kikundi nomino na kikundi kitenzi
2. Kutumia mikondo tofauti ya kikundi nomino na
kikundi kitenzi katika sentensi
3. Kubainisha kikundi nomino na kikundi kitenzi katika
sentensi

Muundo wa sentensi
Muundo wa sentensi hurejelea umbo la sentensi.
Kimisingi sentensi huwa na sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza ni
kikundi nomino (KN) na sehemu ya pili ni kikundi kitenzi (KT).
Sehemu ya kikundi nomino ni ile inayokaliwa na mtenda au mtendwa na sehemu ya kikundi kitenzi ni ile iliyo na kitenzi au kiarifa
Kwa mfano:
Kamau analala.

Hitimisho
Ni muhimu kielewa miundo ya vikundi nomino na vikundi tenzi ili uweze kuvitumia katika kuunda na kuchanganua sentensi kwa njia mwafaka.


Nyakati/Hali ya ukanushaji

Nyakati/Njeo hutumiwa kuonyesha wakati wa kufanyika kitendo. Kuna nyakati tatu kuu :
1.Wakati uliopita,kiambishi (LI),
2.Wakati uliopo ,kiambishi (NA),
3.Wakati ujao (TA).
Viambishi hivi vya nyakati huchopekwa katika vitenzi.
Kwa mfano, kiambishi cha wakati uliopita katika sentensi Alicheza (wakati uliopo), Anacheza( wakati uliopita) , Atacheza(wakati ujao).

WAKATI ULIOPO

i) Musa anaruka kamba.

ii) Mkulima anapalilia mimea yake.

iii) Kongowea anasukuma rukwama.

iii) Fatuma anasoma kitabu.

Dhana ya wakati au njeo huonyesha pia wakati wa kutotendeka kwa kitendo.

i) Musa haruki kamba.

ii) Mkulima hapalilii mimea yake.

iii) Kongowea hasukumi rukwama.

iv) Fatuma hasomi kitabu.

Wakati uliopita


1.Bahari ilichafuka tukaogopa.
2.Kiswahili kilienea kwa kasi barani.
3.Wanagenzi walienda kwa tamasha za muziki.
4.Wakenya wachache walipiga kura ya maoni.
5.Jana tulitembelea makao ya mayatima.


Hali ya ukanushaji
1.Bahari haikuchafuka wala hatukuogopa.
2.Kiswahili hakikuenea kwa kasi barani.
3.Wanagenzi hawakuenda kwa tamasha za muziki.
4.Wakenya wachache hawakupiga kura ya maoni.
5.Jana hatukutembelea makao ya mayatima.

Wakati Ujao


1.Maarusi watakapowasili tamasha zitaanza.
2.Waumini wataomba na kutubu kabla ya ibada kuanza.
3.Watu wote watasafiri kwa ndege kuenda Marekani.
4.Washindi watapewa zawadi na mgeni wa heshima.
5.Wanajeshi watapita kwa taadhima mbele ya jukwaa.

Hitimisho

Imedhihirika kwamba dhana ya nyakati hutokea kama kiambishi katika kitenzi.Ukanushaji pia huonyeshwa kwa kiambishi.Kiambishi cha wakati uliopo 'na' hutoweka wakati wa kukanusha.
Aghalabu kiambishi cha wakati hakitumiwi lakini katika wakati uliopita na wakati ujao, viambishi vya wakati na vya kukanusha hutumiwa.

Hitimisho

Imedhihirika kwamba dhana ya nyakati hutokea kama kiambishi katika kitenzi.Ukanushaji pia huonyeshwa kwa kiambishi.Kiambishi cha wakati uliopo 'na' hutoweka wakati wa kukanusha.
Aghalabu kiambishi cha wakati hakitumiwi lakini katika wakati uliopita na wakati ujao, viambishi vya wakati na vya kukanusha hutumiwa.

aaa

Funzo

Imedhihirika kwamba dhana ya wakati hutokea kama kiambishi katika kitenzi.Ukanushaji pia huonyeshwa kwa kiambishi,hata hivyo,katika wakati uliopo,kiambishi cha ukanushaji huchukua nafasi ya kiambishi cha wakati.Aghalabu kiambishi cha wakati hakitumiwi lakini katika wakati uliopita na wakati ujao, viambishi vya wakati na vya kukanusha hutumiwa.

 

Hali

Hali vilevile huonyeshwa kwa viambishi vinavyochopekwa katika mzizi wa kitenzi. Viambishi vya hali huonyesha utendekaji wa kitendo. Hali huelezea namna ya kutendeka kwa tendo kama vile:
i) Kitendo hufanywa kwa mazoea kwa mfano,
Mimi husoma Kiswahili.
ii) Kama kitendo kimekamilika kwa mfano,
Umesoma sana ukapasi mtihani.
Kuna hali nyingi katika lugha ya Kiswahili kwa mfano,
Hali timilifu, hali ya mazoea, hali ya nge, hali ya ngeli, hali ya ngali, hali ya -ki, hali ya -ka, hali ya -;a, hali ya -po, na hali ya -ku.


Sikiliza na kuyazingatia maelezo yafuatayo kuhusu hali ya -ki.
Hiki ni kiambishi ambacho hutumiwa kuonyesha hali mbalimbali kwa mfano,
i) Masharti
Kiambishi '-ki'huonyesha masharti ambayo yanawezekana, huenda yakawezekana masharti fulani yakitimizwa.
kwa mfano,
Tunaposema- ukila sana utaumwa na tumbo,ina maana kuwa hujala sana kwa hivyo hutaumwa na tumbo. Hata hivyo,kuna uwezekano wa wewe kula sana na hivyo basi kuumwa na tumbo.

Mifano katika sentensi.


1.Ukienda sokoni utakumbana na fujo.


2.Ukiuliza swali zuri utajibiwa.


3.Faida akipika wali atatupakulia.


4.Zena akipigania kiti cha ubunge nitampa kura.


5.Rais akija kwetu atatoa hotuba.
Ukanushaji

Katika ukanushaji, nafasi ya ki ya masharti huchukuliwa na kiambishi cha kukanushia ilhali ki ya hali ya kuendelea hutumiwa sambamba na viambishi vya hali ya kukanusha kwa mfano:
Amekuwa akisoma kwa sauti tangu jana. Inakuwa;
Hajakuwa akisoma tangu jana.

Hali ya'KA'

Kiambishi ka hutumiwa kuonyesha mfuatano wa matukio au vitendo. Aghalabu hutumiwa pamoja na wakati uliopita kuonyesha mfuatano wa vitendo kwa mfano:
Mama aliingia maliwatoni, akamtazama mwanawe, akatikisa kichwa, akakurupuka akaondoka polepole, akaenda zake.
Kiambishi ka pia hutumiwa kuonyesha kwamba kitendo kimoja kinasababishwa na kitendo kingine au ni matokeo ya kitendo kingine kwa mfano:
Mtoto huyo alicheza vizuri akapongezwa.

ka hutumiwa vilevile kuonyesha matarajio ya kufanyika kwa jambo fulani kwa mfano:
Nitakwenda nikamsalimie bibi yangu.
ka hutumiwa kuleta wazo la kuamrisha au rai. kwa mfano:
1.Kaingie ndani ya nyumba.(amri)
2.Njoo ukanijulie hali.(rai)

Hali ya A

Kiambishi -a hutumiwa kwa maana tofauti tofauti.Hata hivyo hakionyeshi wakati maalum wa kutendeka kwa jambo.Aghalabu huonyesha maana zifuatazo.
i)Hutumiwa pamoja na vitenzi vya hali kama vile soma,lima , kuleta dhana ya mazoea.
Kwa mfano;
a)Mtoto apenda kusoma.
b)Mkulima alima shamba.

ii)Kuonyesha jambo ambalo latokea kama kawaida ya maumbile. kwa mfano
a)Jua lachomoza mashariki.
b)Maji ya bahari yajaa magharibi.

iii)Kuandika ripoti au kujuza kilichotokea,tulichosikia,tulichosoma. kwa mfano
a)Baba asema atasafiri.
b)Wakenya wapiga kura ya maoni.

iv) kuonyesha kitendo kinatendeka sasa lakini bila kudhihirisha hali. kwa mfano
a) Wachezaji wacheza uwanjani.
b) Moto wawaka msituni.

v) Kuonyesha kitendo kinatarajiwa kufanyika baadaye. kwa mfano,
a) Mtihani waanza juma lijalo.
b) Wasafiri wafika alhamisi.


Hitimisho

Katika kipindi hiki, unaweza kuona kwamba nyakati huonyesha ni lini kitendo kilitokea na hali huonyesha ni vipi tendo lilitokea. Viambishi vya wakati vinaweza kutumiwa pamoja na viambishi vya hali katika sentensi moja ila wakati uliopo. Kuna viambishi vitatu vya ukanushaji ambavyo ni: si, hu na ha.

Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu