KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kuandika - Kiswahili Kidato Cha 4

Kufikia mwisho wa kipindi unatarajiwa kuweza :

a) Kueleza maana ya viunganishi
b) Kutambua aina za viunganishi
c) Kutumia aina mbalimbali za viunganishi katika sentensi.

Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuweza:

a) Kueleza maana ya mazingira
b) Kuangazia aina mbalimbali za mazingira
c) Kufafanua umuhimu wa mazingira
d) Kueleza njia mbalimbali za kuhifadhi mazingira

Mazingira ni hali au mambo yaliyomzunguka kiumbe pale anapoishi kama vile hali ya anga, ardhi, majumba, miti, mito na bahri.

Hebu tuone aina mbalimbali za mazingira ambayo huwa yanatuzunguka.

Mazingira huwa na manufaa mengi kwetu. Kwa mfano:

Maji: Maji ambayo tunapata kutoka kwa mito na maziwa hutumiwa kwa njia nyingi kama vile, kunywa, kuvulia nguo, kupikia, kunyunyizia mimea..Hebu tazama vibonzo vifuatavyo:

Milima na mabonde huweza kuwa vivutio vya watalii na kutupa fedha za kigeni. Vile vile, hutupa mandhari ya kupendeza. Milima pia huvuta mvua.

Licha kuwa mazingira yana faida chungu nzima, huharibiwa kwa njia mbalimbali kama vile:

a) Moshi kutoka viwandani huchafua hewa.
b) Ukataji ovyo wa miti husababisha kuwe jangwa hivyo kukauka kwa mito na maziwa.
c) Utupaji ovyo wa taka hufanya mandhari kuwa chafu na kuleta maradhi.
d) Kumwaga taka katika mito, maziwa na bahari.

Mazingira yanaweza kuhifadhiwa kwa njia tofauti. Njia hizo ni kama zifuatazo:

a) Kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa mazingira ili waweze kuyahifadhi.
b) Kupanda miti zaidi.
c) Kunadhifisha mazingira.
d) Kuwa na sera au sheria ambazo zinatetea uhifadhi wa mazingira.

Shabaha
Kufikia mwisho wa kipindi, unapaswa kuwa na uwezo wa:
i) kueleza maana ya memo
ii) kufafanua umuhimu wa memo
iii) kupambanua sifa za memo
iv) kuandika memo

Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
i) kueleza maana ya insha ya maelekezo au maagizo
ii) kutaja umuhimu wa insha za maelekezo
iii) kufafanua sifa za insha ya maelekezo
iv) kubainisha aina za maelekezo
v) kuandika insha ya maelekezo.

Memo
Umeona na kusikia nini? (P)

Bila shaka umeona maandishi na kusikia ujumbe maalum wa mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu anawaandikia wanafunzi wake. Barua hii imepachikwa ukutani.

Barua hii huitwa memo au arifa.
Memo ni taarifa fupi ya kiofisi ambayo hutoka kwa mtu mmoja hadi kwa wengineMuundo wa memo

Memo huwa na hatua tano muhimu ambazo lazima zijitokeze.


1. Anwani ya shirika hutangulia na huandikwa sehemu ya juu ya karatasi.


2. Neno 'MEMO' hufuata kwa herufi kubwa na kukolezwa wino.


3. Upande wa kushoto chini ya mstari huandikwa utangulizi ufuatao:
a) Kwa: sehemu hii huelezea ujumbe unalenga akina nani,
b) Kutoka: sehemu hii huonyesha ujumbe umetoka kwa nani,
c) Tarehe: sehemu hii huonyesha tarehe memo ilipoandikwa,
d) Mintarafu: hapa shabaha ya barua hudokezwa kwa herufi kubwa zilizokolezwa wino.


4. Mwili wa memo au maelezo ya mada inayoshughulikiwa huendelezwa


5. Hitimsho la memo hubeba sahihi, jina na cheo cha mwandishi.Tazama mfano huu:Kufikia mwisho wa kipindi hiki unatarajiwa unatarajiwa kuwa na uwezo wa :


1. kueleza maana ya barua kwa mhariri
2. kufafanua ujumbe katika barua kwa mhariri
3. kueleza sifa za barua kwa mhariri
4. kutaja umuhimu wa barua kwa mhariri

Barua kwa mhariri huwa na sifa zaidi ya zile za kimuundo. Baadhi ya sifa hizi ni:

i) huonyesha hisia au mtazamo wa mwandishi
ii) huwa na msimamo mmoja madhubuti,
iii) urefu wake hutegemea jambo ambalo linazungumziwa
iv) lugha rasmi hutumiwa
v) lugha nyepesi ya moja kwa moja isiyohusisha tamathali wala mafumbo

Barua kwa mhariri zina umuhimu kwa jamii kwa jumla. Huwapa wananchi kujieleza waziwazi. Huangazia mambo muhimu yanayofaa kutekelezwa. Hutumiwa kuwakilisha maoni ya watu kwa viongozi mbalimbali ili kuimarisha au kurekebisha hali ya maisha nchini.


Umuhimu wa Maagizo

i. Maagizo huongoza anayefanya jambo kulitekeleza ipasavyo.
ii. Maagizo hutahadharisha, yanapofuatwa huepushia mtu madhara ambayo yangempata.
iii. Maagizo hudumisha nidhamu na utendakazi wa jambo fulani.
iv. Maagizo husaidia kuelewa jinsi kifaa kinavyofanya kazi.
v. Maagizo husaidia kulenga na kuhakikisha ubora.


Bila shaka umesikia jinsi maagizo yalivyo muhimu. Je, unaweza kutaja dhima zaidi za maagizo?

Sifa za Maagizo

Uandishi wa maagizo
Tazama na kusoma mfano huu wa maagizo.

MAAGIZO
1.Hakikisha simu hii ina vifaa vyote.
2.Fungua uchopeke kadi ya simu.
3. Chopeka seliumeme pahali pake.
4.Weka simu hii kwa stima ipate chaji tosha.
5.Betri ikishajaa chaji izibue kutoka kwa umeme.
6.Ianzishe kufanya kazi.

 


Kufikia mwisho wa kipindi, unatarajiwa kuweza:
a) Kueleza maana ya ratiba.
b) Kufafanua muundo wa ratiba.
c) Kuandika ratiba kwa kufuata muundo sahihi. Ratiba ni mpangilio wa matukio ya shughuli au hafla fulani kutegemea jinsi yanavyofuatana kiwakati. Kunazo aina kadha za ratiba kulingana na shughuli. Mifano:

Barua kwa mhariri

Barua kwa mhariri huwa na sifa za kimuundo kama ifuatavyo:


1. Anwani mbili ya mwandishi na mwandikiwa ambaye ni mhariri.
2. Mtajo, mfano Bw,Mhariri.
3. Mada au Kuhusu- sehemu huonyesha kiini cha barua.
4. Yaliyomo (mwili)- huhusu ujumbe husika maoni au msimamo wa mwandishi.
5. Hitimisho- kimalizio cha heshima. Sehemu hii huonyesha jina la mwandishi na sahihi yake. Pia yaweza kutaja mahali.


 Ratiba.
Ratiba ni mpangilio wa matukio ya shughuli au hafla fulani kutegemea jinsi yanavyofuatana kiwakati. Kunazo aina kadha za ratiba kulingana na shughuli. Mifano:

Highlight the following examples as they are mentioned.

a) Ratiba ya masomo
b) Ratiba ya mashindano
c) Ratiba ya sanaa na maonyesho
d) Ratiba ya arusi
e) Ratiba ya mazishi

Kufikia mwisho wa kipindi unatarajiwa kuweza:

a) Kueleza maana ya matangazo.
b) Kutaja na kufafanua sifa za aina mbalimbali za matangazo.
c) Kufafanua dhima za matangazo.
d) Kuandika aina mbalimbali za matangazo ukizingatia kanuni za utungaji.

Shabaha :
Kufikia mwisho wa kipindi, unatarajiwa kuweza:
a) Kueleza maana ya ratiba.
b) Kufafanua muundo wa ratiba.
c) Kuandika ratiba kwa kufuata muundo sahihi.

a) Matangazo ya matukio maalum
b) Tangazo la zabuni
c) Matangazo ya mikutano
d) Matangazo ya matokeo ya mitihani.

Mfano wa pili.

Ratiba ya vipindi vya mwalimu wa Hesabati na Kemia.
Shule ya Upili ya Kikwatani


Kufikia mwisho wa kipindi, unatakiwa kuweza:

a) Kueleza maana ya juu na ya ndani ya methali yoyote.
b) Kuandika kisa kinachoafiki methali uliyopewa.
c) Kuandika kwa ufasaha ukizingatia mtiririko ufaao wa hadithi.

Matangazo ya Kazi

Tangazo la KifoTangazo la Biashara
(kwa hisani ya safaricom )

Baada ya kuangalia au kutazama tangazo hili, umetambua kuwa hili ni tangazo la biashara.

Sifa
a) Kuna viambata vya lugha, kwa mfano, picha na nyimbo.
b) Lugha ya ushawishi, kwa mfano katika tangazo la Safaricom-
nafurahia.
c) Majina ya bidhaa na kampuni hutajwa.
d) Lugha ya chuku hutumiwa.
e) Kuna kusifu bidhaa.
f) Kuna matumizi ya sentensi fupi.

Methali.
Methali ni fungu la maneno lenye maana maalum. Fungu hili huwa na maana ya juu na ya ndani. Vilevile huwa na sehemu mbili.
Insha ya methali hufafanua methali kwa kutumia kisa au hadithi.Kisa hiki hueleza kikamilifu maana ya ndani ya methali.


Maelezo

Hebu sikiliza maelezo zaidi kuhusu uandishi wa insha hii.
Kabla ya kuanza kuandika insha ya methali, ni lazima uyazingatie mambo yafuatayo.

a) Uelewe maana ya juu na ya ndani ya methali. Kwa mfano,
Jifya moja haliinjiki chungu.

Maana ya ndani ni kuwa mtu pweke hawezi kufanya jambo likamilifu. Watu wakiungana wanaweza kufanya mengi, tena vyema.


Fimbo ya mbali haiui nyoka.

Maana ya ndani ni kuwa mtu aliyembali hawezi kukusaidia ukiwa na dharura ila yule aliye karibu.

b) Fikiria kisa kinachoafiki kikamilifu maana ya ndani ya methali.
c) Panga utaratibu wa kisa kuanzia mwanzo hadi mwisho.

d) Simulia kisa ukitumia msamiati ufaao na mapambo ya lugha ya
kuvutia kama vile misemo na methali. Vilevile, zingatia sheria
za kisarufi kama uakifishaji na aya.


Sifa za Insha ya Mawazo
Insha ya mawazo hutumia lugha ya mvuto.Huhitaji ubunifu wa hali ya juu na huhusisha wahusika wa kufikirika kuendeleza ujumbe wa mwandishi. Kisa huwa na mawazo ya kuaminika yaliyona uhalisia wa maisha. Insha ya mawazo huzingatia kanuni za sarufi na uwakifishaji wa makala. Msamiati hujikita katika mada husika. Insha hii huonyesha msimamo wa mwandishi na hujikita katika matukio ya kuwazia.


Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu