KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kusikiliza na Kuzungumza - Kiswahili Kidato Cha 4

MAANA NA UMUHIMU WA LUGHA

maana

Shabaha
Kufikia mwisho wa kipindi, unatarajiwa kuwa na uwezo wa:
1. Kufafanua maana ya katiba na sheria.
2. Kutaja baadhi ya sheria zinazotumika katika nchi ya Kenya.
3. Kutaja taasisi zinazohusika na kuunda na kutekeleza sheria.

UTANGULIZI

(provide a photograph of a copy of the constitution with a voice overstating the following)

Katiba ni sheria au kanuni zilizooanisha namna amnayo nchi, chama au shirika inavyoendesha shughuli zake. Katiba ya nchi ni sheria inayooanisha misingi ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba hubainisha haki za wananchi.
Kidemokrasia katiba inafaa kubatilishwa baada ya kufanyiwa marekebisho yanayokubalika na wananchi kwa jumla. Nchini Kenya tangu kupata uhuru tumekuwa tukitunia katiba iliyoundwa zama za wakoloni. Mwaka wa 2010 wananchi walipata fursa ya kubadilisha katiba hiyo na kuchagua iliyobatilishwa ili kuwafaa kupitia kura ya maoni.
(provide a video clip of the promulgation ceremony of the new constitution at uhuru park on 27th august 2010.)

Katiba mpya nchini Kenya inafafanua haki za kimsingi za wananchi kam vile: haki ya kuishi, usawa na uhuru, usalama wa wananchi, uhuru wa dhamiri na imani ya dini na maoni. Katiba mpya inawapa wakenya uhuru wa kujieleza.

(provide a video clip of human rights activists demonstrating. )

Pia katiba mpya inalinda wnahabari kwa kuwapa uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya habari. Katiba mpya inaendeleza utamaduni na lugha za kiasili. Haki za wafungwa zinazingatiwa kwa mujibu wa kanuni za kibinadamu, kwa mfano, masilahi ya wafungwa yanazingatiwa pia wamepewa haki ya kuchagua wawakilishi wa eneo bunge lao.
Raia kwa jumla wanalindwa na katiba katika maswala ya ndoa, jinsia, urithi, ajira na dini ambapo wanawake na wanaume wanahaki sawa katika nyanja tatu za maisha mathalan kiuchumi, kijamii na kisiasa.

(provide photography of male and female personalities exercising their duties in different capacities.)

Wanasheria hutunga na kujadili sheria za nchi. Sheria ya katiba huhusisha sheria za umma na zile za kibinafsi za wananchi ilhali sheria za kimataifa hutawala shughuli za kibiashara, vikwazo vya kimazingira na mipaka, ulinzi n.k. baina ya nchi na nchi. Katika demokrasia halisi, sheria hutafsiriwa na matawi matatu makuu mahakama, bunge naserikali ya kuwajibika. Matawi haya ndiyo huunda vyombo vya dola vinavyohakikisha uzingativu wa sheria nchini. Kamati na idara tofauti za bunge na serikali huhakikisha sheria zinazoundwa zinatekelezwa vilivyo.
Katiba mpya inasisitiza haki za watoto kwa kuhakikisha kuwa mtoto anapata kuelimika, kutunzwa vyema na hadhulumiwi. Mtoto haruhusiwi kutengwa na wazazi wake kwa njia yoyote.

(provide pictures of children in school, a good home setup and play ground )

Aidha sheria hutilia mkazo matumizi ya lugha nchini. Katiba mpya inatambua aina tatu za lugha nchini, lugha rasmi, lugha ya taifa na lugha zingine kama vile za kiasili,ishara na Braille.
Ni dhahiri kuwa bunge linajukumu la kujumuisha maoni ya vikundi tofauti vya jamii katika kuimarisha sheria zilizoundwa katika katiba.

Memo

(Provide an animation of a student reading a memo on a notice board at the administrative office with a voice over of the following:)

SHULE YA UPILI YA MADIVINI
S.L.P 1234 009
KIKWAO
SIMU: +254 056 5101600
BARUAMEME: madyhigh@yahoo.com

MEMO
_________________________________________________________

KWA: WANAFUNZI
KUTOKA: MWALIMU MKUU
TAREHE: MACHI 12, 2011

KUH: MATOKEO YA MTIHANI WA KCSE 2010

Kutokana na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, ningependa kuwaarifu kuwa shule yetu imeweka rekodi ya ushindi kuibuka nambari tano kati ya shule ishirini bora nchini.

Kwa niaba ya Halmashauri ya shule , ningependa kuwapongeza walimu na wanafunzi kwa kazi nzuri iliyotuletea ufanisi wa kiwango hiki.

Ili kuhakikisha tunadumisha matokeo bora shuleni, kila mmoja wetu anapaswa kuzingatia nidhamu, kutumia vyema mema ya wakati, maktaba na vifaa vyote vilivyomo na kuzidisha juhudi zetu katika utendaji kazi ili kufikia malengo yetu.

Elekezi Robai
Mwalimu mkuu.

Umeona na kusikia nini? (P)

Bila shaka umeona maandishi na kusikia ujumbe maalum wa mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu anawaandikia wanafunzi wake. Barua hii imepachikwa ukutani.

Barua hii huitwa memo au arifa.
Memo ni taarifa fupi ya kiofisi ambayo hutoka kwa mtu mmoja hadi kwa wengine

Sifa za Memo

Memo huwa na sifa zifuatazo:
1. Hutangulizwa kwa anwani
2. huwa na ujumbe maalum
3. Huwa na umbo la kipekee
4. Walengwa wa habari hubainishwa
5. Mwandishi hubainishwa.
6. Mwandishi wa memo hutia sahihi
7. Huwa na sehemu tano kuu: anwani, utangulizi, Mintarafu, ujumbe, mwandishi
8. Huwaandikwa kwa karatasi maalum
9. Neno memo huandikwa kwa wino uliokolezwa
10. Huwa salamu hazitolewi.

Umuhimu wa memo

(Provide an animation of two students, a boy and a girl, discussing as follows beside a notice board with many notices on)

GIRL: Ubao huu una arifa nyingi leo Shamir.

BOY: Kweli. Memo huwa na dhima kubwa sana hasa katika kujuza ujumbe. Hii ndiyo sababu zimepachikwa nyingi labda.

GIRL: Nafikiri ni njia rahisi ya kuwasiliana katika shirika lo lote lile.

BOY: Kweli Maria. Unaona (pointing on the memo) kama hii inatuonya sisi dhidi ya matumizi mabaya rasilmali ya shule yetu.

GIRL: Shamir, hii nayo (pointing to the memo) inatushauri tufanye kazi kwa bidii mwaka. Angalia, imeandikwa, Wanafunzi wote mnatarajiwa kuzidisha juhudi zenu maradufu ili mfaulu katika masomo yenu.

BOY: Lo! Tazama nayo hii hapa. (Pointing to another). Inaelekeza matumizi ya vizima moto. Hii nafikiri imesababishwa na visa vya moto katika shule kadhaa. Ni vizuri kila mwanafunzi kufahamu kutumia vifaa hivi.Aidha tufunzane wenyewe kwa wenyewe ili mkasa kama huu ukitokea tuweze kukabiliana nao.

GIRL: Memo zina umuhimu mwingi tu. Huwa zinakumbusha walengwa wajibu wao kazini, kuweka kumbukumbu ya mambo yaliyojadiliwa na kufahamisha sera za shirika au taasisi kama hii yetu.

BOY: Ala! Kumbe. Maria wewe unafahamu vizuri .

GIRL: Ah! Mimi nimesoma mambo hayo mwenyewe. Vitabu vingi vinaelezea kuhusu memo.

MUUNDO WA MEMO

(Provide animation of a male teacher and student outside a classroom discussing as
follows:)

TEACHER: Hujambo Sophia!
SOPHIA: Sijambo Mwalimu.
TEACHER: Mbona umetoka darasani?
SOPHIA: Tafadhali mwalimu nilikuwa naja kukuona. Naomba unielezee muundo wa memo.
TEACHER: Oh! Hilo tu?
SOPHIA: Hilo tu mwalimu.
TEACHER: Ni muhimu ufahamu kwanza memo ni nini.
SOPHIA: Mwalimu nafahamu maana ya memo na hata umuhimu wake. Nataka kujua kuiandika.
TEACHER: Vizuri sana Sophia. Wewe ni mwanafunzi makini sana. Juhudi zako hizi zitakufikisha mbali.

Memo huwa na hatua tano muhimu ambazo lazima zijitokeze.


1. Anwani ya shirika hutangulia na huandikwa sehemu ya juu ya karatasi.


2. Neno MEMO hufuata kwa herufi kubwa na kukolezwa wino.


3. Upande wa kushoto chini ya mstari huandikwa utangulizi ufuatao:
a) Kwa: sehemu hii huelezea ujumbe unalenga akina nani,
b) Kutoka: sehemu hii huonyesha ujumbe umetoka kwa nani,
c) Tarehe: sehemu hii huonyesha tarehe memo ilipoandikwa,
d) Mintarafu: hapa shabaha ya barua hudokezwa kwa herufi kubwa
zilizokolezwa wino.


4. Mwili wa memo au maelezo ya mada inayoshughulikiwa huendelezwa


5. Hitimsho la memo hubeba Sahihi, jina na cheo cha mwandishi.


TEACHER: Sophia tazama mfano huu:
(Camera to focus on tthis text:)

KIWANDA CHA CHAI CHA MAEMBENI
S.L.P. 998646 00300
MAEMBENI
SIMU: +452 7220 707404 474
BARUAE: chaimaembeni@yahoo.com

MEMO
_____________________________________________________

KWA: WAFANYIKAZI WOTE
KUTOKA: MENEJA MKUU
TAREHE: MACHI 23, 2011

MINTARAFU: NYONGEZA YA MISHAHARA

Kiwanda chetu kimepata faida kubwa msimu uliopita. Mapato ya kifedha yameongezeka maradufu miaka miwili iliyopita. Hii inatokana na juhudi za kila mmoja wetu. Kwa niaba ya Halmashauri ya Wakurugenzi, nawapongeza sana kwa bidii yenu.

Kwa shukrani na pia kuwahimiza kujibidiisha zaidi, halmashauri ya wakurugenzi wa kiwanda hiki wamependekeza nyongeza ya mishahara yenu.

Wafanyikazi wa kiwango cha F na G watapata nyongeza ya asilimia 52. Wale wa kiwango cha H-J watapata nyongeza ya asili mia 21. Wafanyi kazi wa kiwango cha K- P watapata asilimia 8.

Ni matumaini yangu kuwa nyongeza hizi zitawapa motisha wa kufanya kazi hata zaidi. Kila hali ya Uchumi wa kiwanda unavyoimarika ndivyo wasimamizi watazidi kuchunguza na kuimarisha mishahara ya wafanyi kazi wake.


Abdulmajid Rajab.
(Mkurugenzi Mkuu)


SHUGHULI

Katika sehemu hii,utapata maelezo zaidi juu ya somo husika. Bonyeza mada yoyote kati ya zilizoorodheshwa ili ufaidi!


Katika sehemu hii, unatakiwa kubonyeza mazoezi yaliyoorodheshwa ili uweze kujipima iwapo umeyapata yaliyofunzwa katika somo. Vilevile, unaweza kuupima uelewaji wako wa mada hata kabla hujashughulikia mafunzo ili uweze kujua unayopaswa kutilia mkazo zaidi.

Maamkizi na Mazungumzo

Sajili ya Viwandani

Haya ni mazungumzo yanayohusiha.Matumizi ya lugha katika maeneo ya viwandani.Huhusisha mazungumzo kati ya wafanyakazi mbalimbali na wasimamizi wao.


Sikiliza na kutazama mazungumzo haya.
Bofya kifute cha pleya kusikiliza


Je, kufikia hapo, unafikiri mazungumzo haya yanahusu watu wa aina gani?

Bila shaka nataraji umegundua watu hawa wako kazini. Hawa wanafanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza sukari.

Kiwanda ni mahali ambapo mafundi au watu wenye ujuzi katika kazi maalum hufanya kazi ya kutayarisha bidhaa au vifaa fulani. Kuna aina nyingi za viwanda namna kulivyo na bidhaa mbalimbali.

Sajili inayotumika katika viwanda basi hutegemea shughuli za kiwanda husika,wafanyikazi hao na hata vyeo vyao.

Ni sifa gani za sajili hii zinazojitokeza katika mazungumzo haya?


Tazama video hii na kusikiliza mazungumzo.Bonyeza kifute cha pleya.


Unadhani mazungumzo haya ni kati ya akina nani?

Ndiyo, natumai umeona hawa ni wafanyikazi wa ngazi ya juu katika kiwanda.
Meneja mkuu ndiye kiongozi na wasaidizi wake ni meneja.

Lugha ya meneja inatofautianaje na ile ya Mkurugenzi mkuu?

Sajili ya viwandani ina sifa gani kutokana na mazungumzo haya?Hitimisho
Bila shaka umeweza kutambua sajili ya viwandani na sifa za sajili hii. Ni vyema ukifanya
utafiti zaidi ili kujua sifa za sajili ya viwandani kwa vile itakurahisishia mawasiliano
endapo utakumbana na hali hii. Waweza kutalii viwanda mbalimbali na kuchunguza kwa
makini wafanyikazi wa daraja mbalimbali wanavywasiliana.

Hitimisho
Bila shaka umeweza kutambua sajili ya viwandani na sifa za sajili hii. Ni vyema ukifanya utafiti zaidi ili kujua sifa za sajili ya viwandani kwa vile itakurahisishia mawasiliano endapo utakumbana na hali hii. Waweza kutalii viwanda mbalimbali na kuchunguza kwa makini wafanyikazi wa daraja mbalimbali wanavyowasiliana.


Bunge


ZOEZI

Mazungumzo Bungeni
Bonyeza na kusikiliza mazungumzo .

ZOEZI

Hitimisho

Imedhihirika kwamba sajili ya bunge ina sifa za kutumia istilahi maalum. Aidha lugha huwa ya kisheria na huzingatia nidhamu. Ili kuelewa zaidi sajili hii inakubidi kufuatilia mazungumzo hayo katika vyombo vya habari.


Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu