KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Kusoma kwa Mapana - Kiswahili Kidato Cha 4


Maelezo
Utandawazi au kuunganishwa kwa jamii kumechukua mitazamo miwili ya kinadharia. Kwanza, kuna kuunganishwa kwa ushirikiano wa kisiasa ambao ni wa nchi kuu kadhaa na mashirika makubwa ya kimataifa. Hali hii ndiyo huitwa uunganishwaji wa juu.Mtazamo wa pili ni ule wa uunganishwaji wa mashirika ya kiuchumi na nchi moja moja kuelekeza mitaji na fedha zake kwingineko. Uunganishwaji huu hufanyika kama hatua ya kupanua shughuli zake. Uunganishwaji huu ndio hutambulika kama wa chini.


Utandawazi
Bonyeza kucheza video.


Manufaa na matatizo ya utandawazi
Bonyeza na kutazama video iliyoko hapo chini.

Teknolojia ya habari na mawasiliano hushughulika na kuzalisha ,kuendesha, kuhifadhi, kuwasilisha na kusambaza habari.

Utandawazi una manufaa na matatatizo yake. Faida kubwa ni kwamba utandawazi umeimarisha maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa. Hali ya mawasiliano imeboreshwa zaidi miongoni mwa watu wanaokaa mbalimbali. Jamii katika ulimwengu wote zimepata kuunganishwa kiasi cha kufanya dunia kuwa kama kijiji.

Baadhi ya matatizo yanayotokana na utandawazi ni kupanuka na kusuasua kwa uchumi katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Nchi za Asia kusini na Mashariki na Marekani kusini ndizo zilizoathirika. Tatizo jingine ni kupanuka zaidi kwa utabaka kunakoletwa na uwezo wa kiuchumi na kisiasa.


Nchi zilizoendelea, na matabaka ya juu katika ulimwengu wa tatu ndizo hufaidika kwa utandawazi. Baadhi ya viongozi wa serikali na wasomi katika maeneo ya kiuchumi ambayo hayajaunganishwa katika utandawazi hujiona kama wamewekwa pembezoni- wametengwa.


Kumezuka makundi mawili, kundi linalopinga utandawazi na ambalo hudai kuwa utandawazi ni kama ukoloni mamboleo. Kundi hili huamini kuwa mataifa ya juuyana njama ya kuendeleza ukoloni kupitia kwa utandawazi. Kwa upande wa kundi linalounga wao hutaka kumiliki na kudhibiti rasilmali za dunia kupitia kwa utandawazi. Hali hii imeliudhi kundi la kwanza na kusababisha pingamizi yao kwa utandawazi.


Utandawazi umefanya dunia kuanza kuendeshwa kwa masharti mapya. Kwa mfano, sasa kuna mabadiliko katika utoaji wa huduma , Hivi kwamba imewalazimu watu kuchangia kugharamia maisha. Masoko pia yamefanywa kuwa huria. Kila eneo limejipa uwezo wa kujiamulia bei ya kuuza na kununua bidhaa.

Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa :


1. kueleza maana ya utandawazi
2. kueleza dhana kuhusu asili ya utandawazi
3. kujadili upeo na ufanisi wa utandawazi
4. kufafanua matatizo yanayotokana na utandawazi
5. kufurahia na kushiriki katika matumizi ya utandawazi


Kufikia mwisho wa kipindi unatararijiwa kuwa na uwezo wa:
i) kufafanua maana ya teknolojia
ii) kubainisha aina mbalimbali za teknolojia
iii) kueleza umuhimu wa teknolojia
iv) kufurahia kutumia teknolojia

SimuMaendeleo ya kiteknolojia ni mengi na yameenea katika nyanja zote za maisha ya
mwanadamu kama vile elimu, mawasiliano, uchukuzi, biashara, zaraa, utabibu, usalama,
ofisi n.k. Tazama mifano ifuatayo kasha baada ya kila sehemu ya mifano hiyo, utajibu
maswali yanayofuatia.

Aina za Maendeleo
Maendeleo ya kiteknolojia ni mengi na yameenea katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu kama vile elimu, mawasiliano, uchukuzi, biashara, zaraa, utabibu, usalama,ofisi na kadhalika. Tazama mifano ifuatayo.

Uchukuzi na mawasiliano

Tazama picha zifuatazo.

Biashara

Kuna mitambo mingine mingi na vifaa vya kiteknolojia vinavyotumiwa katika sekta ya biashara. Taja mifano zaidi mbali na hii iliyotolewa.Zaraa

Zaraa au sekta ya kilimo imesheheni matumizi ya kiteknolojia. Kila kukicha ndivyo uvumbuzi mpya unajitokeza. Utafiti unazidi. Umewahi kusikia kuhusu kutumbishwa kwa mifugo? Jaribu kutafuta makala zaidi ujisomee.

 

 


Mafunzo meme

Tazama picha hizi. Hawa wanafunzi wanafanya nini?


 

 


Matibabu

Sikiliza na kutazama mazungumzo haya.

Nyumbani
Tazama picha hiziTeknolojia ya nyumbani imerahisisha sana kazi za nyumbani. Tafuta makala zaidi kuhusu teknolojia hii ili upate maarifa zaidi.


Mazingira
Mazingira ni hali au mambo yaliyomzunguka kiumbe pale anapoishi kama vile hali ya anga, ardhi, majumba, miti, mito na bahari.

Hebu tuone aina mbalimbali za mazingira ambayo huwa yanatuzunguka.


Umuhimu wa Mazingira

Mazingira huwa na manufaa mengi kwetu. Kwa mfano:

Maji: Maji ambayo tunapata kutoka kwa mito na maziwa hutumiwa kwa njia nyingi kama vile, kunywa, kufulia nguo, kupikia, kunyunyizia mimea.
Hebu tazama picha zifuatazo:Miti
: Miti hutumiwa kwa njia mbalimbali. Miti hutupa chakula, mandhari ya kupendeza, hutupa mvua, hutumiwa kutengenezea dawa na vitu vingine vya matumizi ya nyumbani.

Hebu tazama picha zifuatazo:

 
Milima na mabonde
Milima na mabonde huweza kuwa vivutio vya watalii na kutupa fedha za kigeni. Vile vile, hutupa mandhari ya kupendeza. Milima pia huvuta mvua.

Hebu tazama picha zifuatazo:

 

 

 

 

 Uharibifu wa mazingira

Licha kuwa mazingira yana faida chungu nzima, huharibiwa kwa njia mbalimbali kama vile:

a) Moshi kutoka viwandani huchafua hewa.
b) Ukataji ovyo wa miti husababisha kuwe jangwa hivyo kukauka kwa mito na maziwa.
c) Utupaji ovyo wa taka hufanya mandhari kuwa chafu na kuleta maradhi.
d) Kumwaga taka katika mito, maziwa na bahari.

Tazama picha zifuatazo. 

Njia za kuhifadhi mazingira

Mazingira yanaweza kuhifadhiwa kwa njia tofauti. Njia hizo ni kama zifuatazo:

a) Kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa mazingira ili waweze
kuyahifadhi.
b) Kupanda miti zaidi.
c) Kunadhifisha mazingira.
d) Kuwa na sera au sheria ambazo zinatetea uhifadhi wa
mazingira.

 

 Katiba

Katiba ni sheria au kanuni zilizooanisha namna ambavyo nchi, chama au shirika inavyoendesha shughuli zake. Katiba ya nchi ni sheria inayooanisha misingi ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba hubainisha haki za wananchi.
Kidemokrasia katiba inafaa kubatilishwa baada ya kufanyiwa marekebisho yanayokubalika na wananchi kwa jumla. Nchini Kenya tangu kupata uhuru, tumekuwa tukitumia katiba iliyoundwa zama za wakoloni. Mwaka wa 2010 ,wananchi walipata fursa ya kubadilisha katiba hiyo na kuchagua iliyobatilishwa ili kuwafaa kupitia kura ya maoni.
Tazama video hii: (Kwa hisani ya KBC channel 1)


Katiba mpya nchini Kenya inafafanua haki za kimsingi za wananchi kama vile: haki ya kuishi, usawa na uhuru, usalama wa wananchi, uhuru wa dhamiri na imani ya dini na maoni. Katiba mpya inawapa wakenya uhuru wa kujieleza.

 

Pia katiba mpya inalinda wanahabari kwa kuwapa uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya habari. Katiba mpya inaendeleza utamaduni na lugha za kiasili. Haki za wafungwa zinazingatiwa kwa mujibu wa kanuni za kibinadamu, kwa mfano, masilahi ya wafungwa yanazingatiwa pia wamepewa haki ya kuchagua wawakilishi wa eneo bunge lao.
Raia kwa jumla wanalindwa na katiba katika maswala ya ndoa, jinsia, urithi, ajira na dini ambapo wanawake na wanaume wana haki sawa katika nyanja tatu za maisha mathalan kiuchumi, kijamii na kisiasa.

 


Wanasheria hutunga na kujadili sheria za nchi. Sheria ya katiba huhusisha sheria za umma na zile za kibinafsi za wananchi ilhali sheria za kimataifa hutawala shughuli za kibiashara, vikwazo vya kimazingira na mipaka, ulinzi na kadhalika, baina ya nchi na nchi. Katika demokrasia halisi, sheria hutafsiriwa na matawi matatu makuu mahakama, bunge naserikali ya kuwajibika. Matawi haya ndiyo huunda vyombo vya dola vinavyohakikisha uzingativu wa sheria nchini. Kamati na idara tofauti za bunge na serikali huhakikisha sheria zinazoundwa zinatekelezwa vilivyo.
Katiba mpya inasisitiza haki za watoto kwa kuhakikisha kuwa mtoto anapata kuelimika, kutunzwa vyema na hadhulumiwi. Mtoto haruhusiwi kutengwa na wazazi wake kwa njia yoyote.

 

 

 

Aidha sheria hutilia mkazo matumizi ya lugha nchini. Katiba mpya inatambua aina tatu za lugha nchini, lugha rasmi, lugha ya taifa na lugha zingine kama vile za kiasili,ishara na 'Braille'.
Ni dhahiri kuwa bunge linajukumu la kujumuisha maoni ya vikundi tofauti vya jamii katika kuimarisha sheria zilizoundwa katika katiba.Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu