KCSE ONLINE

Esoma Online Revision Resources

Sarufi na matumizi ya Lugha - Kiswahili Kidato Cha 4

Vivumishi ni maneno yanayotoa maelezo zaidi kuhusu nomino katika sentensi. Ni lazima kupatanisha vivumishi na nomino katika ngeli mbalimbali ili kuwa na sentensi sahihi kisarufi.

Upatanisho wa kisarufi

Upatanisho wa kisarufi ni hali ya nomino kukubaliana na kiambishi kiwakilishi cha nomino husika katika maneno ambayo huandamana na nomino hiyo katika sentensi kama vile vivumishi.



Hivi ni vivumishi vinavyoeleza nomino kwa njia za kipekee kila moja. Vivumishi hivi ni vya aina sita kama ifuatavyo: - ote, -o-ote, -enye, enyewe, -ingine, ingineo. Tazama mifano ya sentensi: Highlight by blinking the bold sections.

a) Wanafunzi wote wanastahili kuwa na nidhamu.
b) Tunda lolote linaboresha afya.
c) Mwalimu mwenyewe anawapenda watoto wake.
d) Bilauri nyinginezo zinahitajika.

Sasa tazama jedwali lifuatalo.

Highlight the letters written in bold

Ngeli nomino -ote -o-ote -enye -enyewe -ingine -ingineo
A
WA samaki
samaki wote
wote yoyote
wowote mwenye
wenye mwenyewe
wenyewe mwingine
wengine mwingineo
wengineo
U
I mswaki
miswaki wote
yote wowote
yoyote wenye
yenye wenyewe
yenyewe mwingine
mingine mwingineo
mingineo
LI
YA jino
meno lote
yote lolote
yoyote lenye
yenye lenyewe
yenyewe jingine
mengine jinginelo
menginyo
KI
VI kifurushi
vifurushi chote
vyote chochote
vyovyote chenye
vyenye chenyewe
vyenyewe kingine
vinginevyo kinginecho
vinginevyo
U-U ujasiri wote wowote wenye wenyewe mwingine mwigineo
I-I sukari Yote yoyote yenye yenyewe mwingine mwingineo
KU kuimba Kote kokote kwenye kwenyewe Kwingine kwingineko

Hivi ni vivumishi vinavyoonyesha au kuashiria ilipo nomino. Vivumishi vionyeshi pia huitwa viashiria.Vivumishi hivi ni vya aina tatu: vya karibu, vya mbali kidogo na mbali sana. Kwa mfano:

Bubble the examples below.

Vya karibu vya mbali kidogo vya mbali sana
mtu huyu mtu huyo mtu yule
kiti hiki kiti hicho kiti kile
jumba hili jumba hilo jumba lile

Hebu tazama jedwali lifuatalo.

Highlight the words under the four sections, nomino, vya karibu, vya mbali kidogo and vya mbali sana..

Ngeli Nomino Vya karibu Vya mbali kidogo Vya mbali sana
U
I mwiko
miko huu
hii huo
hiyo ule
ile
LI
YA jani
majani hili
haya hilo
hayo lile
yale
U
YA uasi
maasi huu
haya huo
hayo ule
yale
I
ZI darubini
darubini hii
hizi hiyo
hizo ile
zile
KU kushinda huku huko kule

zoezi


Sasa tazama jedwali lifuatalo:


Upatanisho wa kisarufi kati ya nomino na vivumishi hutokea kupitia viambishi vya ngeli au viambishi vya upatanisho wa kisarufi kama ulivyoona katika jedwali.


zoezi

Vivumishi vimilikishi

Hivi ni vivumishi ambavyo huonyesha umiliki wa au kuwa na kitu. Viambishi awali hubadilika kulingana na nomino inayomilikiwa na nafsi inayomiliki.

Tazama mifano katika jedwali lifuatalo:

 

 

Hebu tuone mifano zaidi katika sentensi.

a)Kalamu yangu ina wino mwekundu.

b)Kalamu yako ina wino wa rangi ya samawati.

c)Kalamu yake ina wino mweusi.

 


zoezi

Vivumishi viulizi

Hivi ni vivumishi vinavyouliza maswali kuhusu nomino. Vivumishi hivi vinapotumiwa katika sentensi ni sharti sentensi hiyo ikamilishwe kwa alama ya kiulizi.Vivumishi viulizi huwa ni vitatu: -pi?,-ngapi? na gani(ambacho hakiambishwi).Mifano ya vivumishi viulizi ni kama ifuatayo:

Mtoto yupi anapenda kusoma?

Mishipi gani inatumika kama sare ya shule yetu?

Vyumba vingapi vimesafishwa?

Uhalisia upi wa maisha unawafaa wanafunzi?

Mifano zaidi

Jengo lipi ni kubwa?

Ni mwanafunzi yupi hajavaa sare?

Viatu gani ni vya watoto?

Unga upi ni wa mahindi?


Sasa tazama mifano zaidi katika sentensi.


1.Kitabu kipi ni kizuri zaidi?

Vitabu vipi ni vizuri zaidi?


2.Papai lipi limeiva?

Mapapai yapi yameiva?


3.Uteo gani umenunuliwa na nyanya?

Teo gani zilinunuliwa na nyanya?


4.Maziwa gani yalinywewa na paka?


5.Wasichana wangapi walikuja?

6.Maradhi mangapi yalitibiwa?


zoezi

Vivumishi vya idadi

Hivi ni vivumishi vinavyotaja idadi ya nomino. Kuna vinavyotaja idadi maalum na vyenye kutaja idadi kwa jumla. Tazama mifano ifuatayo:
Vya kutaja idadi maalum:
Tembe mbili za dawa zilimezwa.


Viti vitatu vimetengenezwa.


Vya kutaja idadi jumla:

Chakula kingi kimebaki.


Maji mengi yamehifadhiwa.

Tazama jedwali lifuatalo;


Kutokana na jedwali imebainika kuwa viambishi vya upatanisho katika vivumishi vya idadi hutegemea aina ya kivumishi cha idadi na nomino inayohusika.


zoezi

Vivumishi vya A-unganifu

Hivi ni vivumishi vinavyohusisha nomino moja na nyingine. Vivumishi hivi huishia kwa herufi 'a'. Kwa mfano:


1.Mtu wa watu.
2.Chama cha wananchi.
3.Mizizi ya mimea.
4.Nyumba za wazee.
5.Gari la mwalimu.


zoezi

Vivumishi visisitizi.

Hivi ni vivumishi ambavyo husisitiza nomino fulani. Vivumishi hivi huundwa kwa kurudiarudia vivumishi vionyeshi.Visisitizi hujitokeza katika viwango vitatu:
Nomino ikiwa karibu; nomino ikiwa mbali kidogo nomino ikiwa mbali. Kwa mfano:

 


 


Tuangalie mifano zaidi katika sentensi.

 • Jiwe lili hili ndilo lililowafaa waashi.
 • Taarifa iyo hiyo ndiyo ilinipa matumaini.
 • Machungwa yale yale yaliwaburudisha watu.
 • Papa yuyo huyo ndiye aliyepikwa.
zoezi

Hivi ni vivumishi vinavyohusisha nomino moja na nyingine. Vivumishi hivi huishia kwa herufi ‘a’. Kwa mfano:

a) Mtu wa watu
b) Chama cha wananchi
c) Mizizi ya mimea
d) Nyumba ya wazee
e) Shule ya watu wote

Vivumishi vya pekee 

Hivi ni vivumishi vinavyoeleza nomino kwa njia za kipekee kwa kuwa kila kimojawapo huwa na maana mahsusi. Vivumishi hivi ni vya aina sita kama ifuatavyo: - ote, -o-ote, -enye, enyewe, -ingine, ingineo. Tazama mifano ya sentensi:



1.Wanafunzi wote wanastahili kuwa na nidhamu.


2.Tunda lolote huboresha afya.


3.Mwalimu mwenyewe anawapenda watoto wake.


4.Bilauri nyinginezo zinahitajika.


5.Kitabu chenye manufaa kimenunuliwa.

6.Maji mengine yanahitajika.


Sasa tazama mifano zaidi katika jedwali lifuatalo.


Blink the following examples.

Karibu mbali kidogo mbali

a) Mtoto yuyu huyu Mtoto yuyo huyo Mtoto yule yule
b) Gari lili hili Gari lilo hilo Gari lile lile
c) Nyumba zizi hizi Nyumba zizo hizo Nyumba zile zile


Highlight words in the three sections, karibu, mbali kidogo and mbali in different colours.

ngeli nomino karibu mbali kidogo mbali
U
I mfupa
mifupa uu huu
ii hii uo huo
iyo hiyo ule ule
ile ile
KI
VI kichuguu
vichuguu kiki hiki
vivi hivi chicho hicho
vivyo hivyo kile kile
vile vile
U-U urembo uu huu uo huo ule ule
YA-YA manukato yaya haya yayo hayo yale yale
KU kusoma kuku huku kuko huko kule kule

Vivumishi vionyeshi

 Hivi ni vivumishi vinavyoonyesha au kuashiria ilipo nomino. Vivumishi vionyeshi pia huitwa viashiria.Vivumishi hivi ni vya aina tatu: vya karibu, vya mbali kidogo na mbali sana. Kwa mfano:

Jedwali hili lina mifano zaidi ya viashiria.



Hapa kuna mifano zaidi katika sentensi.

a) Mama yule anaenda sokoni.
b) Kiti hiki ni cha mtoto.
c) Magoti yangu haya yanauma.
d) Ukuta huo una rangi gani?
e) Chai hii haina sukari.


Hitimisho
Hivi ni vivumishi vinvyoeleza nomino kwa namna ya kipekee kwa sababu kila kimoja wapo kina maana yake mahususi.



Viunganishi viongezi au vya kuongeza.

Viunganishi hivi huleta dhana ya 'zaidi ya'. Mifano zaidi ya viunganishi hivi ni: na, tena, pia, aidha, pamoja na, zaidi ya.
Tazama mifano ya sentensi zifuatazo,
1. Utulivu wake na bidii yake ilimfanya atuzwe katika hafla
hiyo.
2. Wanafunzi pamoja na walimu wao waliingia maabara.
3. Fatma aliruhusiwa kwenda Mombasa na wewe pia
utaandamana naye.

Viunganishi visababishi/vya sababu
Provide an animation of a male teacher reading this with a voice over

Viunganishi hivi hutoa sababu ya kutendeka kwa jambo. Huweza kutumiwa mwanzoni au katikati ya sentensi. Mifano ni ; kwa sababu,kwa vile,na kutokana na.


1. Wanafunzi walisherehekea kwa sababu ya matokeo yao bora( Provide an animation of students celebrating because of good results)


2. Kwa vile hakuwa na nauli hakuendelea na safari yake.




Kiunganishi cha asili ya kibantu

Kiunganishi ambacho ni cha asili ya kibantu ni 'na'.

kwa mfano,

1) Mtoto na mzazi wametoka shambani.
2) Waziri mkuu na naibu wake wanaelekea bungeni.

Viunganishi vya asili ya kigeni

Kuna viunganishi vya asili ya kigeni.
Mifano ni : fauka ya, ilhali, sembuse/seuze.

1) Zuleka anawasaidia majirani wake sembuse aila yake.
2) Nchi zinazoendelea zina uwezo wa kuyaboresha maisha ya
raia wake seuze nchi zilizoendelea!
3) Aliniagiza kwenda kwake ilhali hakunipa nauli.




Aina za vitenzi
Vitenzi hugawanyika katika makundi yafuatayo,vitenzi halisi,vikuu,visaidizi,vishirikishi na sambamba.
Vitenzi halisi
Hivi ni vile vinvyoarifu tendo linalotendwa na kitu chochote kile chenye uwezo wa kutenda.
Kwa mfano,

  • Mkulima analima shamba.
  • Watalii walizuru nchi yetu.
  • Abdul atatembelea Afrika kusini.
  • Mutua anasakura kwenye mtandao.
  • Faiza amempigia mama simu.

Vitenzi vikuu(T)

Kitenzi kikuu huelezea tendo kuu katika sentensi.Huhusisha ujumbe kwa usaidizi wa kitenzi kingine ambacho huitwa kitenzi kisaidizi.

Mifano


1.Marangi anapenda sana kupaka rangi.


2.Wanafunzi wamekuwa wakisoma tangu asubuhi.

Kitenzi kisaidizi

Hiki ni kitenzi ambacho huandamana na kitenzi kikuu. Kitenzi kisaidizi huwa na kazi ya kukisaidia kitenzi kikuu ili sentensi ilete maana kamilifu.

  • Mwalimu alikuwa anawafunza wanafunzi.
  • Umewahi kumwona fisi.
  • Amina alijitahidi kumbebea mzee huyo mzigo.
  • Hataenda kuoegelea mtoni.

Vitenzi Vishirikishi

Vitenzi vishirikishi ni vile ambavyo vinashirikisha kiima cha sentensi na kijalizo. Kwa mfano,

Kisu hiki ni kikali
Katika sentensi hii kisu ni kiima na kikali ni kijalizo. Kijalizo husaidia kukamilisha maelezo kuhusu kiima. Kwa mfano
Huyu ni mwalimu.

 1. Huyu ni kiima.
 2. Ni ni kitenzi kishirikishi.
 3. Mwalimu ni kijalizo.

Mifano mingine ni kama:
Hayo yalikuwa maneno mazito.
Hayo ni kiima.
Yalikuwa ni kitenzi kishirikishi.
Maneno mazito ni kijalizo.

Kuna aina mbili ya vitenzi vishirikishi

 1. Vitenzi vishirikishi vipungufu
 2. Vitenzi vishirikishi vikamilifu

Vitenzi vishirikishi vipungufu huchukua viambishi nafsi/vya ngeli. Vitenzi hivi havichukui viambishi vya njeo(wakati) na hali. Kwa mfano,


1.Otieno ni daktari.



2.Mwanafunzi yu darasani.
Vitenzi vishirikishi vikamilifu huchukua viambishi vya  njeo/wakati/hali/nafsi/ngeli,kwa mfano

 • Wanafunzi wanastahili kuwa darasani.
 • Wabunge walikuwa wangali bungeni.
 • Wanakijiji watakuwa wakihudhuria arusi.

Vitenzi Sambamba
Vitenzi sambamba ni vitenzi ambavyo hutokea katika mfululizo. Mfululizo wa aina hii unaweza kuleta pamoja kitenzi kisaidizi au kishirikishi na kitenzi halisi. Uweza pia kuhusisha vitenzi visaidizi kadha na kitenzi kikuu. Kwa mfano
1.Wanafunzi wanakimbia wakiimba uwanjani.
Wanakimbia ni kitenzi kikuu.
Wakiimba ni kitenzi kikuu.

2.Watahiniwa walikuwa wanataka kujiandaa kupita mtihani.
Walikuwa ni kitenzi kisaidizi.
Wanataka ni kitenzi kisaidizi.
Kujiandaa kitenzi kisaidizi.
Kupita kitenzi kikuu.

3.Wakulima  wangali wanalima.
Wangali ni kitenzi kisaidizi.
Wanalima ni kitenzi kikuu.


Kufikia mwisho wa kipindi unapaswa
1. Kufafanua maana ya vitenzi
2. Kubainisha aina za vitenzi
3. Kutumia vitenzi katika sentensi zoezi

zoezi

zoezi VITENZI KISAIDIZI

Kikundi Kitenzi

Hii ni sehemu ambayo huwa na kitenzi na pengine maneno mengine kama vile kielezi, shamirisho, kishazi tegemezi na kadhalika. Kitenzi chaweza kuwa kikuu, halisi, kishirikishi, au hata kisaidizi.
Kwa mfano,
Juma anaimba vizuri;
Mombasa ni mji safi;
Mwanafunzi anasoma kitabu chake.




zoezi VITENZI VISHIRIKISHI zoezi

Vitenzi sambamba ni vitenzi ambavyo hutokea katika mfululizo. Mfululizo wa aina hii unaweza kuleta pamoja kitenzi kisaidizi au kishirikishi na kitenzi halisi. Uweza pia kuhusisha vitenzi visaidizi kadha na kitenzi kikuu. Kwa mfano
Wanafunzi wanakimbia wakiimba uwanjani
Wanakimbia ni kitenzi kikuu
Wanakimbia ni kitenzi kikuu

Watahiniwa walikuwa wanataka kujiandaa kupita mtihani
Walikuwa ni kitenzi kisaidizi
Wanataka ni kitenzi kisaidizi
Kujiandaa kitenzi kisaidizi
Kupita kitenzi kikuu

Wakulima wangali wanalima
Wangali ni kitenzi kisaidizi
Wanalima ni kitenzi kikuu

zoezi





 

 

 



Yambwa kitondo ni nomino ambayo hutendewa jambo. Huathiriwa na jambo kwa njia isiyo moja kwa moja. Kitondo hunufaika au kupata hasara kutokana na vitendo vya mtenda
.

Kwa mfano,
1. Watoto wametambiwa hadithi na babu.


2.Mwashi amemjengea Farida nyumba nzuri.
3. Kasisi alinipa mawaidha bora.


4. Mpishi amekupikia chai tamu.

Kutokana na mifano hii utaona kuwa viambishi viwakilishi nomino huweza pia kuchukua nafasi ya kitondo.

 

 

Yambwa Ala/Kitumizi
Yambwa ala au kitumizi hurejelea kifaa ambacho hutumika katika kufanikisha tendo. Kile kifaa kinahusika katika kutekeleza kitendo kile.
Kwa mfano,
1. Wanafunzi wanaandika kwa
kalamu ya wino.( ala/ kitumizi )
2. Tulisafiri kwa
gari la moshi. (ala/ kitumizi) 


3. Waimbaji wanaimba kwa tarumbeta.(ala/ kitumizi)


4. Wanafunzi wanasoma kwa miwani.(ala/ kitumizi)


Chagizo(CH)
Chagizo ni sehemu ya sentensi ambayo aghalabu huja baada ya kitenzi au yambwa/shamirisho. Chagizo huwa kielezi au kirai kielezi.Chagizo hutofautishwa na kielezi kwa kuzingatia uamilifu wake katika sentensi.
Kwa mfano;
1. Mkulima anapanda miti
sasa.(chagizo)
2. Mwanafunzi anasoma kitabu
kwa makini.(chagizo)
3. Mtoto anacheza
mpira uwanjani.(chagizo)


4.Mara kwa mara mimi huandikiwa barua kwa kalamu nzuri.
(chagizo)

Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa :


1. kufafanua maana ya yambwa/ shamirisho
2. kubainisha aina za shamirisho
3. kutumia shamirisho ipasavyo katika sentensi.


AINA ZA YAMBWA

Virai Nomino
Katika aina hii ya kirai neno kuu huwa ni nomino au kiwakilishi chake. Nomino huandamana na maneno mengine.
Kwa mfano,
kivumishi, kiunganishi, kielezi na kadhalika.Hata hivyo, kundi hilo lote huwa lina uamilifu wa nomino.

Tazama mifano hii.
1.Mama mpole amefika.
2.Moshi ambao hutoka viwandani ni hatari.
3.Mwanafunzi bora ametuzwa.
4.Baba na mama wamefika.


Kirai Kivumishi

Katika kirai kivumishi neno lake kuu huwa ni kivumishi. Kirai kivumishi hufafanua sifa za nomino au kiwakilishi chake kundi la maneno huweza kuwa na kivumishi na maneno mengine kama vile, kielezi, kiunganishi, kihusishi na kadhalika.

Kwa mfano
1.Mwashi amejenga jumba kubwa sana.
2.Kasisi yule mwanasiasa amewapotosha wananchi.
3.Nguo yangu mpya imepotea.
4.Gari kubwa jeusi la mwalimu limepakwa rangi upya.


CHAGIZO (CH)

Kirai Kielezi
Katika kirai kielezi, neno lake kuu ni kielezi. Kirai kielezi huwa mwandamano wa vielezi.
Kwa mfano;
1.Panya ameingia
shimoni haraka mno.


2.Tutaenda kuchezea uwanjani kasarani kesho alasiri.


3.Utandawazi umeenea vururu kote dunia.

Kirahi Kihusishi
Kirai kihusishi ni kundi la maneno ambalo hufanya kazi ya kihusishi na neno lake kuu ni kihusishi.
Mifano ya sentensi zenye kutumia kirai husishi ni kama vile,
1.Ndege ametua
juu ya mti.
2.Uongozi
wa nchi hii umeimarika sana.
3.Shule yetu iko
karibu na bwawa la sulu.
4.Kijiti
cha mti huo kimevunjika.


Vishazi

Kishazi ni kundi la maneno lenye muundo wa kiima na kiarifa. Kishazi hutokea katika muktadha wa sentensi kuu. Baadhi ya vishazi hujisimamia kimaana hata vikiondolewa kwenye sentensi kuu. Hivi ni vishazi huru .Vile haviwezi kuleta maana vikiondolewa katika sentensi kuu huitwa vishazi tegemezi.

Aina za vishazi

Kuna aina mbili za vishazi.
1. Vishazi huru.


2. Vishazi tegemezi.

Vishazi huru

Hivi ni vishazi ambavyo vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu vitaweza kujisimamia kimaana.

Kwa mfano;


1.  Kengele imelia na wanafunzi na wanafunzi wameingia darasani.
Kengele imelia ni kishazi huru.

Wanafunzi wameingia darasani pia ni kishazi huru.


2. Ukuta uliojengwa umebomoka.
Umebomoka ni kishazi huru.


3.  Mvua imenyesha kwa wingi hivyo wakulima wamevuna mazao mengi.
Wakulima wamevua mazao mengi ni kishazi huru.


4. Ijapokuwa hakunialika, nilitamani sana kuhudhuria arusi yake.
Nilitamani sana kuhudhuria arusi yake ni kishazi huru.
5. Katiba iliyopitishwa itaimarisha maisha ya wananchi.
kishazi huru

Vishazi huru

Hivi ni vishazi ambavyo vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu vitaweza kujisimamia kimaana.

Kwa mfano;


1.  Kengele imelia na wanafunzi na wanafunzi wameingia darasani.
Kengele imelia ni kishazi huru.

Wanafunzi wameingia darasani pia ni kishazi huru.


2. Ukuta uliojengwa umebomoka.
Umebomoka ni kishazi huru.


3.  Mvua imenyesha kwa wingi hivyo wakulima wamevuna mazao mengi.
Wakulima wamevua mazao mengi ni kishazi huru.


4. Ijapokuwa hakunialika, nilitamani sana kuhudhuria arusi yake.
Nilitamani sana kuhudhuria arusi yake ni kishazi huru.
5. Katiba iliyopitishwa itaimarisha maisha ya wananchi.
kishazi huru


Vishazi huru

Hivi ni vishazi ambavyo vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu vitaweza kujisimamia kimaana.

Kwa mfano;
1.Kengele imelia na wanafunzi na wanafunzi wameingia
darasani
.
Kengele imelia ni kishazi huru.
Wanafunzi wameingia darasani pia ni kishazi huru.
2.Ukuta uliojengwa umebomoka.
Umebomoka ni kishazi huru.
3.Mvua imenyesha kwa wingi hivyo wakulima wamevuna mazao mengi.
Wakulima wamevua mazao mengi ni kishazi huru.
4.Ijapokuwa hakunialika, nilitamani sana kuhudhuria arusi yake.
Nilitamani sana kuhudhuria arusi yake ni kishazi huru.
5.Katiba iliyopitishwa itaimarisha maisha ya wananchi.
Inaimarisha maisha ya wanachi ni kishazi huru.


Vishazi Tegemezi
Hivi ni vishazi ambavyo haviwezi kujisimamia kimaana vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu. Vishazi tegemezi huhitaji vishazi vingine ili kuleta maana.
1.
Ungesikia ushauri wa mwalimu ungepita mtihani.
2.
Akimlipia nauli atamletea vitabu hivyo.
3.
Maadam umeniomba msamaha, nimekusamehe na kusahau.
4.
Wananchi wakibadilisha mienendo yao maenezi ya ugonjwa wa
ukimwi yatapungua.
5.
Mwajiri aliyekiuka haki za watoto ameshtakiwa.

Shabaha
Kufikia mwisho wa kipindi hiki,unatarajiwa kuwa na uwezo wa :
1.kufafanua umbo la sentensi sahili, ambatano na
changamano.
2.kuchanganua aina tofauti za sentensi kwa:

 • mtindo wa mchoro wa matawi
 • mtindo wa mistari
 • mtindo wa visanduku

Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa :


1. kufafanua maana ya:
a. virai
b. vishazi
2. kubainisha kirai na kishazi katika sentensi
3. kutaja na kufafanua
a. aina tofauti za virai
b. aina tofauti za vishazi

Uchanganuzi wa Sentensi


Kuchanganua sentensi huhusu kutenga sentensi katika sehemu mbalimbali za kisarufi.

Sentensi yaweza kuchanganuliwa kwa:

 • mtindo wa mchoro wa matawi
 • mtindo wa mistari
 • mtindo wa visanduku

Katika aina hii ya kirai neno kuu huwa ni nomino au kiwakilishi chake. Nomino huandamana na maneno mengine.
Kwa mfano, kivumishi, kiunganishi, kielezi n.k. hata, hivyo, kundi hilo lote huwa lina uamilifu wa nomino.

Tazama mifano hii.

Uchanganuzi wa sentensi sahili
Sentensi sahili huwa na muundo ufuatao:
S-KN+KT

Katika uchanganuzi sehemu ya kikundi nomino na kikundi kitenzi huweza kuchanganuliwa ili kuonyesha vijenzi vya kila kijisehemu.

a) Uchanganuzi wa sentensi sahili kwa mchoro wa matawi.
Utandawazi umeenea duniani
Utandawazi umeenea duniani
Mwanafunzi mwerevu amepita mtihani
Mwanafunzi mwerevu amepita mtihani
Gari lililoharibika limekarabatiwa
Gari lililoharibika limekarabatiwa
Atakupikia wali mtamu.
Atakupikia wali mtamu

b) Mtindo wa mstari

Ufisadi hurudisha nyuma maendeleo.
S_________KN(N) + KT(T+E+N)

Uendeshaji wa magari vibaya husababisha ajali
S________KN(N+H+N+E) + KT(T+N)

Mazingira ni uhai
S______KN(N) + KT(t+N)

c) Mtindo wa visanduku

Mwandishi huyu ameandika riwaya.
Ali amenitumia arafa
Mwanariadha hodari ameshinda nishani


Katika kirai kivumishi neno lake kuu huwa ni kivumishi. Kirai kivumishi hufafanua sifa za nomino au kiwakilishi chake kundi la maneno huweza kuwa na kivumishi na maneno mengine kama vile, kielezi, kiunganishi, kihusishi na kadhalika.

Kwa mfano

Uchanganuzi wa sentensi ambatano

Sentensi ambatano huwa na muundo ufuatao:

 

S_________S + U +S

Uchanganuzi wa sentensi ambatano kwa michoro ya matawi

Mwalimu: Karani unaweza kutukumbusha kirai kihusishi ni nini?

Karani: Kirai kihusishi ni kundi la maneno ambalo hufanya kazi ya kihusishi na
neno lake kuu ni kihusishi.

Mwalimu: Hongera Karani. Nitakupa mifano ya sentensi zenye kutumia kirai
Husishi.

AINA ZA VISHAZI

Kuna aina mbili za vishazi.

VISHAZI HURU Hivi ni vishazi ambavyo haviwezi kujisimamia kimaana vikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu. Vishazi tegemezi huhitaji vishazi vingine ili kuleta maana.

Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatarajiwa kuwa na uwezo wa :

1) kufafanua umbo la sentensi sahili, ambatano na ambatano
2) kuchanganua aina tofauti za sentensi kwa:
i. mtindo wa mchoro wa matawi
ii. mtindo wa mistari
iii. mtindo wa visanduku

Sentensi sahili huwa na muundo ufuatao:

Vitenzi vya asili ya kibantu

Hivi ni vitenzi ambavyo kwa kawaida huishia kwa irabu 'a'. kwa mfano,

soma

cheza

enda

imba

lima


Jedwali hili linaoonyesha mifano ya mnyambuliko wa vitenzi vya asili ya kibantu.


Mnyambuliko wa vitenzi vya asili ya kibantu
Mnyambuliko wa kitenzi ni hali ya kukiongezea kitenzi silabi ili kukipa maana zaidi.
Vitenzi hunyambuliwa katika kauli au jinsi mbali mbali.

Vitenzi vya Asili ya kigeni
Hivi ni vitenzi ambavyo kwa kawaida huishia irabu 'e','i',na 'u'. vitenzi hivi hutokana na lugha za kigeni kama vile kiarabu.
Mifano ya vitenzi vya kigeni ni:.
1. sahau
2. samehe
3. thamini
4. fuzu
5. fariji
6. salimu
7. safiri
8. durusu
9. zuru
10. hukumu


Mfano wa mnyambuliko wa vitenzi vya asili ya kigeni.



Mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja

Hivi ni vitenzi ambavyo huwa na tamko moja au silabi moja.Mara nyingi huongezewa kiambishi ku- ili viweze kutamkika ipasavyo.

mfano

-la huongezewa ku ikawa 'kula'

Mifano zaidi ya vitenzi vya silabi moja.
i) -ja
ii) -pwa
iii) -la
iv) -pa
v) -wa
vi) -chwa
vii) -nywa
viii) -nya
ix) -pwa
x) -fa


Tazama jedwali lifuatalo ili luona mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja.


Hitimisho
Ni matumaini yangu kuwa unaweza sasa kubainisha vitenzi vya asili ya kibantu, vitenzi vya asili ya kigeni na vile vya silabi moja na kuweza kuvinyambua . Sasa jaribu kuvitungia sentensi na kueleza maana ya sentensi hizo.

Kufikia mwisho wa kipindi unatarajiwa kuwa na uwezo wa
i) kubainisha vitenzi vya asili ya kibantu
ii) kutambua vitenzi vya asili ya kigeni
iii) kubainisha vitenzi vya silabi moja
iv) kutambua mzizi na shina la kitenzi
v) kunyambua vitenzi hivi katika kauli mbalimbali








Imedhihirika kuwa vitenzi hivi vinaishia irabu ‘a’.
Isitoshe, vitenzi vilivyoorodheshwa viko katika kauli mbalimbali.

Aghalabu, irabu ‘a’ huambikwa katika mzizi wa kitenzi ili kuunda shina la kitenzi.

Ninafikiri unaweza kutofautisha kati ya mzizi na shina. (P)

Mzizi wa kitenzi ni sehemu ya kitenzi inayobakia baada ya kuondolewa kwa viambishi awali na tamati katika kitenzi hicho. Mizizi ya vitenzi vya asili ya kibantu huwa mizizi funge au ambata.

Uundaji wa nomino
Nomino huweza kuundwa kwa njia tatu, nazo ni:
a) Nomino kutokana na
nomino.
b) Nomino kutokana na
vivumishi.
c) Nomino kutokana na
vitenzi.

Uundaji wa nomino kutokana na mzizi wa nomino

Tazama jedwali lifuatalo;


Sasa tazama mifano katika sentensi zifuatazo.
i.Mtu ni utu.

ii.Mdeni amenilipa deni langu.

iii.Kiwango cha umaskini kinapozidi, idadi ya maskini
huongezeka marudufu.

iv.Daktari alirudi chuoni kupigia msasa ujuzi wake wa udaktari.

 


Uundaji wa nomino kutokana na mzizi wa kitenzi

Hebu tazama jedwali lifuatalo.


Tazama mifano ya sentensi zifuatazo.

a) Nilikula chakula kitamu sana jana.
b) Baada ya kuomba, ombi langu lilijibiwa.
c) Msafiri huyo alisafiri kwa muda wa siku arobaini.
d) Rudisha aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wanariadha
wengine wote.

Uundaji wa nomino kutokana na mzizi wa kivumishi.

Tazama jedwali lifuatalo.


Sasa tazama mifano katika sentensi.

a)Umoja wao uliwafanya kuwa kitu kimoja hasa.

b)Jumba hilo likuwa chafu sana, lilijaa uchafu wa kila aina.

c)Yeye ni mwerevu kwelikweli, aliweza kutudhibitishia werevu wake kupitia mtihani huo.

d)Bidhaa bora hutegemea ubora wa malighafi.


Uundaji wa vitenzi.

Vitenzi huweza kuundwa kutokana na aina nyingine za maneno kama vile nomino na vivumishi.

Uundaji wa vitenzi kutokana na mizizi ya nomino

Hebu tazama jedwali lifuatalo.


Sasa soma sentensi zifuatazo ili kuelewa zaidi.

a)Maana ilieleweka alipoeleza vyema alichomaanisha kutumia msemo huo.

b)Wanasayansi wanaendelea kutafuta tiba ili waweze kutibu ugonjwa wa ukimwi.

c)Ni muhimu kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa elimu.

d)Alisababisha maafa, sababu zake zikiwa kujinufaisha mwenyewe.

e)Mali aliyoibia taifa letu, ilitaifishwa.


Uundaji wa vitenzi kutokana na mizizi ya vivumishi.

Tazama jedwali lifuatalo.

Highlight the words under the three sections below.

Kivumishi

mzizi

kitenzi kilichoundwa

Fupi

fupi-

fupisha

Bora

bor-

boresha

Sanifu

sanif-

sanifisha

Chafu

chafu-

chafua

Kamili

kamili-

kamilisha

Sasa soma sentensi zifuatazo ili upate kuelewa zaidi.

Meza fupi ilifupishwa zaidi na seremala.

Chakula bora huboresha afya.

Lugha sanifu ya Kiswahili iltokana na kusanifishwa kwa lahaja ya kiunguja.

Watu wengi huchafua mazingira kwa kutupa vitu vichafu ovyo ovyo.

Mwalimu alimuamuru mwanafunzi kukamilisha insha yake alipowasilisha insha isiyokuwa kamili.


Uundaji wa vitenzi kutokana na mizizi ya vivumishi.

Tazama jedwali lifuatalo.


Sasa soma sentensi zifuatazo ili upate kuelewa zaidi.

a) Meza fupi ilifupishwa zaidi na seremala.
b) Chakula bora huboresha afya.
c) Lugha sanifu ya Kiswahili iltokana na kusanifishwa kwa
lahaja ya kiunguja.
d) Watu wengi huchafua mazingira kwa kutupa vitu vichafu
ovyo ovyo.
e) Alikamilisha maandishi yake yakawa taarifa kamili.


Uundaji wa vivumishi

Vivumishi huweza kuundwa kwa kutumia maneno mengine kama vile nomino na vitenzi.

Uundaji wa vivumishi kutokana na mizizi ya nomino

Tazama jedwali hili.


Sasa tazama mifano ifuatayo ya sentensi.
a) Mtu huyo mwerevu alijitajirisha kwa kutumia werevu wake.
b) Wahusika wajinga hutumiwa katika fasihi ili kuonyesha
ujinga
miongoni mwa watu.
c) Wembamba wake ulimwezesha kuivaa nguo hiyo
nyembamba
.


Uundaji wa vivumishi kutokana na mizizi ya vitenzi.




Sasa angalia mifano ifuatayo ya sentensi.
a)Ingawa mzee yule mlemavu amelemaa miguu yote, anajitahidi kutembea kwa mkongojo.
b)Nilikutana na mtu mtulivu sana, alikuwa ametulia kama maji ya mtungi.
c)Usipopoa hutaweza kuwa mpole kwa watu wengine.
d)Msichana huyu mnyamavu alinyamaza tu kimya bila kujitetea.



Kufikia mwisho wa kipindi,untarajiwa kuweza:

i) Kutambua aina tofauti tofauti za maneno.
ii) Kuunda aina mbalimbali za maneno kutokana na maneno mengine.
iii) Kuyatumia maneno hayo katika sentensi.

Lugha huwezesha uundaji wa maneno mapya kwa njia mbalimbali. Njia mojawapo ni uundaji wa maneno kutokana na yale yaliyopo. Kwa mfano: nomino kutokana na nomino, vitenzi kutokana na nomino na nomino kutokana na vivumishi.

Nomino huweza kuundwa kwa njia tatu, nazo ni:

a) Nomino kutokana na nomino
b) Nomino kutokana na vivumishi
c) Nomino kutokana na vitenzi

Uundaji wa nomino kutokana na mzizi wa nomino



2. Hutumiwa kama kiwakilishi cha nafsi ya pili umoja (wewe)

Mifano katika sentensi.
a) Nitakusomea riwaya ya Utengano.
b) Mwalimu anakuita.
c) Watakutumbuiza ukiwaruhusu.


3. Hutumiwa kama kiwakilishi cha mahali. Kwa mfano,
a) Kuliko na fujo kuna wasiwasi.
b) Kwenye miti kuna wajenzi.
c) Wanafunzi wataimbia huku.

Kiambishi NDI-

ndi- hutumiwa kwa namna mbili.

a) Pamoja na kitenzi kishirikishi kipungufu kwa mtindo wa kufupisha.

b) Hutumiwa kuonyesha msisitizo.Msisitizo huu hurejelea kiima yaani kinachozungumziwa. Ili kuonyesha kurejelea huku lazima pawepo na upatanisho wa kisarufi. Kwa mfano,

Ndisi(ni sisi)
Ndiwe (ni wewe)
Ndiye (ni yeye)
Ndio(ndio wao)

 

Kiambishi-JI-

Kiambishi ji- hutumiwa kwa namna zifuatazo.

a) Kama kiambishi cha ngeli ya li-. Kwa mfano:
i) jino
ii) jiko
iii) jipu
i) Jino linalouma litang'olewa.
ii) Jiko hilo lilichukuliwa na mwenyewe.
b) Kuonyesha ukubwa wa nomino. Kwa mfano.
i) Jitu hilo liliwahangaisha wanakijiji.
ii) Jitu hili latisha mno.

c) Kuonyesha dharau. Kwa mfano.
i) jiatu
ii) jivulana
iii) jizee

i) Jivulana lile ni jisumbufu sana.
ii) Jizee hilo linashikilia utamaduni uliopitwa na wakati.


d) Kama kiambishi cha urejeshi katika vitenzi katika nafsi zote tatu. Kwa mfano:
a) Nilijikata
b) Ulijikosea
c) Alijitia hatarini
i) Nilijitia matatani kwa kutofika mapema.
ii) Alijikosea kwa kutofuata maagizo aliyopewa.


e) Huambishwa mwishoni mwa kitenzi kuunda nomino ili kuonyesha mtu anayetenda kitendo fulani.
Mifano katika sentensi
a) Mlimaji huyo alipata mavuno mengi.
b) Msemaji yule alielewa kwa urahisi.

Vitenzi huweza kuundwa kutokana na aina nyingine za maneno kama vile nomino na vivumishi.

Uundaji wa vitenzi kutokana na mizizi ya nomino

Kwa

1)Neno kwa hutumiwa kuonyesha mahali.

a) Nitakula chamcha kwa Ahmed.
b) Mkutano utakuwa kwa Nyaga.
c) Walipofika kwa nyanya walishangazwa na jinsi
walivyopokelewa kwa mikono miwili.

2)Neno kwa hutumiwa kuonyesha sehemu ya kitu kizima.
a) Wanafunzi ishirini kwa hamsini wanajizatiti.
b) Atieno alipata themanini kwa mia katika somo la Kiswahili.

3)Huonyesha jinsi kitendo kilivyofanyika.
a) Walisherehekea arusi hiyo kwa furaha.
b) Uchaguzi huo ulimalizika kwa amani.

4)Hutumiwa pamoja na vivumishi vimilikishi kuonyesha
umilikaji
.

a) Kule kwao kunaogofya.
b) Kuimba kwake kuliwafurahisha.


5)Huonyesha dhana ya 'pamoja na'

a) Napenda kula wali kwa mchuzi wa samaki.
b) Mkutano huo ulihudhuriwa na wazee kwa vijana.

6)Huonyesha kitu fulani kilitumiwa kufanya jambo fulani.

a)Aliambua mhogo kwa kisu.
b) Alichanja kuni kwa shoka.

7)Huonyesha kusudi, nia au sababu.
a)Waliadhibiwa kwa uovu walioutenda.
b) Alimwendea nyanya kwa kutaka kumjulia hali.

Ila

Neno ila ni kiunganishi kinacholeta dhana ya kinyume. Pia hutumuka kuleta maana ya isipokuwa.

Kwa mfano


1.Alipopatwa na msiba jamaa zake walimtoroka ila rafikize.


2. Alijaribu kumshawishi katika swala hilo ila hakukubali.


3.Anab alitarajiwa mkutanoni ila hakufika.


Vivumishi huweza kuundwa kwa kutumia maneno mengine kama vile nomino na vitenzi.

Uundaji wa vivumishi kutokana na mizizi ya nomino




Labda
Huonyesha shaka au kutokua na uhakika nao.
a) Labda sitampata kwake nyumbani.
b) Najihisi kichefuchefu labda nina malaria.
c) Sijui viliko vijiko labda tumwulize mama.

Na

A) Hutumiwa kama kiambishi cha wakati uliopo hali ya kuendelea. Kwa mfano:

a) Fatuma anasoma riwaya ya utengano.
b) Wabunge wanajadili bungeni.
c) Daktari anatibu mgonjwa.

B) Hutumiwa kama mzizi wa kitenzi cha kuonyesha hali ya kumiliki au kuwa na.

a) Mzee juma ana wajukuu wane.
b) Shamba hili lina magugu mengi.
c) Nguo hii ina madoadoa mengi.

C) Hutumiwa kama kihusishi kuonyesha mtenda/kitenda.

a) Unaitwa na mwalimu.
b) Mtoto alinyweshwa maziwa na Yaya.
c) Katiba hiyo ilipendekezwa na wananachi.
D) Hutumiwa kama kiunganishi kuleta maana ya'pamoja na'

a) Mwimbaji yule alivaa tai na kofia.
b) Mama alinunua mafuta, sabuni na rangi ya viatu.

Order this CD Today to Experience the Full Multimedia State of the Art Technology!

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the Sample e-Content link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Sample Coursework e-Content CD

Other Goodies for KCSE ONLINE Members!

Coursework e-Content CD covers all the topics for a particular class per year and costs 1200/- ( Per Subject per Class ).

Purchase Online and have the CD sent to your nearest Parcel Service. Pay the amount to Patrick 0721806317 by M-PESA then provide your address for delivery of the Parcel. Alternatively, you can use BUY GOODS TILL NUMBER 827208 Ask for clarification if you get stuck.

Install ADOBE Flash Player for Best Results

For Best results INSTALL Adobe Flash Player Version 16 to play the interactive content in your computer. Test the link below to find out if you have Adobe Flash in your computer.

Search

Subject Menu